Tume ya ajira ina upendeleo waziwazi. Waziri wa kazi mulika hapa

makambakoo

New Member
Mar 8, 2012
3
1
Napenda kutoa malalamiko yangu katika hii tume inayoitwa Public Service Recruitment Secretariet. Nimefanya interview hivi majuzi. Wakati wa interview wamegawa vibahasha. Eti tuweke simu ndani na kuzima. Kumbe wao walikuwa wanataka tuweke pesa. Kuna watu wamepata kazi na wakaniambia wao walitumbukiza kitu kidogo. Ni bora serikali ikatizama namna mpya ya kuajiri wafanyakazi. Watu wenye sifa za kufanya kazi tupo. Ila undugu na rushwa hasa katika nafasi za senior positions katika serikali ndo unafanya hata nchi isiendelee. Nliomba nafasi ya Senior Human Resources Officer ktk Chuo cha Ustawi wa Jamii. Acheni ubabaishaji. Mnatakiwa kufanya kitu kinaitwa Competence Based Interview kupata watu sahihi kwa kazi sahihi. Waziri wa Kazi. Fanya reshufle ya hawa watu ktk tume ya ajira.
 
pole sana! yan haki inasemwa itatendeka wanapotangaza interview lakini haionekani hikitendeka.
 
kaka hii habari uliyoandika una uhakika nayo??maana ulichoandika ni serious issue
 
hiii ndo TZ hutaki kutoa unataka kupokea tuu mkuu!
Mambo yamebadilika mkuu!
 
Waliwahi kunibeeep siku moja hawa tume ya ajira kwa kuwa nina number yao na nishafanya interview ya kwanza, nilifata asubuhi yake lakini walikaata eti hawakunipigia nilipo waonyesha number yao wakaniomba msamahaa, eti niwa samehee. maaana walinipigia kimakosa.Hii tume ina urasimu sana bora ingefutwa tuuuuuuu.
 
Back
Top Bottom