Tuma salaam spesho za miaka 50 ya uhuru

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
5,759
5,289
Napenda kuwa2mia salaam Mzizimkavu,kongosho,ff,mzee wa loliondo bila kusahau mods wote wakiwa jf.Ujumbe miaka 50 tushamaliza 2songe mbele ili tuongeze 50 mingine.....Wewe unamsalimu nani na nani na unawapa ujumbe gani??
 
Napenda kuwa2mia salaam Mzizimkavu,kongosho,ff,mzee wa loliondo bila kusahau mods wote wakiwa jf.Ujumbe miaka 50 tushamaliza 2songe mbele ili tuongeze 50 mingine.....Wewe unamsalimu nani na nani na unawapa ujumbe gani??

wewe gamba tu. umemaliza miaka 50 kwa mafanikio au hasara?
 
katika miaka hii 50 ya uhuni, namsalimu mmalaria sugu.
 
leo bonta anavaa nguo nyeusi kuomboleza miaka 50 ya mateso..:confused3:
 
Natuma salamu kwa hayati mwl JK Nyerere popote pale alipo.
Ujumbe: baba, tuma walau email ya ku-redefine uhuru manake sina hakika kama ulituhusu sie wadanganyika
 
Salam kwa
MKWAWA,KINJEKETILE NGWALE,
nawaambia kuwa mlipgana na wakolon il kulinda utu wetu,mali zetu na utamaduni wetu!LEO HII WENZENU WANAWAITA WAZUNGU,WAARABU NA WAHINDI KWA JINA LA WAWEKEZAJI,WANABEBA MADINI,WANYAMA PORI NA KILA KITU
 
salaam kwa wale wote waliozaliwa tarehe kama ya leo miaka hamsini iliyopita. Salaam maalum ni kwa wana jukwaa walikuwepo siku ya Uhuru wa Tanganyika kama akina Faizafoxy. Happy birthday.
 
Natuma Salam kwa Malkia Wa Uingereza

UJUMBE: Njoo uchukue tu koloni lako angalau utarudisha Reli, bandari za ukweli, mashamba, viwanda n.k, Huyu mkoloni alieko sasa anasafisha kila kitu mpaka mchanga anasafirisha
 
Natuma salamu za rambirambi kwa TANGANYIKA. Namwomba mora ampumzishe kwa amani kwani ni miaka 47 sasa ametutoka.
 
Nawapa pole watanzania wote kwa kufikisha miaka 50 kwa mateso, kuendelea kuchagua viongozi kwa kuwasikiliza matapeli kutaendelea kdidimiza taifa.
Nashauri watanzania uchaguzi wa miaka 2015, tusipo fanya mabadiliko, tutayatafuta kwa nguvu, patakuwa hapakaliki kubebana tumechoka
 
salam zangu ziende kwa wale wafanyakazi wote wa serikali waliocheleweshewa mishahara yao mwezi huu kwa uvumilvu wao waliounyoshesha.
 
Back
Top Bottom