Tume ya Maadili ya Viongozi - The Joke and the Joker!

Ni kweli kabisa they are laughing us tunapopiga kelele, sioni sababu ya kuwaeleza watanzania kuwa hatuwezi kuwashitaki wezi wa EPA, sio wezi tu bali pia waliforge documents kwa kuogopa pesa yao.
nikiingia akilini mwao naona wanasema "Waache waseme mwisho watatulia, mangapi yamesemwa lakini hawafutilii tena na tukigombe tunashinda kwa kishindi"
Lakini siku za mwizi ni arobaini na za mwenyewe ni moja, one day yes tutawaonyesha kuwa we are people's power

Chuma kimepata kutu...ukikwangua sana kitakatika.
 
nakubaliana na wewe mkuu maneno yako.
mie mtazamo wangu nahisi kama MUUNGWANA hayupo kimya,ila tu anaacha MWIZI SIKU ZAKE 40 zitimie,so tumeshaona ya CHENGE 40 yake imetimia,kwa maana hiyo JK anamuchia tu upepo uchukue nafasi yake mwenyewe aachie ngazi.
niliwahi sikia nyeti moja kuwa ile alivyoingia JK na kuwapa nafasi za uwaziri wapambe wake inasemakana aliwambia "haya jamani nakupeni nafasi za uwaziri/n.waziri etc mtu akifanya madudu na maozaoza basi wananchi watamhukumu wenyewe"tumeona akina EL na wenzake jinsi w'nchi walivyowahukumu na kupata AJALI ZA KISIASA.

i may be wrong,lalkini naamini JK term yake ya pili anaweza kufanya wonders kubwa sana,kwa nini nasema hivyo??? naamini kwa dhati ameshawasoma watendaji wake wote,anajua nani mbabaishaji nani mchapa kazi n.k

mkuu unajua unapoingia ktk madaraka kuna mambo mengi sana unakumbana nayo,system ilokuweka n.k huwezi tu kuingia na kuanza safisha safisha n.k,ingawa wengi wanaulaumu USALAMA WA TAIFA(RO na timu yake),mie bado naamini kuwa jamaa wanafanya kazi nzuri sana ila tu unajua usimhukumu mtu mchunguze kwa kina na mapana ili ujue ile chains nzima ya walaji ili ukija kuondoa unaondoa yote na sio kipande cha nyama tu.

mkuu nyimbo mbaya habembelezewi mtoto,kwa maana hiyo sio dua zuri kuliombea taifa letu.

kumbuka maneno ya INVISIBLE "TANZANIA NI YETU SOTE"

HUO NI MTAZAMO WANGU TU.i may be wrong.


Nadhamini mchango wako mkuu wenye mtiririko mzuri.
Nashukuru umesema unavyoona wewe na ukataka mtazamo wa wengine juu ya hayo uliongea.

Ila kwa maoni yangu ktk dunia ya sasa iendayo kasi rais anatakiwa achague watu makini competent ili kwenda na kasi ya dunia ya sasa.Hakuna muda wa kujaribisha au kuweka marafiki ati mkiboronga basi wanainchi watawahukumu.Kwanza rafiki si mzuri ktk uongozi kwa kuwa unakuwa mzito kutoa discipline na pia wao wanakuwa wana take things for granted.

Jambo la pili mafanikio ya kitu chochote tunatakiwa kuangalia output ndio tunasema project imefanikiwa na dunia ya sasa ndivyo inataka sio kuwa tu na malengo ya kufanya jambo fulani zuri au nia zuri.Approach anayotumia ni mbovu na kwa muda uluobaki hatutegemei miujiza.Don't tell me tumemchagua huyu jamaa kwa term mbili No!.Competent ya mtu inapimwa ktk kipindi kigumu with respect to time limit,he is not the one.Kama anashindwa kuonyesha accomplishment yoyote sasa kwa nini tumchague tena kama tuna akili timamu tena kipindi cha pili ambacho hata jali kwa kuwa hataomba kula tena.
Vinginevyo umesema vema kuwa tusiombee mabaya nchi yetu
 

...Miongoni mwa taasisi hizo ni Tume ya Maadili ya Viongozi ambayo ina Sekretariati ya kudumu ambayo jukumu lake ni kusimamia utekelezaji (compliance) ya sheria ya Maadili ya 1995 as ammended.

Tatizo kubwa la Tume/Sekretariati hii ni kuwa wao hawawezi kuanzisha uchunguzi wa uvunjaji wa maadili kwa viongozi hadi pale mtu au chombo kingine kilete malalamiko rasmi dhidi ya kiongozi huyo. Bila malalamiko hakuna uchunguzi. Yaani, kisheria hakuna "trigger mechanism" kuwa jambo fulani likitokea basi Tume inafanya hivi au vile...

Mwkjj;
Inawezekana pia ni Kamishena mwenyewe hana nia ya kuanzisha uchunguzi bila malamiko kwa sababu Bunge lilirekebisha sheria na kuongeza lugha inayoweza kutafsiriwa kama nguvu unayosema inakosekana:

2001/5 An Act to amend the Public Leadership Code of Ethics Act, 1995 Act, to provide for smooth implementation of the Act.

Section 18, subsection (4)

The Secretariat shall, in addition to the duties conferred on it under subsection (2) and (3) have power to initiate and to conduct any investigation in respect of breach of ethics prescribed under this Act.


[Subsection (2) inashurutisha uchunguzi baada ya shutuma.]

Pia, iliongezwa lugha inayomwongezea Kamishena nguvu ya kuchunguza kwa kulegeza namna malamiko yanavyoweza kuletwa. Unaweza kushutmu kwa mdogo, hivyo masharti ya u-rasmi yamepunguzwa:

Subsection (3)
The Secretariat shall, in performing its duties under this section, have the power to receive and entertain all allegations in respect of any public leader, whether oral or written from members of the public
 
Nimemsikia Waziri Chikawe juzi akilalamikia suala la Tume ya Maadili... Miaka zaidi ya miwili baada ya watu humu kuanza kulalamikia..
 
Nadhani tumpe muda mwezi 1 JK kama hajabadilisha ule uozo...tujaze petition....kuwatoa wote akiwemo Jaji Ihemi ndio liliobakia labda kuna vikwazo wao kufanya kazi wapishe wengine
 
Ukisoma katiba ya JMT ibara ya 132 (1-5) 5a-f) nashindwa kuelewa je hii sekretarieti ni usanii au vipi maana tangu nimekuwa mkubwa sijawahi kusikia imempeleka kiongozi mkubwa a.k.a kigogo mahakamani kwa ubadhiifu au kumchukulia hatua.
Ukiangalia ibara ya 132 inasema Kutakuwa na sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma ambayo itakuwa na mamlaka ya kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha masharti ya sheria ya ya maadili ya viongozi wa umma yanazingatiwa ipasavyo.
132(5) misingi ya maadili ya viongozi wa umma
a...................................
b...........................
c. itapiga marufuku tabia na mienendo na tabia inayopelekea kiongozi kuonekana hana uaminifu, anapendelea au si muadilifu au inaelekea kukuza au kuchochea rushwa katika shughuli za umma au inahatarisha maslahi au ustawi wa jamii
d. itafafanua adhabu zinazoweza kutolewa ili kuhakikkisha utekelezaji wa maadili

Hii pamoja na sheria ya maadili ya viongozi wa umma na adhabu wallizoweka hadi leo sijasikia kiongozi ameadabishwa.
wapo viongozi wengi wanahamasisha rushwa, hawana maadili na wanalipeleka taifa pabaya lakini hii tume ni hovyo tu kila mwaka wanaandika mali na madeni lakini hakuna llolote kuishwahishi jamii kuwa hii tume inafanya kazi ipasavyo limefanyika. Je ina manufaa yeyote kwa taifa au inaliingizia taifa hasara kwa kuwalipa mishahara wafanyakazi ambao hawafanyi kazi yao ya kuchukua hatua yoyote kwa mafisadi.
Kwa yeyote anayejua mazuri ya sekretariet hii anihabarishe tafadhali maana watanzania wanakufa kwa umaskini huku wachache wakineemeka chini ya tochi ya sekretarieti hii ikiwalinda
 
Imekuwa ni namna ya kupeana ulaji tu,
nishajikatia tamaa mie.
Na kweli, naamini hata wafanyakazi wa hii sekretarieti ni watoto wa vigogo, na wanajua wazi wazazi wao wanachokifanya na wanachomiliki na hawachukui hatua,
Halii hii mpaka lini????
 
Ha haaaa haaa! Umewahi kuona mbwa anambwekea bosi wake?
Napita tu wakuu![/QUOTE
Huwa anafyata mkia daima, vivyo hivyo kwa hawa jamaa, hivi kweli ni waziri yupi ambaye hamiliki mali zinazozidi kipato chake, yule jamaa wa jeshi anamiliki mapesa hadi serikali ya South inashangaa then sekretarieti ipo kimya tu, na wala haijui na haitaki kujua, mawaziri wenye mahoteli je? Wale walioilleta dowans, richmond hii sekretariet haikuwepo?
 
:lol::lol:Sioni kazi wanafanya coz ndio kwanza watu wanazidi kujilimbikizia mali:lol::lol:
Huu ni ukweli na utabakia kuwa hivyo daima hata wao wakija hapa na kubisha. Alafu eti usalama wa taifa upo na unajisifia unafanya kazi. Kweli utawala wa JK ni bab kubwa na tutamkumbuka
 
Wadau nahitaji elimu kidogo,hiki kitu ni nini? Kina majukumu gani? Wafanyakazi wake wanapatikanaje? Naomba msaada kwa mwenye taarifa sahihi!
 
hii tahasisi sijui kazi yake,nilitegemea ingekuwa inaingilia kati kwenye swala la wabunge kutoa matusi
 
Tuwasubiri waje watoe majukumu ya taasisi yao; lakini kama watendaji wameteuliwa na JK; siamini kama watajitokea.
 
Serikali imesema bado kuna tatizo la usimamizi na ufuatiliaji wa maadili katika taasisi za umma kutokana na kukosekana kwa afisa mahsusi mwenye jukumu hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria , Angellah Kairuki katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa wakuu wa idara ya utawala na rasilimali watu katika wizara, idara zinazojitegemea, sekretarieti za mikoa, wakala na taasisi za umma.

Kairuki alisema kuwa kukosekana kwa afisa huyo kunaacha mwanya kwa watumishi kukiuka maadili pasipo kujulikana au kuchukuliwa hatua.

"…hali ya kutochukua hatua kwa wanaokiuka sheria na taratibu inachangia ongezeko la ukikwaji huo," alisema.

Alitolea mfano wa ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni, taratibu na miiko ya kazi katika utumishi wa umma kuwa ni pamoja na ulevi, ufisadi, uzembe, rushwa, utumiaji mbaya wa madaraka, mali na magari ya serikali.

Naibu waziri huyo aliwataka wakuu hao kujiangalia kwanza kabla ya watumishi wengine kwani kuna taarifa kuwa wengine baada ya kushushwa na gari ofisini, wanaruhusu gari kutumika kufanya shughuli za nyumba zao.

“Wengine wanatumia kuwabeba waumini wenzao wanaosali nao kanisani hata wengine kutumia magari ya serikali kubeba mkaa na vitu mbalimbali kama ilivyo hapa kwa Mkoa wa Dodoma nimeona yakibeba mkaa,”alisema.

Alibainisha kuwa rasilimali watu ikisimamiwa vibaya matokeo yake
ufanisi na tija hushuka na tija ikishuka na uchumi nao hauwezi kukua inavyotakiwa.

Hata hivyo, alisema badala ya maafisa kuwachukulia hatua za
kinidhamu watumishi wanaofanya makosa kwa kuzingatia miongozo yao, wanaandika barua utumishi kuomba maelekezo na wengine kuwahamisha jambo ambalo alidai kuwa ni kutowajibika au uvivu wa kufikiri.

Akizungumzia utoaji maoni ya rasimu ya Katiba mpya, Kairuki
alisema mpaka sasa hakuna wizara au taasisi ya serikali iliyoomba kuendesha mabaraza ya katiba.

Aliwaagiza wakuu hao kujielimisha na kuelewa juu ya mwongozo wa mabaraza ya katiba ili kusimamia ipasavyo utoaji maoni ya rasimu ya Katiba.

CHANZO: NIPASHE
 
Kuna Tume ya Maadili ya Viongozi, hivi imefanya nini vile mpaka sasa hivi? Tatizo la viongozi wetu ni kufikiri maadili, utii wa sheria ni kwa watu wa chini tuu. Nafikiri tungeona kazi ya tume ya maadili wa viongozi inafanya kazi ipasavyo huku kwingine ingekuwa rahisi sana.
 
Kuna umuhimu gani wa viongozi wetu (wa umma na wanasiasa) kutangaza mali zao? Kama upo...Sekretarieti ya

Maadili ya Viongozi wa Umma inatimiza jukumu lake IPASAVYO au routine tu? Kama Mpiga

kura/Mwananchi,

ninawezaje kujua mali za mbunge wangu anapoingia na ANAPOTOKA MADARAKANI?
 
Wakati wa mwalimu Nyerere, ukiwa kwenye shughuli za kikazi na ukapewa zawadi ulitakiwa upeleke kwa muajiri wako kwa maamuzi, mama prof Tibaijuka kale ka billion alidecrare kwa prof Jakaya?
 
Back
Top Bottom