tumbo kujaa muda wote

mopm

New Member
Feb 13, 2012
2
0
hivi ni ugonjwa au ni kawaida kwa tumbo kua kama limejaa gesi au umeshiba muda wote hata umeze dawa za ktoa gesi hazisaidii kuna wakati unaweza fikiri ni mimba ukupima hakuna .hali hii inasababishwa na nini?
 
Pole sana.Tumbo lina mambo mengi na huko kujaa huwasumbua watu wengi kiasi cha kuwafanya wakose raha sana
Hebu sema kama una symptoms hizi:

  • Tumbo kufutuka
  • Kujisikia gesi tumboni
  • Kucheua kulikozidi
  • Kujiskia kama umevimbiwa
  • Maumivu tumboni
Kama ndio hebu jichunguze ni aina ya vyakula gani ukila vinakuletea hali hiyo.
Nenda hospital upime haja kubwa kuona kama kuna bacteria au vimelea vinavyojikita kwenye utumbo na kukuletea gesi.

Daktari atafanya uamuzi kuhusu tiba baada ya kuona vipimo.
 
We mama we, ukiwa na mimba unajisikia umeshiba?

Nenda kapime vidonda vya tumbo na kwa wakati huu jihadhari na beverages. Gesi sio nzuri kwako
 
kweli hizo dalili ninazo,nashukuru ntafanyia kazi ushauri wako
.
 
jaribu pia kuvaa nguo zisizo bana tumbo. ukifunga mkanda uwe lose.
 
hivi ni ugonjwa au ni kawaida kwa tumbo kua kama limejaa gesi au umeshiba muda wote hata umeze dawa za ktoa gesi hazisaidii kuna wakati unaweza fikiri ni mimba ukupima hakuna .hali hii inasababishwa na nini?



jaribu kuangaria kama unamatatizo yafuatayo

ugonjwa wa ini (liver cirrhosis)
kansa ya tumbo
intestinal obstruction kwa kiswahili sijui
peritonitis

hayo magonjwa huambatana na kujaa kwa tubo inaweza kuwa ascites kujaa maji tumboni na kusababisha kujaa kwa tumbo sometime wanaita abdomen distension gasi na maji
dalili kama
1.kukoswa usingizi
2.kutojisikia vizuri(discomfort)
3.kushindwa kupumua vizuri
4.maumivu ya tumbo
5.kuishiwa hamu ya kula
kwa ushauri nanda hosp ukachukue vipimo kama FBP, x-ray, na pia umuone Dactari kwa ajili ya dawa
 
kula tu bila kufanya mazoezi yoyote pia ni tatizo. Angalia kama unakaa ofisini na ukitoka ni kwa gari bila kua activity yoyote.
 
mopm GESI TUMBONI (COLIC): Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.

TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.
 
Last edited by a moderator:
hivi ni ugonjwa au ni kawaida kwa tumbo kua kama limejaa gesi au umeshiba muda wote hata umeze dawa za ktoa gesi hazisaidii kuna wakati unaweza fikiri ni mimba ukupima hakuna .hali hii inasababishwa na nini?
Abari yako...nime ona ulikuwa na hili tatizo...mimi pia lina ni tesa sana nilikwa nakuuliza pengine ulitumia dawa gani uka poa.?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom