Tume ya katiba wajumbe kupewa gari na nyumba kila mmoja siyo rushwa?

Josephine

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
786
812
Ni jambo la kusikitisha sana,pale wajumbe wanapokuja kutumikia nafasi yao kwa kulinda heshima na marupurupu waliyonayo,badala ya kutumikia hoja zawananchi.

Kwangu mimi kupewa Nyumba na gari ni rushwa,wengi watapaswa kutumikia nyazifa hiyo badala ya kazi maalum waliyopewa,na hapa ndipo uwajibibikaji utakuwa tatizo.

Nimeleta hapa tujadili na kutuma ujumbe kwa wahusika.
 
Hata mi nilishangaa.

Kwa wale wenye nyumba tayari watapewa allowance nono.

Lakini nadhani magari ni ya matumizi ya kazini , gari muhimu lakini wakimaliza wanayaacha...????????? !!
 
Nasubiri kuona kama wataacha hayo magari,lakini hata nyumba,wao wanapaswa kuzunguka nchi nzima na si kuka kwenye hizo nyumba.

Nikija kwenye magari,serikali inamagari mengi sana,kunasababu ya kununua mapya,kwanini wasitumie magari ya wizara.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

....Nakubaliana nawe kabisa kwamba wizara zinaweza kutoa magari ili kusaidia zoezi hili hivyo kutokuwa na sababu za kununua magari mapya. Kununua magari mapaya ni ufujaji wa pesa za walipa kodi. Kuhusu nyumba... kwanini wapewe nyumba wakati watakuwa hawakai sehemu moja zaidi ya mwezi!? Kwa maoni yangu hakuna sababu za kuwapa nyumba wajumbe wa zoezi hili.
 
ni jambo la kusikitisha sana,pale wajumbe wanapokuja kutumikia nafasi yao kwa kulinda heshima na marupurupu waliyonayo,badala ya kutumikia hoja zawananchi.

Kwangu mimi kupewa nyumba na gari ni rushwa,wengi watapaswa kutumikia nyazifa hiyo badala ya kazi maalum waliyopewa,na hapa ndipo uwajibibikaji utakuwa tatizo.

Nimeleta hapa tujadili na kutuma ujumbe kwa wahusika.

jambo la msingi hawa wajumbe kuwa wazalendo na kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria iliyowaweka hapo, lakini hebu fikiria wale kutoka mikoani mnataka walale nje? Au watembee kwa miguu au daladala zetu za kugombea? Hata heshima na hadhi waliyopewa na rais haitaonekana na kuthaminika.
Yuwaombe wateule hao kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuwasaidia watanzania wenzao ambao wameweka matumaini makubwa kwao. Tunataka katiba mpya yenye maslahi kwa taifa letu na sio kujadili eti kupewa nyenzo za kazi kuwa rushwa!!!!!
 
Kama kuna mtu anataka umaarufu wa kusikika kwamba amekataa gari basi afanye hivyo, kwani tumeona wangapi wakisema hawataki magari wala posho lakini leo hii maisha yao ni tofauti na maisha ya watanzania wanaowawakilisha, kusema kuwa wameokota mali hizo? Watanzania wenzangu, tuwaombe hawa wajumbe kutufanyia kazi yetu ya msingi na wala sio kukataa nyumba na magari kwa kudhani kuwa ndio ufanisi wa yale waliyoteuliwa kwayo.
Mungu ibariki tanzania.
 
duh hii nilikua sijaisikia aisee, kweli Bongo hakuna waadilifu sasa nyumba za nini?
 
jambo la msingi hawa wajumbe kuwa wazalendo na kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria iliyowaweka hapo, lakini hebu fikiria wale kutoka mikoani mnataka walale nje? Au watembee kwa miguu au daladala zetu za kugombea? Hata heshima na hadhi waliyopewa na rais haitaonekana na kuthaminika.
Yuwaombe wateule hao kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuwasaidia watanzania wenzao ambao wameweka matumaini makubwa kwao. Tunataka katiba mpya yenye maslahi kwa taifa letu na sio kujadili eti kupewa nyenzo za kazi kuwa rushwa!!!!!

Kwani kuwa mjumbe wa tume ni sawa na kuwa waziri? Je, maoni ya Watanzania watakuwa wakiyapokea kwenye nyumba hizo? au una maana watapewa nyumba kila mkoa au kila wilaya nk?
 
Back
Top Bottom