Tume ya Katiba mpya, ni jambo gani ungetaka tukakusemee kwenye mikutano inayoendelea?

Nimegundua mawazo mengi yapo kwenye utawala bora badala ya uongozo bora ( refer Prof Shivji na mijadala yake ITV) Tunahitaji pia kujadili Autonomy ya uongozi ktk ngazi ya Msingi/shina, kijiji/mitaa na wilaya.

Uwezo wao wa kujichagulia viongozi, kumiliki ardhi na kuamua hatma ya maisha yao kwa ujumla. mjadala huu ni mwelekeo wa uongozi bora vs utawala bora.

Kwa maoni yangu lazima tuachane na utawala bora ktk katiba mpya, badala yake tukazanie uongozi bora ambao umejikita kwenye dhana ya nguvu ya umma. Najua hili linahitaji maelezo marefu sana kueleweka kwa mtu ambaye hana background hii na hajamsikiliza prof Shivji.
 
Kwenye Red,
FJM Hivi ni lazima Rais apendekeze halafu wabunge wapitishe JINA mmoja? Kwanini tusiseme kuwa Wataomba kazi kwa utaratibu tofauti kabisa wa kuchaguliwa bungeni ili wawe huru. Hapa namaanisha wakuu wa Polisi, mkiti wa tume ya Uchaguzi, Mkurugenzi wa Takukuru, DCI nk. Ni swali la ufahamu tu.

Kwangu mimi sioni kabisa sababu ya kuwa na TAKUKURU, hii idara ifutwe, it is waste of public funds. Ukiwa na DPP, police zinazofanya kazi vizuri huna haja ya TAKUKURU.

IGP, DCI, DPP, and most definately mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wanaweza ku-apply hapo sina tatizo. Lakini kwa mkuu wa TISS lazima ufanyike utararibu mwingine tofauti na wa ku-apply na pendinge nilifiki internal organs zinasaidiana na ofisi ya rais ili kupata nominee, then bunge lipewe nafasi ya kuthibitisha au kukataa. (hapa ni kwa TISS), Lakini hata hivyo TISS yenyewe inabidi kuundwa upya including sheria zinasimamia hiyo taasisi.
 
1. Tunataka Tanganyika Yetu

2. Wakuu wa wilaya waondolewe, nafasi zao zishikwe na wabunge

3. Majimbo yawe wilaya, na ya punguzwe

4. Ili kinamama wagangamale viti maalumu vifutwe

5. Wakuu wa mikoa wapigiwe kura (Uchaguzi mkuu)

6. RAS na DAD wawe makatibu wa mikoa wakisaidiwa na wakurugenzi wanatosha kuwakilisha serikali

7. Mawaziri na manaibu wao wasizidi 25.

8. Wakuu wote wa taasisi nyeti waombe kazi, kamati ya bunge iwainterview, na wapitishwe na bunge (TISSS Nk)

9. TISS iboreshwe kimfumo, na FIU, TAKAkuru na vingine viwe chini ya TISS) na policy zoa zipitiwe na kamati ya bunge. Kwanza nahisi hawana hata policies za operation (Hizi za mabwepande a-a)

10 Mfumo wa kiutawala uwe unganifu, Kijiji, kata, Wilaya, Mkoa, Taifa. Miundo bado iko hovyo ngazi za chini.

11. Tume isimamishe mara moja kazi za wajumbe wa nyumba kumi, maana ni wa CCM. Wasitambilike katika serikali ya mtaa

12. Wajue kabisa kwamba wanatakiwa kuandika rasimu ya katiba ya Tanganyika kama standby.

13. Jesh JWTZ lipunguzwe, hawana kazi, tuweke idadi ndogo na vifaa vya kisasa. Tupo sisi reserve army.

14. Tuwe na viwango, vya chini katika shule zetu zote, bila hivyo isifunguliwe, afya NK.

15. Viwanja vyetu vya michezo na vingine vilivyoporwa na CCM virudishwe serikalini

16. Raisi awajibiswe na bunge na asiwe na mamlaka ya kuwajibisha bunge

17. mawaziri wote wawajibishwe na bunge

18. Wabunge, Madiwani, Maviti wote wawajibike kwa mabaraza yao.

19. wajumbe wa mabaraza ngazi za chini wajulikane na wachaguliwe.

20. Mikataba yote ya taifa ipitishwe bungeni, either katika kamati na ile mikubwa bungeni.

21. TISS itoe taarifa zake kwenye magazeti, bungeni, na kadhalika. Ila tu zile za ulinzi ziende kwa kamati ya bunge. Eti hata ununuzi wa rada ni siri.

Kwa kifupi tuna taka Dola Umma

Aweda, Good work, unaelekea unapotakiwa.
 
Safi sana Aweda!

Binafsi sipo kwenye nafasi ya kutulia hapa ila ningependa kutoa mawazo ya mjumuisho, hvyo labda baadae nikipata mda nitafafanua au mtanisaidia kufafanua!

Kwanza ni suala la structure ya Executive yetu, hvi ni lazima tuwe na Rais, Makamu na Waziri Mkuu?
Nadhani ni mda sasa tuamue moja, kama tunamtaka waziri mkuu basi nafasi ya rais ni either ifutwe kwa maana ya kwamba tuwe na rais ambaye ni alama tu ya utaifa wetu ila hana mamlaka sana,
au kama vipi tuondoe cheo cha Waziri Mkuu asiye na mamlaka kamili ya kuliwajibisha baraza ambalo hajaliteua wala kuiwajibisha serikali ambayo yeye ni mtendaji mkuu....
Huu umekuwa ni mvurugo wa mda mrefu sana na umetuachia mgogoro wa maingiliano ya kimamlaka.
Ni bora tuwe na Waziri Mkuu mwenye mamlaka kamili na Rais atakayekuwa kama ni nembo tu ya utaifa wetu ila asiwe mtendaji wala mfanya maamuzi, au tuwe na rais mwenye mamlaka kamili akisaidiwa na makamu wake ila hcho cheo cha waziri mkuu garasa tukifutilie mbali.

Pia kuna masuala ya rasilimali za TAIFA, kama Watu, Madini, Gas, Mafuta, Ardhi, Mifugo, Misitu na rasilimali zingine zote za thamani za nchi tuangalie tunaweza kusema nini juu ya hivi vitu pia
 
1. Huduma zote za jamii zisimamiwe na serikali yaani( elimu, afya, maji na barabara)
2. Viongozi wote tunaowachagua(kama walivyopendekeza wenzangu) ndio wasimamizi wa huduma zote
3. Viongozi kwa kuwa ndio wasimamizi wa huduma hizo ni marufuku na ni mwiko kwa viongozi kwenda kupata huduma hizo kwenye taasisi binafsi au ngambo. Ni lazima wao na hata famila zao kupata huduma hizo kwenye taasisi za umma.
 
1.tume ya uchaguzi iundwe kwa kushirikisha wajumbe wa vyama vyote na isiteuliwe na rais, iwe chini ya jaji mkuu.
2.Wabunge wawe madarakani kwa vipindi viwili ya miaka mitano mitani basi
3.Wananchi wawe na uwezo/ modality ya kumuondoa madarakani mbunge wao endapo atakuwa hatekelezi ahadi zake na kuwahudumia ipasavo
4. Madaraka ya rais ni makubwa mno hasa ya uteuzi, pia sheria ikishatungwa na bunge hakuna haja rais kuisani iwe sheria, ikishapitishwa na bunge automatically iwe sheria
5. Kinga ya rais ya kutoshitakiwa akiwa madarakani au baada ya madaraka iondolewe
6.Matokeo ya uchaguzi wa urais yahojiwe mahakamani, na pia yakishatangazwa kuwe na kipindi cha mwezi mmoja kabla ya kuapishwa rais ili kama kuna mtu mwenye shaka na matokeo afungue kesi
7.Idadi ya wizara na mawaziri itamkwe kwenye katiba mpya na kila rais ateue kufuatana na katiba sio ilivo sasa hivi anateua kwa kushauriana na mke na watoto wake
8.Mawaziri wasiwe wabunge ila waombe kazi ya uwaziri wajiriwe na hakuna haja ya manaibu waziri na katibu mkuu wa wizara na wakurugenzi wanatosha kuongoza wizara, na mawaziri washiriki ushabiki wa vyama.
9.Speaker wa bunge akitoka chama tawala naibu wake atoke kwenye chama rasmi cha upinzani bungeni yaani kinafuatia kwa wingi wa wabunge
10.Jaji mkuu asiteuliwe bali aajiriwe na ajira idhibitishwe na bunge hivo hivo kwa mkurugenzi wa TAKUKURU, tume ya haki za binadamu, mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali.
11.Muundo wa muungano uwe na wa serikali tatu ya Tanganyika na Zanzibar zitakazoongozwa na mawaziri wakuu watakaoteuliwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
12.Adhabu ya kifo ifutwe kwenye sheria za nchi
13. vyeo vya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya vifutwe na badala ya wawepo wakurugenzi wa wilaya na mikoa watakaomba kazi hizo na ajira zao kuidhinishwa na bunge.

14 .Chama cha siasa amabacho hakitapata hata mbunge mmoja wakati wa uchaguzi mkuu kifutwe mara moja

kwa leo inatosha nitaendelea kuchangia mengine
 
Safi sana Aweda!

Binafsi sipo kwenye nafasi ya kutulia hapa ila ningependa kutoa mawazo ya mjumuisho, hvyo labda baadae nikipata mda nitafafanua au mtanisaidia kufafanua!

Kwanza ni suala la structure ya Executive yetu, hvi ni lazima tuwe na Rais, Makamu na Waziri Mkuu?
Nadhani ni mda sasa tuamue moja, kama tunamtaka waziri mkuu basi nafasi ya rais ni either ifutwe kwa maana ya kwamba tuwe na rais ambaye ni alama tu ya utaifa wetu ila hana mamlaka sana,
au kama vipi tuondoe cheo cha Waziri Mkuu asiye na mamlaka kamili ya kuliwajibisha baraza ambalo hajaliteua wala kuiwajibisha serikali ambayo yeye ni mtendaji mkuu....
Huu umekuwa ni mvurugo wa mda mrefu sana na umetuachia mgogoro wa maingiliano ya kimamlaka.
Ni bora tuwe na Waziri Mkuu mwenye mamlaka kamili na Rais atakayekuwa kama ni nembo tu ya utaifa wetu ila asiwe mtendaji wala mfanya maamuzi, au tuwe na rais mwenye mamlaka kamili akisaidiwa na makamu wake ila hcho cheo cha waziri mkuu garasa tukifutilie mbali.

Pia kuna masuala ya rasilimali za TAIFA, kama Watu, Madini, Gas, Mafuta, Ardhi, Mifugo, Misitu na rasilimali zingine zote za thamani za nchi tuangalie tunaweza kusema nini juu ya hivi vitu pia

Nakuunga mkono hakuna haja ya makamu wa rais na waziri mkuu! mmojawapo anatosha,.pia hakuna haja ya manaibu waziri au manaibu katibu mkuu! wizara ikiwa na waziri, katibu mkuu na mkurugenzi mkuu imekamilika!!
 
Acheni mambo ya kikoloni, katiba mpya kila mtu anatakiwa ajisemee, nyie mnaenda kila mkutano kuziba nafasi za wengine, udhulieni mkutano mmoja toa maona yako basi, mnataka kumsemea nani?
Hii ni kinyume na haki za wananchi na ni udhalilishaji mkubwa.

Mmelewa support ya jf mnaanza kudhani nyie ndo wasemaji wa wananchi?
 
1. Tuwe na mikoa isiyozidi 12
2. Kila wilaya iwe na; mkurugenzi na wataalamu mbalimbali watakaoshughulika na kazi mbalimbali ya kitaalum yanayohusiana na majukumu ya kila siku ya kiwilaya.
3. Kila wilaya mbuge mmoja.
4. Wizara zisizozidi 12.
5. Hakuna meya
6. Hakuna mkuu wa wilaya
7. Hakuna katibu tarafa
 
Acheni mambo ya kikoloni, katiba mpya kila mtu anatakiwa ajisemee, nyie mnaenda kila mkutano kuziba nafasi za wengine, udhulieni mkutano mmoja toa maona yako basi, mnataka kumsemea nani?
Hii ni kinyume na haki za wananchi na ni udhalilishaji mkubwa.

Mmelewa support ya jf mnaanza kudhani nyie ndo wasemaji wa wananchi?

Hatuendi kila mkutano mkuu, ila tunawawezesha wanaJF na watz kuchota mawazo mazuri hapa. Ila nini maoni yako kuhusu Ma DC wanaowakusanya watu wanaowataka na kuwapa cha kusema?
 
Vipi kuhusu uraia wa nchi mbili?
Uongozi wa ngazi ya chini kabisa uanzie wapi? Misingi/mashina au vijiji/mitaa? Kwa kwanini?
Vipi kuhusu nafasi ya mabalozi wa nyumba kumi? Turasimishe hiyo nafasi au ifutwe? If yes, why? If no, Why? Tusijikite mijini tu.
 
1. Huduma zote za jamii zisimamiwe na serikali yaani( elimu, afya, maji na barabara)
2. Viongozi wote tunaowachagua(kama walivyopendekeza wenzangu) ndio wasimamizi wa huduma zote
3. Viongozi kwa kuwa ndio wasimamizi wa huduma hizo ni marufuku na ni mwiko kwa viongozi kwenda kupata huduma hizo kwenye taasisi binafsi au ngambo. Ni lazima wao na hata famila zao kupata huduma hizo kwenye taasisi za umma.

Mkuu no 1 na 2 nina swali,
Nijuavyo, hata sasa huduma zote za umma zinasimamiwa na serikali au? Fafanua kidogo.
 
Hatuendi kila mkutano mkuu, ila tunawawezesha wanaJF na watz kuchota mawazo mazuri hapa. Ila nini maoni yako kuhusu Ma DC wanaowakusanya watu wanaowataka na kuwapa cha kusema?
Kuna wengine hawapendi wengine waelewe, wanapenda waelewe wenyewe. Usishangae kamanda.
 
Vipi kuhusu uraia wa nchi mbili?
Uongozi wa ngazi ya chini kabisa uanzie wapi? Misingi/mashina au vijiji/mitaa? Kwa kwanini?
Vipi kuhusu nafasi ya mabalozi wa nyumba kumi? Turasimishe hiyo nafasi au ifutwe? If yes, why? If no, Why? Tusijikite mijini tu.
Hapana, tutatengeneza wahaini. Kama mtakubali basi na mwanamke mmoja aruhusiwe kuolewa na wanaume wawili.
 
Hodi hodi wana jf. Nipo!. Hii mada nimeipenda.
Ningetaka katika katiba yaingizwe haya.
1.kwamba sera kuu za nchi ziingizwe kwenye katiba kusudi anayetaka uongozi atuambie atakavyotekeleza sera zetu. Isiwe kama sasa kila chama kinakuja na zake.
2.wakuu wa mikoa wagombee kama wanavyofanya wabunge.
3.elimu itamkwe ya kuwa ni bure kuanzia msingi mpaka chuo kikuu. Wakimaliza, jkt kwa kipindi cha miaka miwili.
4.ardhi kamwe isimilikishwe kwa wageni kwa namna yeyote ile. Iwe kwa wazawa tu.mapori yaliyoko yaachwe yalivyo. Watanzania wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki. Kwa vizazi vijavyo.
Ahsante sana!
 
Wakuu wa mikoa wakigombea, vipi kuhusu wakuu wa wilaya? Je, kama mkuu wa wilaya akichaguliwa kwa kura atakuwa anawajibika kwa mkuu wa Mkoa au kwa wapiga kura wake? Ufafanuzi.
 
1. Mshahara na mapato ya viongozi wa wakuu wa kitaifa yajulikane kwa walipa kodi/Watanzania (How? I don't know)
2. Viongozi wote wa kitaifa wastaafu wanaoendelea kuhudumiwa na kodi zetu wasijihusishe na siasa za vyama. (A Case Study Mkapa huko Arumeru Mashariki)
3. Wakuu wa Majeshi ya ULINZI na USALAMA eg CDF, IGP, yule wa Magereza, FFU wasijihusishe na SIASA za vyama hata baada ya kustaafu (A case Study Mboma (CDF) alitaka kugombea ubunge)
 
Back
Top Bottom