Edwin Mtei
Senior Member
- Dec 13, 2008
- 181
- 342
Licha ya kwamba J.K. kajitahidi kuwa na vigogo kweli kweli, na Katiba ya sasa imezingatiwa ktk kuandaa m'badala wake, muundo wa hii Tume umedhihirisha kwamba demokrasia ya kweli ni ndoto kwa Watanzania wa leo. Kama tunanuia kwa dhati kuwa na Demokrasis ya kweli, itabidi Watanzania wanaoamini kwamba hilo ni muhimu, waendelee na juhudi za kuandaa hata Mabadiliko kwa Katiba Mpya ijayo.
Kwa mfano ni jambo la kichekesho kwamba Tanzania Bara ambayo ina Watu takriban 42 milioni iwakilishe na wajumbe sawa na Tanzania Zanzibar ambayo ina watu wasiozidi 1.5 milioni. Mfano wa pili ni kwamba, licha ya kwamba Tanzania siyo nchi inayozingatia dini katika maamuzi yake ya kisiasa, ni lazima tukubali kuwa madhehebu ya dini yana influence katika mchakato na hatimaye maamuzi. Nikihesabu Waislamu katika hii Tume kwa kuzingatia majina naona zaidi ya theluthi mbili ni Wao. Wengine ni Wakristo au watu wasiokuwa na dini yoyote.
Hata kama ni lazima tujali Muungano wa Jamhuri yetu, hatuwezi kupuuza ukweli kuwa sasa kuna matatizo ya umilikaji wa raslimali maliasili (e.g. gas), na kuna wananchi wamediriki hata kwenda Umoja wa Mataifa kudai Zanzibar ijiondoe.
Haya ni mambo mazito na nimeona ni vema niyataje sasa, siyo tu yajadiliwe na Tume, bali ikiwa ni lazima, basi mjadala uendelee hata baada ya Tume kutoa taarifa na Bunge Maalum kupitisha Katiba Mpya.