Tume ya Uchaguzi yakanusha vikali kuwepo vituo hewa 55 vya kupigia kura Arumeru.

1.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC)Jaji Mkuu mstaafu Bw. Damiani Lubuva akiongea na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa mikutano wa tume hiyo jijini Dar es salaam, kuhusiana na uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru mashariki kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu uchaguzi huo, ambapo jaji lubuva amekanusha vikali tuhuma za kuongeza vituo bandia zilizotolewa na chama cha (CHADEMA) Katika picha ulia Mkurugenzi wa tume ya uchakuzi Bw. Julias Mallaba, Kushoto Jaji mkuu mstaafu Zanzibar Makamu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Bw. Hamio Mahmoud Hamio.

2.jpg

Jaji John Joseph Mkwawa Kamishina wa tume (NEC)akifafanu jambo katika mkutano huo.kulia jaji Mary h.C.S Longway kamishina wa tume.


3.jpg

Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo


Kurunzi 07:23 Today
ituo bandia
Wakati hayo yakiendelea, tuhuma kwamba kuna
vituo 55 vya bandia vilivyoandaliwa kwa lengo
la kutumika kuiba kura kwenye uchaguzi huo,
zinaonekana kugonganisha vichwa vya maofisa
wa uchaguzi.
Tuhuma hizo ni zile zilizotolewa na Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa juzi
kwamba kuna vituo 55 bandia 55 vya kupigia
kura katika uchaguzi huo mdogo madai ambayo
yalikanushwa na Msimamzi wa Uchaguzi wa
Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi.
Juzi Kagenzi alipozungumza na waandishi wa
habari alisema vituo halali ambavyo
anavitambua ni 327 tu na hakukuwa na kituo
ambacho kimeongezwa na kwamba hata kama
ikitokea hivyo, itakuwa ni baada ya majadiliano
na vyama vyote shiriki.
“Vituo vilivyopo ni 327 pekee, na kama ikitokea
kituo kinakuwa na watu zaidi ya 500 ndipo
kunaweza kuongezeka, lakini historia
inajionesha kila uchaguzi mdogo unapofanyika
idadi ya wapigakura inapungua,”alisema
Kagenzi.
Lakini jana Kagenzi alikiri kuwapo kwa kasoro
kwenye orodha ya vituo hivyo na kwamba
alikuwa anawasiliana na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), ili kuwezesha kufanyika kwa
marekebisho.
Maeleo ya Kagenzi yanatokana na ushahidi
ambao gazeti hili liliupata kwa kuona orodha ya
vituo hivyo, ambayo ilikuwa ikionyesha
takwimu mbili tofauti za idadi ya vituo vya
kupigia kura.
Katika orodha hiyo, safu ya idadi ya vituo vya
kupigia kura katika kata 17 za jimbo hilo ilikuwa
ikionyesha vituo 327, wakati safu ya mwisho ya
orodha hiyo hiyo ilikuwa ikionyesha kuwapo
kwa jumla ya vituo 382, likiwa ni ongezeko la
vituo 55.
Waraka wa orodha hiyo unaonyesha kuwa katika
Kata ya Akheri kutakuwa na vituo 20 idadi
ambayo inayofautiana na iliyotolewa na tume
ambavyo ni vituo 18.
Kata nyingine ambazo vituo hivyo vinaonekana
kuongezwa ni Kikatiti vituo 22 badala ya 18,
Kata ya Kikwe vituo 12 badala ya halali 11, Kata
ya Kingori vituo 29 badala ya halali 26 na Kata
ya Leguruki vituo 23 badala ya halali 20.
Kata nyingine ni Makiba vituo 21 badla ya halali
18, Majiya chai 24 badala ya 29 halali, Maroroni
vituo 21 badala ya 17 halali, Mbuguni vituo 25
badala ya halali 21,Nkoarsambu vituo 10 badala
ya 8 vinavyohitajika na Kata ya Ngarenanyuki
ambako vimeongezwa vituo sita kutoka halali
20 hadi 26.
Orodha hiyo ambayo Kagenzi alithibitisha
kwamba ilikuwa na makosa pia ina kasoro
katika Kata za Nkoaranga ambako vituo
vimeongezwa kutoka halali 17 hadi 22, Pori
kutoka vituo halali 16 hadi 20, Nkwandua
kutoka vituo 22 hadi kufikia 25 na Kata ya Seela
- Sing’isi vituo hivyo viliongezwa kutoka halali
12 hadi 15.
Kata nyingine ni Songoro nyumbani kwa
Mgombea wa Chadema, Joshua Nassari vipo
vituo 15 na hakuna kilichoongezeka huku Kata
ya Usa River ilikuwa na vituo 36, lakini
vimeongezeka vitano na kufikia 41.
Kagenzi alisema alipowasiliana na idara ya
teknolojia ya habari ya NEC kuhusu kasoro hizo
walimwambia kwamba orodha ya awali haikuwa
toleo la mwisho na kwamba wangefanya
marekebisho ya kuondoa kasoro hizo.
“Wameniambia kwamba hiyo orodha ilikuwa ni
working draft tu (rasimu ya kufanyiwa kazi),
kwahiyo nimeomba hiyo orodha kamili ya
mwisho, wakishanitumia nitaisambaza kwa
vyama husika,”alisema Kagenzi jana.
Baadaye msimamizi huyo wa uchaguzi alisema
wataalamu kutoka NEC walitarajiwa kuwasili
Arumeru jana mchana kwa ajili ya kurekebisha
kasoro hizo pamoja na kufanya maandalizi
mengine kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo.
Hata hivyo, kauli ya Kagenzi ilikuwa ikipishana
na ile iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Julius Mallaba ambaye awali alisema hakukuwa
na vituo vya nyongeza kama ilivyodaiwa na Dk
Slaa.
Baada ya kuelezwa kuhusu orodha hiyo ya
tume, Mallaba alisema: “Basi kama iko hivyo
nitawasiliana na wahusika ili tuone hatua
waliyofikia katika kurekebisha kasoro hizo”.
Dk Slaa alisema hali kama hii waliibaini katika
Jimbo la Igunga mara baada ya matokeo
kutangazwa na baada ya kufuatilia walikuta
vituo hewa ambapo vilikuwa na kura kati ya 160
na 280.
 
Kama ni jimbo moja tu wameongeza vituo hewa 55, je Uchaguzi Mkuu wa 2010 waliongeza vituo hewa vingapi!

Halafu Tume ihakikishe karatasi na fomu zote zinazotumika kwenye Uchaguzi zinakuepo za kuosha .
 
Siku ya Uchaguzi ikifika saa nne tu unashangaa fomu sijui namba ngapi zimeisha, watu wanakatishwa tamaa ya kupiga kura mpaka fomu nyingine zije.
NEC hatutaki kusikia habari ya Fomu kuisha, kwani hamjui idadi ya wapiga kura.
 
NEC ni ovyo kabisa...Kumbe kweli CDM ilishinda Igunga?..Nimeona jana mi afisa ya NEC kibao na mitumbo mikubwa ikikanusha habari za ongezeko la vituo hewa huko Arumeru ni kadhani ni kweli...Sasa hivi tena imekuwa ilikuwa ni draft working...Ina maana mnafanyakazi bila takwimu?...Si ndiyo nyie wenyewe mliutangazia umma kuwa takwimu zitakazotumika ni zile za 2010 au?...
 
ahsante sana dr. Slaa, katibu wangu na rais wangu! Kama walimuua baba wa taifa, they can do anything.
 
Hii Inakuwa Aibu sana kwa Taifa Linalohubiri demokrasia na Haki!! Ila Nadhan Yana Mwisho!! Lubuva Tenda Haki Hata Ukifa Watu Watakukukumbuka!! Usije Ukaaribu Uadilifu wako Uzeeni na Ukalaaniwa kwa Damu Yoyote Itakayomwagika kwa wewe kutotenda Haki!!
 
NEC ni ovyo kabisa...Kumbe kweli CDM ilishinda Igunga?..Nimeona jana mi afisa ya NEC kibao na mitumbo mikubwa ikikanusha habari za ongezeko la vituo hewa huko Arumeru ni kadhani ni kweli...Sasa hivi tena imekuwa ilikuwa ni draft working...Ina maana mnafanyakazi bila takwimu?...Si ndiyo nyie wenyewe mliutangazia umma kuwa takwimu zitakazotumika ni zile za 2010 au?...
Hii Ni aibu Unapomuona Msomi na Mtaalamu anakataa Takwimu zake mwenyewe!! Ila tumwombe Mungu ndio Tulikofikia Hapa!!
 
Lowassa na NEC ni wajinga sana. Akili zao zinawaza madaraka tu, ndiyo maana marehemu Nyerere hakutaka huyu mtu ashike madaraka.

Kwa tamaa za mkwe wake kushika madaraka anataka kunyang'anya haki ya msingi ya wanachi ambao ni wazi ni kauli ya Mungu.
 
NEC ni ovyo kabisa...Kumbe kweli CDM ilishinda Igunga?..Nimeona jana mi afisa ya NEC kibao na mitumbo mikubwa ikikanusha habari za ongezeko la vituo hewa huko Arumeru ni kadhani ni kweli...Sasa hivi tena imekuwa ilikuwa ni draft working...Ina maana mnafanyakazi bila takwimu?...Si ndiyo nyie wenyewe mliutangazia umma kuwa takwimu zitakazotumika ni zile za 2010 au?...
punguza ukali wa maneno mkuu,tuna hasira na wadudu hawa yatupasa tuwashinde kwa hoja na data sio ma****
 
Hapo cha msingi CDM wachukue sample ya kata sita then waende na watu wa NEC wakahakiki hivy vituo na wananchi wa kata hyo wavitaje vituo vyote hili viakikiwe!
 
Painful...kweli sifa mojawapo ya kuwa ccm ni kutomwogopa Mungu,kuwa mwizi,muuaji na muongo...ipo cku!!!
 
Sana JF takwimu iliyotolewa ni kweli isije magamba wanakosoa kila kitu kisemwacho na upinzani ni uongo kutimiza nia yao ya kubaka demokrasia. Nashanga mzee Lubuva kubisha na kumshambulia Dr. Slaa bila kuwasiliana na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo. Anatakiwa awe neutral badala ya kubeba chama cha magamba japo Ndiyo iliyomwajiri.
 
Na hapa msimamizi anakubalina na tofauti za idadi ya vituo na kuahidi kufanyia Kazi. Nashangaa mkurugenzi wa uchaguzi kusema iliyotolewa ni "working document" maana yake "draft" inatia wasiwasi kwa time outlaw draft wakati vyama kazini na hiyo document iliyokamilika watatoa lini wakati huu ni uchaguzi. Hii inaonyesha tume inafanya Kazi wakati uchaguzi muda mwingine wanalala na kula fedha walipa kodi wa nchi Hii bila sababu yoyote.
 
Leo ajabu ujaweka My Take...Chadema tumeishawazoe kwa kulalamika bila ushahidi wowote, mara nyingi uwa wanaanza kulalamika kipindi cha kampeni, kama mtakumbuka Slaa, alishawahi kusema kuna kontena la futi 20 limekamatwa Tunduma limejaa karatasi za kupigia kura, Polisi walipolifungua wakakuta vipodozi.
hiyo kesi ya kontena Tunduma ilishatolewa hukumu,I doubt hujaiona nakala ya hiyo hukumu otherwise wewe ni Vuvuzela hujui unachoongea. Wenye akili zetu tushajua what was up. Nyie mlio bado kwenye blanket la u-chama mmelala usingizi ndio mnaoliangamiza taifa hili.
 
Hapa tume ya ccm iko kazini tayari kufanya uchakachuzi. Hongera Dr. Slaa kwa kusimamia ukweli na kuwaumbua hawa wapuuzi wa tume ya uchaguzi. Wanakataa hata taarifa walizoziandaa wenyewe? What a shame.

hewa,hewa,hewa hakuna ujanja lazima cdm washinde!!
 
Kwa vile hakuna uandikishaji wa wapiga kura wapya nini sababu ya kuongeza vituo?, wasikibali kuongezwa kituo chochote
 
Leo ajabu ujaweka My Take...Chadema tumeishawazoe kwa kulalamika bila ushahidi wowote, mara nyingi uwa wanaanza kulalamika kipindi cha kampeni, kama mtakumbuka Slaa, alishawahi kusema kuna kontena la futi 20 limekamatwa Tunduma limejaa karatasi za kupigia kura, Polisi walipolifungua wakakuta vipodozi.

Maranyingine nilikuwa nakuamini kuwa upo fair, kumbe nawewe ni mpiga propaganda tu. Unajua haya uliyotapika hapa yanadhiirisha ni kweli kwani hao watu wa tume wenyewe wamekubali kuwa wameongeza vituo ingawa wanajifanya kimakosa. Inashangaza kazi ya jimbo moja tu wanajifanya wamefanya makosa na kuita DRAFT, lakini chakushangaza zaidi makosa yenyewe ni kwenye kuongeza tu kasoro jimbo la mgombea wa upinzani ndiyo takwimu zipo sawa. Inawezekana kama Dr. Slaa angekaa kimya, hivyo vituo hewa vingekuja na kura kama ilivyotokea Igunga, sasa naamini hata IGUNGA ushindi uliporwa. Mara nyingi mmekuwa mnasema kwamba Dr. Slaa ni mchochezi wa vurugu, je haya hamyaoni ndiyo yanayosababisha vurugu?? Msifanya wapinzani waonekane ******* nyaji, kwani upinzani ni changamoto ya kusukuma maendeleo ingawa Tanzania ni uadui. Hata hao wapinzani wakishika nchi na kuwa watawala, na wao watakuwa na wapinzani. Msipandikize chuki kwa watu wanaoitwa wapinzani, kama nchi inaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, basi tufate taratibu/demokrasia halisi.
 
CCM kila tawi wanaloshika linateleza, kama Slaa alivyosema vituo hewa huwa na kura kati ya (160-280), kwa hiyo CCM walitegemea hivyo vituo vitaongeza kati ya kura 55 x 160 =8,800 na 55 x 280 = 15,400. Hiyo mbinu imekwama sasa tegemeo lililobaki kwa CCM ni kutumia ubabe kama ule wa Segerea wa kukimbia na masanduku ya kura.

Halafu CCM yalivyo majinga eti kata ya Songoro anayotoka Nassari hawakuongeza hata kituo kimoja, hayajui hata kuiba.
 
Lowassa na NEC ni wajinga sana. Akili zao zinawaza madaraka tu, ndiyo maana marehemu Nyerere hakutaka huyu mtu ashike madaraka.

Kwa tamaa za mkwe wake kushika madaraka anataka kunyang'anya haki ya msingi ya wanachi ambao ni wazi ni kauli ya Mungu.
Hapa Lowassa ameingiaje tena mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Ukiona mtu kama MH .Jaji Lubuva aliyetumikia nchi hii kwa uaminifu anageuka na kuwa jiwe la chumvi ,kwa kujiingiza kwenye wizi ili kumsaidia mkwe wa shemeji na dada yake ujue mfumo mzima wa sheria na haki umebakwa na majambazi wezi wauaji wa CCM na serikali yake inatubidi sisi wenyewe watanzania kutafuta haki yetu kwa namna yeyoteWorking draft haiwezi ikaangalia eneo analotoka mgombeya wa CDM ndio kituo hewa kisiongezwe,Naomba Chadema waendelee kuwashitaki TuME na serikali yake kwa wananchi kwamba waliongeza vituo hewa 55 ili kumbemba Siyoi wajulishwe jinsi hatua hiyo ilivyoweza kupoka ushindi Igunga na wawaase kuwa walinzi wa kura zao na kujitokeza kwa wingi kupiga kura
 
Back
Top Bottom