Tume ya mabadiliko ya katiba

Mzee mtei hapa umepotoka kabisa, mambo ya kuweka udini kwenye mambo ya kitaifa ndo yanaviathiri vyama vya upinzani kutokana na propaganda za ccm. Ww ulitakiwa ujadili mambo ya kitaifa na sio mambo ya dini.
 
Mkuu Ukweli unabakia pale tu hata kama huutaki.. Acha kumhangaisha mzee wa watu wakati kasema point na ushahidi upo. Refer kwenye majina ya tume.

Lakini kama ungetaka uwiano wa dini, Zanzibar kuna wakristu wangapi wanaoweza kuwa kwenye hiyo tume? Wengi kule ni Waislamu. Hata kama wale walioteuliwa kutoka bara wangekuwa Wakristu, Waislamu wa Bara nao wangekuwa na haki ya kulalamika, kwa sababu wale wa Visiwani wanatoka upande mwingine wa Muungano.

Tukumbuke kuwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili na kulingana na terms za muungano lazima kuwe na uwiano kwenye masuala ya msingi kama kubadilisha katiba ya Jamhuri. Kwa upande mwingine, tatizo ni kwamba walionzisha huu Muungano hawakutiliana maanani kama kutakuja kutokea vitu kama hivi ambavyo inabidi pale zote mbili za Muungano zihusishwe kwa uwiano.

Kwa hiyo, suala la kuwepo kwa uwiano kwenye tume ya katiba ni moja ya shortcomings za Muungano wenyewe. Rais alikuwa hana cha kufanya hapo zaidi ya kufuata sheria. Tukitaka haya yasitokee tena basi tu-address the core problems underlying the Muungano.
 
Most of the members are from CCM... My take all members should declare their interests (Which political party are they affiliated with) so that we know what kind of people we do have in the committee... Some names are not so popular when it comes to political party affiliation but women like Esther Mkwizu, she belongs to TISS so at any material time she will be defending the interests of her political party!

Let them declare their interests! I know sometimes they may want to agree on some issues if they decide to vote... the trend is clear that the majority (Whom I believe to be those of CCM until proven otherwise) will win and at the end of the day we might end up with something that does not align with the wishes of most of the Tanzanians...

I remain to be corrected

Karikenye.....
 
hapa hakuna katiba mpya, wazanzibar kupitia maalim na justa walisema iletwe katiba ya zenji na ya tanganyika mezani then waamue mambo yepi ya kuunganisha. Tanganyika hatuna katiba, zanzibar wanayo. Hakuna nia ya dhati kupata katiba mpya kwa upande wa tanganyika
 
Kama huyu ndie Edwini mtei wa CDM basi ameonyesha true color ya chama chake!
alitaka JK aweke wtu kwa uwiano wa kidini? kama angefanya hivyo hao wajumbe si wangefanya kazi kwa mujibu ya dini zilivyowatuma na sio wananchi!
 
Tamko la CHADEMA ndio hilo

Mtei ni baba mkwe wa Freeman Mbowe sasa mnategemea nini?

Nitashangaa sana kama Tamko halijaandaliwa na mzee Mtei from his "farm" huko Migombani aka Moshi


 
Mzee Mtei, siamini kama ni wewe ndio umeandika hii thread au mjukuu wako anatumia ID yako..

Zanzibar ni nchi kamili sio sehemu ya Tanganyika halafu umenisikitisha kuonyesha udini wako kwenye hiyo orodha.

Ebu toa maoni yako ulikuwa unataka hiyo tume iwe na muundo gani kuliko kukosoa tu.
Udogo wa Zanzibar haiwakoseshi haki ya kuwa nchi kamili.
Kwahiyo kama ni nchi kamili na ni ndogo huoni mantiki ya hoja yake?Ama muungano huu si wa watu?Hivi wazanzibari wanauchukulia huu kuwa ni muungano wa vitu gani?Maana wao wako juu, kuanzia kwenye rasilimali hadi watu, kiukweli naelekea kuichukia zanzibar na huu muungano kabisa.
 
Mkuu namuhangaisha vipi wakati kaleta mjadala jamvini namuheshimu Mzee Mtei kama unavyomuheshimu tunajadili alichokileta.

Kuna watu wengine kutoka Tanganyika wanalalamika pia kuwa JK kachagua Wakiristo wengi kuliko Waislam.

Waislam wa 4 tu wakati Wakirsto 15 na wakuu wa tume wote wakiristo Jaji J, Warioba, Jaji A. Ramadhan.
Kwani katiba mpya ni ya Tanganyika ama ya Zanzibar?
Kuna ujinga mkubwa sana unaendelea na umekuwa ukiendelea kwa muda miongoni mwetu, huu ni wakati wa kuufutilia mbali once and for all!
 
Kwahiyo kama ni nchi kamili na ni ndogo huoni mantiki ya hoja yake?Ama muungano huu si wa watu?Hivi wazanzibari wanauchukulia huu kuwa ni muungano wa vitu gani?Maana wao wako juu, kuanzia kwenye rasilimali hadi watu, kiukweli naelekea kuichukia zanzibar na huu muungano kabisa.

Anachosema Mtei mimi nimekisema kuwa JK amekosea na amewapendelea wakristo wa Tanganyika

kati ya wajumbe 15 wanne ndio waislamu ina maana Tanganyika nchi ya wakristo hii? balaa
 
Mmmhhhh!!! hata mimi siamini mzee Mtei kweli ndiye anaweza kuandika kilichoandikwa hapo juu.

Naamini ni msomi mzuri ambaye kabla ya kuandika lazima aziangatie facts mbalimbali zilizo wazi. Tunaweza kupinga uwingi wa watu kutoka Tanzania visiwani kwenye tume hiyo. Hilo ni suala la katiba zaidi na perception of fairness. Ili katiba ikubalike sehemu zote ni muhimu kwa Tanzania visiwani kuhisi wameshirikishwa ipasavyo.

Sasa tukiacha hilo, asilimia 99 ni Wazanzibari ni Waislam kwa majina pamoja na dini. Hivi kweli ulitegemea kwenye tume ambayo ina uwakilishi sawa wa bara na visiwani majina ya kislam yafanane na ya kikristo? Hii haiwezekani logically and factually.

Ili premise yako ya kuwa na uwiano wa majina ya Kiislam na Kikiristo ifanane ni lazima majina yote ya Kiislam yaondolewa kwa watu wa bara au watu wenye majina ya kikristo watafutwe zanzibar hata kama hawana sifa. Hiyo less than one percent ya Wazanzibar wakristo wawakilishe nusu ya tume kwa Zanzibar. kwa mawazo nyangu hilo haliwezekani.

Hizi dini za kuletewa na wageni inaelekea zimeingia sana vichwani mwetu.
Kama katiba tunayoitafuta ni ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, basi ni kweli tume ina waislam wengi, tena ukizingatia kuwa CUF na CCM ni dam dam, basi udini uko in the mix, trust me on this!
Inahitaji uelewa kuiona hii kitu.
 
Anachosema Mtei mimi nimekisema kuwa JK amekosea na amewapendelea wakristo wa Tanganyika

kati ya wajumbe 15 wanne ndio waislamu ina maana Tanganyika nchi ya wakristo hii? balaa
Hatutafuti katiba ya Tanganyika, rejao, sorry, rejea swali nililomwuliza nduguyo Ritz.
 
Mzee Mtei, mimi nakuita baba kwa sababu nimesoma darasa moja na mtoto wako Meli.

Pili nakupongeza kwa kutoa maoni yako kuhusu hii tume, bali lazima nikiri wazi, baba umeanza kuzeeka!.

Hii ni tume, kazi ya tume sio kutupatia katiba bali ni kukusanya maoni, hii inamaanisha kazi ya tume hii ni kutusikiliza sisi Watanzania tunataka nini, halafu ndipo iya compile maoni hayo, sasa wewe wasiwasi wako wa nini?.

Hoja zako zote mbili baba, hazina mashiko.

1. Hili la uwiano, wa wajumbe 15 kutoka bara na 15 kutoka Zanzibar, sio la JK, hili ni takwa la kisheria ambalo ni lazima litimizwe!. Rais hapa hakuwa na choice ametimiza jinsi sheria ilivyosema.

Kijana wako Tundu Lissu hili alilipigia sana kelele mpaka akaonekana ni mpinga maendeleo. Kwa vile wewe ni miongoni mwa visima vya hekima, busara na uzoefu tulivyo navyo, ungetoa hoja binafsi kuwa kutokana na uwingi wa watu na ukumbwa wa eneo, muungano wetu uendeshwe kwa proportional representation na sio equal basis kama ulivyo sasa!. Naamini ungesikilizwa!.

Hizi haki za Zanzibar ndani ya muungano, zimekuwa zikikiukwa kwa miaka mingi mpaka tujajisahau kwa kudhania Tanzania bara ndio yenye haki kubwa ndani ya muungano kutokana na wingi wa watu na ukubwa wa eneo, kitu ambacho sii sawa. Tanzania na Zanzibar ni two partners wenye haki na hadhi sawa ndani ya muungano wetu kama zilivyo ndoa za kiserekali mkishaoana, siku mkiachana, mnagawana mali pasu kwa pasu na mkeo, hata kama ni wewe ndio ulikuwa umechuma hiyo mali na mkeo ni mama tuu wa nyumbani!.

Zingatia simaanishi hii ndio uwiano bora, ila hapa rais Kikwete ametimiza matakwa ya kisheria!.

2. Hili la pili la udini pia halijakaa vizuri, kwa vile idadi ni watu 14 toka kila upande tena kwa rais kupelekewa mapendekezo ya majina, hakuna shaka kuwa asilimia 99% ya Wanzanzibari ni Waislamu, hivyo ili kuweka uwiano wa dini, jee ungetaka hao wajumbe 14 toka Zanzibar ndio wawe Waislamu halafu wale 14 wa bara ndio wawe Wakristu?.Au hata kama hakuletewa hata jina moja la Mkristu kutoka mapendekezo ya Zanziabar, basi rais angejitafutia japo Mkristu mmoja amteua ili ionekane Zanzibar nayo ina Wakristo?!.

Kwa vile katiba tunayoitafuta ni katiba ya nchi na sio katiba ya uendeshaji wa ibada wala kupanga utaratibu wa swala, naomba tuipe imani, hata kama inawajumbe wengi kutoka dini fulani, hadidu za rejea hazionyesha kama aumuzi wa nini kiwepo kwenye katiba mpya na nini kisiwepo, utaamuliwa kwa wajumbe hao kupiga kura, hivyo Wakristo watashindwa!. Hoja hii ya uwiano wa bara na visiwani na Ukiristu na Uislamu, utakuwa na mashika wakati wa uundaji wa bunge maalum la katiba ambalo ndilo litaamua nini kiwepo na nini kisiwepo kwa kupiga kura, na wa mwisho kabisa ni sisi wananchi, kupiga kura ya maoni "referendum" kuikubali au kuikataa!.

Naamini yule mdogo wako mule kwenye tume, atayasimamia maslahi yako ipasavyo hata kama yuko yeye mmoja tuu!.

Namalizia kwa kuomba radhi tena kama kutaonekana ukosefu wowote wa adabu kwa wakuu wetu.

Asante.

Pasco.
Mkuu Pasco nitakujibu kifupi sana,

Tume hii ni lazima i reflect tunachokitafuta, yani katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Period.

Hatutafuti katiba ya Tanganyika ama Zanzibar.

Hivi haki ya Zanzibar ndo haki ya waislam?Usichanganye madwa hapa.
 
Mzee Mtei, siamini kama ni wewe ndio umeandika hii thread au mjukuu wako anatumia ID yako..

Zanzibar ni nchi kamili sio sehemu ya Tanganyika halafu umenisikitisha kuonyesha udini wako kwenye hiyo orodha.

Ebu toa maoni yako ulikuwa unataka hiyo tume iwe na muundo gani kuliko kukosoa tu.
Udogo wa Zanzibar haiwakoseshi haki ya kuwa nchi kamili.

ritz, ki ukweli huwa natofautiana sana na wewe hasa pale unapoteteaga chama chako kwenye hoja ambazo ziko wazi..Ila kwa hili nakuunga mkono 100%.

Zanzibar ni nchi kamili, kama ni muungano basi unapaswa kuwa 50-50. Pia hata swala la udini lisiwe kigezo cha kuchagua watu kwenye hii tume, watu wachaguliwe sbb ya uwezo wao
 
  • Thanks
Reactions: EMT
hapa hakuna katiba mpya, wazanzibar kupitia maalim na justa walisema iletwe katiba ya zenji na ya tanganyika mezani then waamue mambo yepi ya kuunganisha. Tanganyika hatuna katiba, zanzibar wanayo. Hakuna nia ya dhati kupata katiba mpya kwa upande wa tanganyika
Hatuna mtu anayeitwa justa ZNZ, tunaye mwanaharakati jussa na mkombozo wa wananzibar.
 
Mkuu Pasco nitakujibu kifupi sana,

Tume hii ni lazima i reflect tunachokitafuta, yani katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Period.

Hatutafuti katiba ya Tanganyika ama Zanzibar.

Hivi haki ya Zanzibar ndo haki ya waislam?Usichanganye madwa hapa.

We kweli huwajui wananzibar,
hujawahi kusikia viongozi wa serikali ya mapindizi ya zanzibar wakiunga mkono uvunjaji wa baa na uchomaji wa moto? uliza hadi sasa ni zaidi ya baa 50 zimeteketea na hakuna hata mtu mmoja aliye wekwa rumande, hawasemi kuwa ni uislam ila wanasema ni kinyume na mila na desturi za wazanzibar!
Sisi wazanzibar tunaamini kabisa wajumbe wa zanzibar lazima walinde UTAMADUNI WETU!
 
Mzee Mtei, siamini kama ni wewe ndio umeandika hii thread au mjukuu wako anatumia ID yako..

Zanzibar ni nchi kamili sio sehemu ya Tanganyika halafu umenisikitisha kuonyesha udini wako kwenye hiyo orodha.

Ebu toa maoni yako ulikuwa unataka hiyo tume iwe na muundo gani kuliko kukosoa tu.
Udogo wa Zanzibar haiwakoseshi haki ya kuwa nchi kamili.
Vile vile ukubwa wa Tanganyika hauikoseshi sifa ya kuwa nchi kamili na wala sio sehemu ya Zanzibar by whatever means you are trying to kill Tanganyika and christianity you will never succeed it is illogical for over 40 millions Tanganyikans to be represented by 15 and not more than 2million Zanzibaris to be represented by the same number of 15 and at the same time in the region where christians are more than 70 percent of the whole population to be overidden by the minority in the population.
 
Licha ya kwamba J.K. kajitahidi kuwa na vigogo kweli kweli, na Katiba ya sasa imezingatiwa ktk kuandaa m'badala wake, muundo wa hii Tume umedhihirisha kwamba demokrasia ya kweli ni ndoto kwa Watanzania wa leo. Kama tunanuia kwa dhati kuwa na Demokrasis ya kweli, itabidi Watanzania wanaoamini kwamba hilo ni muhimu, waendelee na juhudi za kuandaa hata Mabadiliko kwa Katiba Mpya ijayo.

Kwa mfano ni jambo la kichekesho kwamba Tanzania Bara ambayo ina Watu takriban 42 milioni iwakilishe na wajumbe sawa na Tanzania Zanzibar ambayo ina watu wasiozidi 1.5 milioni. Mfano wa pili ni kwamba, licha ya kwamba Tanzania siyo nchi inayozingatia dini katika maamuzi yake ya kisiasa, ni lazima tukubali kuwa madhehebu ya dini yana influence katika mchakato na hatimaye maamuzi. Nikihesabu Waislamu katika hii Tume kwa kuzingatia majina naona zaidi ya theluthi mbili ni Wao. Wengine ni Wakristo au watu wasiokuwa na dini yoyote.

Hata kama ni lazima tujali Muungano wa Jamhuri yetu, hatuwezi kupuuza ukweli kuwa sasa kuna matatizo ya umilikaji wa raslimali maliasili (e.g. gas), na kuna wananchi wamediriki hata kwenda Umoja wa Mataifa kudai Zanzibar ijiondoe.

Haya ni mambo mazito na nimeona ni vema niyataje sasa, siyo tu yajadiliwe na Tume, bali ikiwa ni lazima, basi mjadala uendelee hata baada ya Tume kutoa taarifa na Bunge Maalum kupitisha Katiba Mpya.


I don't want to believe that Edwin Mtei can stoop this low and demonstrate his long held phobia against moslems. I would understand if he had issues with the intellectual pedigree of those who have been appointed to serve in the Commission. If what he alleges is true, then it means 50% of the members appointed from the mainland Tanzania are christians. Mzee Mtei knows that 99% of the Zanzibaris are moslems. How then did he expect to find christians in the Zanzibar's half of the Commission?

I would be delighted if Mzee had come up with a statement on the number of moslem MPs that his party appointed after the 2010 elections. We know that the number of christian MPs by far outstripped that of the moslem colleagues and he found it to be in good taste? Hypocrisy of the hughest order.
 
Mie sijamnyooshea kidole mtu mwingine nimeandika nachokiamini.

Wewe hujaandika unachokiamini bali nafsini mwako pia ulikuwa na dukuduku, cha ajabu badala ya kulitoa baada ya kuona Mtei alichoandika ukamshambulia badala ya wewe kutoa wazo lako. Hii ndio tabia ya watanzania walio wengi wala sishangai. We have diverse and conflicting views which we must share and agree the way forward, sio kumshambulia mtu huku umeminya mawazo yako binafsi.
 
Back
Top Bottom