Tume ya PM Pinda na madaktari hali si shwari

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Nyepesi nyepesi nilizozipata kutoka kwenye vyanzo aminifu ni kwamba hali si shwari hata kidogo kati ya Tume aliyoiunda mheshimiwa Bw.Mizengo pinda ya kushughulikia mgogoro wa madaktari ambayo inatakiwa iwe imemaliza kazi kabla ya 3/3/2012

-Serikali imecheza siasa kujaribu kuwagombanisha/kuwachangaya pande mbili za madaktari i.e. kamati ya Ulimboka na kwa upande mwingine viongozi wa MAT na inaelekea kufanikiwa kwani kuna mgogoro unaofukuta chini kwa chini ili kuvunja umoja huu.
-Sasa ninavyoongea ni kwamba hata MAT wenyewe kwa wenyewe hawaelewani kwani kuna kiongozi mmoja wa ngazi ya juu amefikia hata hatua ya kutishia kuachia ngazi.
-Tume ya Ulimboka wameamua kujiweka pembeni kwa sasa, na wanasubiri tu ifike hiyo tarehe 3/3, kama bado hakieleweki waitishe tena mgomo.
-MAT wanaonekana wamekuwa'fixed kwani wamekuwa legelege sana kimsimamo

MY TAKE: Madaktari wako imara sana, huo mchezo mchafu hautafanikiwa kamwe, naona Serikali wanasahau haraka sana kile
kilichotokea wiki 2 zilizopita..Hili halipaswi kutokea tena mbele ya macho yetu wananchi..CHONDE CHONDE BWANA
PINDA KUWA MAKINI!!!!
 
isee hiyo si itakuwa ndo WMD nyingine, chonde chonde madaktari twafaaaaaaaaaa!
 
Pinda and his advisers should understand that its no longer political like past years!!!! we subiri tu
 
Chonde chonde pinda tatua tatizo hilo wataalamu wenzangu wa TISS mfikishieni ujumbe pinda haraka
 
Ni mbaya tena sana pale serikali inapofanyia mzaha maisha ya wananchi,hivi hii serikali ni nini wana take serious au emergency kufa kwa kiongozi au ni nini?maana wananchi kufa sio issue,hivi kweli serikali ye2 kama kusoma haiwezi hata picha haioni,au viongozi hamna tv,wenzenu hamuoni wanafanyaje?
 
Ndumila huwa hawakosekani ktk jamii yoyote. Na mwogope msomi akiwa ndumila,mtu wa fitina na majungu!
 
hata mimi nimesikia kwamba badala ya hiyo kamati ya pinda kutatua chanzo cha mgogoro,inaelekea inataka kuingiza siasa kwenye suala hili.inavyoelekea kikao kati ya serikali na madaktari au wateule wa madaktari hakijafanyika mpaka leo.ina maana hakuna negotiation kati ya madaktari na serikali badala yake kamati ya pinda imejifungia ndani na kula perdiems halafu baadae itoke na mapendekezo ......huu mgogoro utaiingiza nchi pabaya tuwe serious.
 
Naamini madakitari ni watu makini hawata naswa na mitego ya kitoto ya kilazaa Pinda na serikali yake ya magamba
 
Sisi move lote tunaliona wee waache wafanye hesabu zao zote, watkuja tutakutana tuu. Lkn gharama itakuwa kubwa zaidi!
 
Pinda hao nyoka wako wanaokuletea intel inabidi uwafanyie vetting upya, otherwize watakuingiza shimoni... Afu unapenda kuzalilika sana wewe kiumbe sijui kwa nini, utafikili huo uwaziri mkuu ulizaliwa nao!
 
Pinda hao nyoka wako wanaokuletea intel inabidi uwafanyie vetting upya, otherwize watakuingiza shimoni... Afu unapenda kuzalilika sana wewe kiumbe sijui kwa nini, utafikili huo uwaziri mkuu ulizaliwa nao!
Nani awafanyie vetting?Hapa issue ni mshahara,na siyo vetting.Polisi hawapati posho,wastafu wa jeshi wameunda chama cha kudai Mishahara na Posho,sasa unategemea nyoka wanakula nini?Unajua endapo mlinzi wa benk hajalipwa mshahara benk itapona?.Unadhani kumunyima mtoto chakula utakuwa salama? Mtoto lazima ale ila akiiba mzazi utawajibika kumuwekea dhamana akikamatwa polis
 
Back
Top Bottom