Tume ya kupanga ADA za shule binafisi.

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,326
5,263
Wakuu salaam sana,ni mara ya kwanza kukanyaga jukwaa hili.
Katika magazeti ya leo kulikuwa na habari kuwa tume ya kuratibu ada kwa shule binafisi itaanza kazi januari,na tume itapanga bei moja kwa shule zote na ikitokea kuna shule inataka kuweka ada ya bei ya juu lazima ipewe kibali maalum.
My take,january ndio shule zinafunguliwa na hao wameliki wameshaarifiwa au ndio yale ya mgomo kama kwenye mafuta.
Naomba kuwasilisha hoja.
 
Yaani hiyo wasilete longolongo ya ahadi hewa tunataka utekelezaji mara ifikapo January, siyo waje na kauli; tunajipanga, mchakato unaendelea,na maupuuzi kama hayo.
Hizi shule zinatuumiza sana, eti kabla ya mtoto kujiunga unalipa laki 4 za majengo kisha katikati ya mwaka wanaitisha mkutano tena wakiwa na mikakati hiyohiyo na kuwalazimisha wazazi wachange laki mbilimbili kila mwaka kwa ajili ya ujenzi - inakera sana, yaani mzazi ni kitega uchumi cha wamiliki wa shule.
Yaani ikiwezekana warudishe na zile walichangisha kwa hila kama nilivyoeleza hapa.

Natanguliza shukurani kwa serikali kwa kuliona na kulishughulikia hili.
 
........Kwa kweli serikali hii ifanye kama ilivyoahidi.... umuhimu wa ada elekezi ni jambo zuri, kuna shule ambazo zinajipangia ada na kuwaumiza wa TZ tunasubiri kwa hamu kubwa sana.....
 
Wakuu nashukuru sana kwa kujadili hii mada,mimi ni mwathirika na hiza ADA nina watoto wawili nasomesha shule binafsi nalipa ada sh 940,000 kila mtoto na hapo ni bila usafiri na chakula.kwa kipato changu siwezi kujega wala kufanya chochote cha maana zaidi ya kusomesha.
 
Tanzania kila kitu ni tume tume! makabati yena hayajajaa tu mkaachana na vitu msivyovifanyia kazi nyie viongozi?
 
Mimi natofautiana nanyi ndugu zangu kama ifuatavyo, hizi shule zinaitwa PRIVATE SCHOOLS, hulazmishwi kumpeleka mwanao pale na iwapo unampeleka mwanao pale tnategemea kua wewe umekubaliana na kuridhika na vigezo vyao, kama wewe n mwenzangu na mimi shule za kata zipo jaman. Huu uratibu wa ada kwa hizi shule utazipunguzia uwezo hizi shule kwa kiasi kikubwa hivyo kushusha kiwango cha elimu nchini kwetu. Tukumbuke kua serikali haihusiki hata kidogo kwenye uendeshaji wa hizi shule.
 
Wapunguze ada ili wanawake wakubali kuzaa watoto zaidi maana walikuwa wanalalamika issue ya kusomesha ingawa wababa ndio walipaji.
 
Tanzania kila kitu ni tume tume! makabati yena hayajajaa tu mkaachana na vitu msivyovifanyia kazi nyie viongozi?
Kama wiki moja iliyopita nilizungumzia kuhusu ulaji mwingine kwa wakubwa, utaona wanapeana ajira mwisho wa siku ada zitabaki pale pale!
 
na ukizingatia hizo shule wao ndio wamiliki,kama ile moja ya bagamoyo nasikia ni ya mr dhaifu ada yake si mchezo
 
Yaani hiyo wasilete longolongo ya ahadi hewa tunataka utekelezaji mara ifikapo January, siyo waje na kauli; tunajipanga, mchakato unaendelea,na maupuuzi kama hayo.
Hizi shule zinatuumiza sana, eti kabla ya mtoto kujiunga unalipa laki 4 za majengo kisha katikati ya mwaka wanaitisha mkutano tena wakiwa na mikakati hiyohiyo na kuwalazimisha wazazi wachange laki mbilimbili kila mwaka kwa ajili ya ujenzi - inakera sana, yaani mzazi ni kitega uchumi cha wamiliki wa shule.
Yaani ikiwezekana warudishe na zile walichangisha kwa hila kama nilivyoeleza hapa.

Natanguliza shukurani kwa serikali kwa kuliona na kulishughulikia hili.

Wewe wasema, wakizivuruga zikawa kama za kata, watoto wa hao wanaozivuruga ndio watakuwa watawala pekee wa nchi hii! Watoto wao hawatasoma hizo shule! Yangu macho!
 
Pamoja na kwamba ada ziko juu hii inatokana na mfumuko wa bei. badala ya serikali kuharibu mfumo wa hizi shule ambazo ndiyo tumaini lililobaki ishughulikie mfumuko wa bei gharama zitapungua zenyewe.
 
Wakuu nashukuru sana kwa kujadili hii mada,mimi ni mwathirika na hiza ADA nina watoto wawili nasomesha shule binafsi nalipa ada sh 940,000 kila mtoto na hapo ni bila usafiri na chakula.kwa kipato changu siwezi kujega wala kufanya chochote cha maana zaidi ya kusomesha.

umelazimishwa kuwasomesha kwenye shule binafsi?
 
Waunde na tume ya bei za gesti pia.......what nonsense......hviv hawajui kuwa viwango vya huduma za kielimu hutofautiana kama ilivyo uwezo wa wazazi kilipa ada?
 
Mh makubwa zinakupa shida bro punguza matumizi ya nyumba hizo, mwisho wake si mzuri sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom