Tumbo linamnyima raha mchumba wangu jamani.

Mliga

Senior Member
Oct 4, 2011
101
16
Wakuu kwa heshima yenu naomba mnisaidie kuirudisha furaha ya mchumba angu ilopotea tangu aanze kusumbuliwa na tumbo.

Tulifuatilia hospital wakatuambia dawa ni kumtandika MIMBA Ndo atapona! Tatizo suala la mimba yamekaa vibaya sababu hatukupanga, na isitoshe binti wa watu bado anapekua madaftari so ntampa mzigo mno na pia bado hatujaoana kwahyo inaweza leta shida zisizo za lazma.

Naomba msaada kama kuna tiba tofaut na hii, maana vilio haviishi had naogopa kupokea sim yake, ila alinigusia kuwa aliambiwa na wenzie eti ni "chango!" yaani hata sielewi! Nawasilisha wakuu.
 
Mkuu ndio ivyo walivyo nishauri aisee, na wakasema akishapata hiyo mimba tu matatizo yote yataisha ila ndo ivyo hali hairuhusu!
Mkuu pole kwa kuuguza,...ila naomba kuuliza unamaanisha ulishauriwa umpe mimba ndiyo atapona tumbo mkuu?!!
 
Mbona kama huo ushauri unaosema wa Hospitalini hauna mashiko? Upo serious na mada yako?
 
Yaani natoka ban nakutana na uzi kama huu.Sasa ushauri wangu ni huu kwanza uwe unapokea simu yake halafu fanya mpango mpeleke india haraka iwezekanavyo.
 
Pole sana mkuu,japo hujaweka wazi,najuwa unazungumzia tumbo la hedhi.Tafuta tangawizi na ukwaju kwa uwiano wa 1:2 Mf. (kg 1tangawizi) kwa kg 2)ukwaju. Safisha ukwaju,menya tangawizi,changanya tia maji Lita 3,chemsha,mgonjwa anywe kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa siku 5. KUMBUKA dawa hii inanywewa ikiwa ktk hali ya uvuguvugu,dawa ikiisha kabla,andaa kwa uwiano tajwa,ili siku zote 5 zitimie.
 
Nko serious sana mkuu, hata mi nlishangazwa lakini kutokana na kutokuwa na utaalam wa kitabibu ikabidi niwe mpole. Kwakweli anateseka mno hasa anapokaribia kipindi cha hedhi.
Mbona kama huo ushauri unaosema wa Hospitalini hauna mashiko? Upo serious na mada yako?
 
Pole sana mkuu,japo hujaweka wazi,najuwa unazungumzia tumbo la hedhi.Tafuta tangawizi na ukwaju kwa uwiano wa 1:2 Mf. (kg 1tangawizi) kwa kg 2)ukwaju. Safisha ukwaju,menya tangawizi,changanya tia maji Lita 3,chemsha,mgonjwa anywe kikombe cha chai kutwa mara 3 kwa siku 5. KUMBUKA dawa hii inanywewa ikiwa ktk hali ya uvuguvugu,dawa ikiisha kabla,andaa kwa uwiano tajwa,ili siku zote 5 zitimie.
Kwakweli mkuu umepitia humo humo, yaani kikikaribia kipindi cha hedhi hali ndo inakuwa mbaya mno, tena ukizingatia yeye huwa anavusha hata mwezi! Nashkuru sana kwa ushauri wako ngoja niufanyie kazi naamini utamsaidia.
 
Ila pia kwa ushauri wangu kama wewe ni mkristo naomba umshauri aende kwenye maombi, mimi nilikuwa na hilo tatizo ikifikia kipindi kama hicho siku 3 siendi kazini niliagiziwa dawa zote lakini iliyoniponya ni baada ya kufanyiwa maombi na kubeba hilo tatizo kama mzigo wakati ninapoomba.

Kuna watu wana tabia ya kurushia wasichana mapepo yanaenda kukaa kwenye kizazi ili kila anapokaribia hedhi awe anaumwa ila nina imani kama mimi nilipona naye atapona maana nilikuwa naumwa asikuambie mtu anayejua adha niliyokuwa naipata ni mungu aliyeniponya.
 
Hakuna daktari atakae kwambia "mtandike mimba" mkeo. Hakuna

Chagueni maneno ya kutumia mnapozungumzia watu mnaowaheshimu
 
Nko serious sana mkuu, hata mi nlishangazwa lakini kutokana na kutokuwa na utaalam wa kitabibu ikabidi niwe mpole. Kwakweli anateseka mno hasa anapokaribia kipindi cha hedhi.

Dawa ni mazoezi kuna ambao nilikuwa nasoma nao mpaka wanazimia kwa ajili ya tumbo na kilichowasaidia ni mazoezi
 
Hakuna daktari atakae kwambia "mtandike mimba" mkeo. Hakuna

Chagueni maneno ya kutumia mnapozungumzia watu mnaowaheshimu
Ni kweli hilo neno sio neno zuri kwa mtu unayemuheshimu, na nimelitumia makusudi kuonyesha kuwa daktari hakumuheshimu mchumba wangu kwa ushauri ambao haukuzingatia mazingira aliyonayo kama yana mruhusu kubeba mimba.

So sikuandika ili kumkosea heshima mtarajiwa wangu.
 
Ni kweli hilo neno sio neno zuri kwa mtu unayemuheshimu, na nimelitumia makusudi kuonyesha kuwa daktari hakumuheshimu mchumba wangu kwa ushauri ambao haukuzingatia mazingira aliyonayo kama yana mruhusu kubeba mimba. So sikuandika ili kumkosea heshima mtarajiwa wangu.

Daktari yeye kazi yake ni kukutajia dawa. Dawa ni kuwa mjamzito. Ulitaka uambiweje?

Daktari hajamvunjia heshima hata chembe huyo mchumba wako, ulomvunjia ni wewe
 
Ni kweli hilo neno sio neno zuri kwa mtu unayemuheshimu, na nimelitumia makusudi kuonyesha kuwa daktari hakumuheshimu mchumba wangu kwa ushauri ambao haukuzingatia mazingira aliyonayo kama yana mruhusu kubeba mimba. So sikuandika ili kumkosea heshima mtarajiwa wangu.

Ni vema ukubali kwamba si vema kutumia lugha ya "kutandika mimba" au ya namna hiyo katika mazingira yoyote.
 
Ni vema ukubali kwamba si vema kutumia lugha ya "kutandika mimba" au ya namna hiyo katika mazingira yoyote.
Nimekuelewa Mkuu ila cha umuhimu ni kupata msaada wa kulimaliza tatizo lake kwa njia tofauti na ujauzito, sababu hayuko tayar, na vilevile haliko katika mipangilio yetu kwa sasa.
 
Kwa tumbo la uzaz(chango)weng tukienda hosptal tunaulizwa "je,upo tayar kupata mtoto?" whch means kubeba mimba na kujifungua ndiko humaliza tatizo..kwa ushaur na njia mbadala achemshe maj aweke kwenye chupa awe anajikanda,ale vyakula vyenye calsium kma dagaa,anywe maziwa fresh lakn ayaweke tanbond ya kutosha na anywe yakiwa yamoto kias.

Dawa za hosptal zipo ila si nzuri hasa kwa mwanamke ambae hajapata mtoto bado.
 
Nashkur kwa ushauri wako, tena tumbo lenyewe linauma kwenye kitovu au chini ya kitovu. Hayo maumivu anayolalamika, Aisee we acha tu
...!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom