Tume ya Uchaguzi yatofautiana Mbeya kuhusu CHADEMA

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Lewis Makame ametofautiana na Msimamizi wa Uchaguzi, Malange kuhusu CHADEMA na Operesheni Sangara Mbeya.

Wakati Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amenukuliwa na gazeti la Mwananchi(5/1/2009), Msimamizi wa uchaguzi ameandikia barua CHADEMA ya tarehe hiyo hiyo kupiga marufuku Operesheni Sangara katika jimbo hilo hilo la Mbeya Vijijini.

Hayo yako katika barua tuliyotumiwa hivi punde kwa faksi kwenye chumba chetu cha habari toka Mbeya Vijijini. Katika barua hiyo, msimamizi ametoa maelezo nyeti yanayopingana na kauli ya Makame

Habari zaidi soma gazeti letu siku ya kesho.


PM
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Lewis Makame ametofautiana na Msimamizi wa Uchaguzi, Malange kuhusu CHADEMA na Operesheni Sangara Mbeya.

Wakati Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amenukuliwa na gazeti la Mwananchi(5/1/2009), Msimamizi wa uchaguzi ameandikia barua CHADEMA ya tarehe hiyo hiyo kupiga marufuku Operesheni Sangara katika jimbo hilo hilo la Mbeya Vijijini.

Hayo yako katika barua tuliyotumiwa hivi punde kwa faksi kwenye chumba chetu cha habari toka Mbeya Vijijini. Katika barua hiyo, msimamizi ametoa maelezo nyeti yanayopingana na kauli ya Makame

Habari zaidi soma gazeti letu siku ya kesho.


PM


Operesheni Sangara marufuku Mbeya

Merali Chawe, Mbeya
Daily News; Tuesday,January 06, 2009 @00:02


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepigwa marufuku kuendelea na Operesheni Sangara katika Jimbo la Mbeya Vijijini, licha ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kukiruhusu kuendelea na kampeni hizo mkoani Mbeya.

Msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Juliana Marange, alisema chama hicho hakitaruhusiwa kuendelea na operesheni hiyo katika jimbo hilo ili kutoathiri kampeni za vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Alisema taratibu za uchaguzi haziruhusu chama kisichoshiriki uchaguzi kufanya kampeni kipindi cha uchaguzi, hivyo Chadema itaruhusiwa kuendelea na Operesheni Sangara baada ya uchaguzi huo wa Januari 25, mwaka huu.

Chadema imekuwa ikiendesha Operesheni Sangara kwa nia ya kueleza mambo mbalimbali kwa wananchi kuhusu serikali iliyopo madarakani, hasa baada ya kushinda kiti cha ubunge cha Tarime, Oktoba mwaka jana.

Chadema ilienguliwa kuwania kiti cha Mbeya Vijijini kilicho wazi kutokana na kifo cha mbunge Richard Nyaulawa aliyefariki dunia Novemba mwaka jana, baada ya mgombea wake kukiuka masharti ya sheria ya uchaguzi, ikiwamo kiapo chake kusainiwa na wakili, kinyume cha sheria inayotaka kipate baraka kutoka kwa hakimu.

Baada ya Chadema kuenguliwa wiki iliyopita kutokana na rufaa ya mgombea wake, Shimwee Shitambala kutupwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kinyang’anyiro hicho kimebakia kwa vyama vitatu. Vyama hivyo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha Sauti ya Umma (SAU).

Wakati huo huo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Tambwe Hizza, amewataka wananchi wa Jimbo la Mbeya Vijijini kutoichagua CUF kwa kuwa ni chama cha kibaguzi na kinatoa ajira kwa watu wa Pemba pekee, huku Watanzania wengine wakikosa nafasi za ajira katika chama hicho.

Tambwe aliyasema hayo wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM, Mchungaji Lackson Mwanjale zilizofanyika katika Kata ya Santilia na kusema wananchi wanatakiwa wawahoji viongozi wa CUF ni kwanini chama hicho kimekuwa kikitoa ajira kwa Wapemba tu.

Pia alitaka wananchi wawahoji viongozi hao ni kwa namna gani watapigania haki za wananchi ikiwa kimeshindwa katika hilo la ajira ndani ya chama chao. Kadhalika aliwaonya wananchi kutoshiriki katika vitendo viovu zikiwamo vurugu zinazochochewa na chama hicho na kusema wasipoangalia, wataishia pabaya kwa kukamatwa na kufungwa na hivyo kushindwa kutekeleza haki yao ya kupiga kura siku ya uchaguzi.

“Vyama vya upinzani vimejiwekea utaratibu wa kutamka kwa hasira kuwa miaka orobaini ya CCM haijafanya kitu cha maana huku wakitembea katika barabara zilizojengwa na Serikali ya CCM, watoto wao wanasoma shule za Serikali ya CCM,” alisema na kuongeza kuwa CCM inatekeleza kwa vitendo Ilani yake katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Alisema wananchi wanatakiwa kuelewa kuwa vyama vya upinzani havina hoja ya msingi na badala yake vimekuwa vikibambikiza tuhuma dhidi ya chama na serikali huku viongozi wake wakielewa fika kwamba CCM imetekeleza Ilani ya Uchaguzi katika sekta mbalimbali zikiwamo elimu, afya na miundombinu.
 
Back
Top Bottom