Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania.......!!??

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Matatizo ya Tume ya Taifa ya uchaguzi Tanzania ni makubwa sana.

Misuguano iliyopo katika uongozi, serikali lege lege yote hayo yanatokana na tume ya uchaguzi.

Udhaifu wa Tume ya uchaguzi ndo chanzo cha madai ya katiba mpya.

Hawa viongozi wa Tume ya uchaguzi wangetakiwa wawe ngangari na wasitumiwe na watawala. Na kama wangekataa kutumiwa kama tissue paper, wakafichua vitisho na wakajiuzulu wangelindwa na Umma.

Wabunge vibogoyo wanaotetea serikali ovu wamepatikana kwa kuchakachua.....

Rais ambaye hajali maslahi ya watanzania atakuwa ametokana na Tume legelege. Hajachaguliwa na wananchi, ndo maana hawajali wananchi.

Tume za uchaguzi zinaleta vita, Example Kenya, Ivory coast.

Afadhali hata ya Ivori coast maana hata matokeo yalijulikana.

Viongozi walio wengi wanaopatikana na Tune ya uchaguzi ya Tanzania hawajali masilahi ya watanzania.

Watanzania sasa, tuanze kupiga kelele na hii tume ya uchaguzi ya Tanzania.

Mwaka jana 2010 wameharibu uchaguzi, mwaka huu wameharibu Igunga. Bado tu tumenyamaza.

Tuwapigie kelele, tuandamane. Tuwanyime usingizi hawa tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi wajiuzulu wote.

Ingetakiwa mwaka jana tungepiga maandamano mpaka tume ya uchaguzi wangejiuzulu
 
Mahakama kuu au Mahakama ya Rufaa nayo ihusike katika kuverify matokeo
 
Hii inatokana na TLS kupanga kufungua kesi mahakamani.

Ni kweli hii sheria ni mbovu, na haitatoa katiba tunayoitaka. Kwa hiyo ni bora hiyo sheria aliyosaini JK ikazuiwa na tuache mambo ya katiba kwanza,

Au Baraza huru liundwe ili lishughulikie katiba na sio hawa magamba

madai ya katiba yametokana na uchaguzi wa mwaka jana kuvurugwa - Tume ya uchaguzi ni dhaifu na haiko huru.

Hata uchaguzi wa Igunga tumeona
 
Back
Top Bottom