nijuavyo mimi ni kuwa CT scanner inaweza kupatikana kwa bei ya $80000
je brand new land cruiser ni sh ngapi?
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Hakuna ugumu wowote kwa Tanzania kuwa na CT scanner kila wilaya. Uwezo upo, ni swala la wataalamu kuweka hilo kwenye vipaumbele tu. CT scanners hazinunuliwi kwa sababu wataalam hawajaziweka katika vipaumbele. Mwanasiasa hawezi kunyanyuka na kusema anataka kununua kifaa ambacho hajui kama ni kipaumbele katika sekta husika.
mkuu hatutaki the best wakati hatuna zile ambazo ni za msingi.just find a good one!hata ya kichina ipatikane kwa kuanzia.niambie kama simu au computer unayotumia ni the best au la.
Mkuu sometimes tuwe wakweli. Hiyo bei uliyo-mention labda ni kwa USED CT Scanner. Na kwa bahati mbaya sana kwa sheria "tulizojiwekea wenyewe", serikali hainunui vifaa chakavu. Kwa mashine mpya, nikichukulia mfano wa "Toshiba CT Scanners" ambazo ni one of the best in the world, bei kidogo inatisha. Statement hii nimei-quote kutoka site moja:
"The machine is expensive -- about $2.5 million, versus $1.5 million for a typical CT scanner. But hospitals should be able to pay back the difference in as little as two years, because they might save as much as $3,000 diagnosing a heart attack or stroke."; Ref: http://www.wired.com/gadgets/miscellaneous/news/2008/04/Toshiba_CTScanner
Ukiangalia, kwa uwekezaji wa hiyo mashine, mgonjwa atalipia around $3,000 (T.Shs. 5,000,000/=) hadi $5,000 (T.Shs. 8,000,000/=) ndizo bei za sehemu nyingi duniani gharama ya hicho kipimo!
HATA HIVYO, hoja ya msingi ni kwamba ni wajibu wa Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake regardless of gharama; si busara kuacha wananchi wateketee kwa kisingizio cha gharama. Kama mapato ya nchi yangedhibitiwa vizuri, wala hiyo bei siyo issue kama serikali ingeamua na kujali wananchi wake.
Viongozi wetu hawana utashi wa kuwasaidia wananchi wake. Kama ingekuwa ni "issue" ya kununua jet ya rais, hapo suala la ughali lisingezungumzwa hata kidogo. Wananchi tungeambiwa tule nyasi kuliko kukosa ndege ya rais! Kama Serikali ikinunuliwa CT Scan, viongozi watapata wapi mwanya wa kupata "per diem" (in $s) za kwenda kwenye matibabu Appolo na nchi zingine?
hivi aghkhani wamenunua sh ngapi mpaka serikali ishindwe kununua
ct inaumuhimu sana! ila najiuliza hawa madr wa kipindi cha nyuma wao ct yao ilikuwa ni kitu gani, na mbona walikuwa wanato huduma vizuri na ya uhakika tu!mgonjwa ukitoa maelezo yako alikuwa anauwezo wa kukuelekeza kwenye kipimo husika bila hat haya mambo ya ct! hii ct itabaki kuwa muhimu hasa kwa sasa mana ninamashaka ma uwezo wa madokta wa sasa hasa hawa masharo! wasije kutuumiza bure! sirikali inapaswa kufanya hii kitu muhimu na ct inaei kuliko hayo magari lakini isiwe sababu ya wao kuto zinunua wakati uwezo wanao!
ningekuona mwenye akili iwapo ungeuliza hawa wanasiasa wetu walitembelea usafiri gani hapo zamani kabla ya kuanza kutumia Mashangingi,je walikuwa hawafiki majimboni mwao?je wagonjwa wetu wanatumia mashangingi kufika hospitali?
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
wewe si umependekeza madokta watibu kizamani?kwa nini wanasiasa wasifanye siasa kizamani?
Elewa mahitaji ya nchi kwa hali ya sasa ndio ujibu hoja,usikuripuke!
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA