Tulizeni mioyo Watanzania

Sheep-3.jpg

twabadilika
 
Nimechoka sana! nimechoka tuuuu!. sikuwahi kufikiri kuhusu mchoko wangu, sijui imetokeaje, do i know? Nipe MG yangu nitoe mchoko wangu, yuko wapi aliyenichosha?
nawaza kuhusu hili, jibu ninalo, lakini sina uhakika, ni wewe? hawata kosea? Pingu zangu..aaah! zetu ziko wapi?
kweli ukiwaza unawazua....unawazua? yes, inawezekana. ngoja nitarudi.
 
Mwaka huu ni mwaka wa Uamuzi wetu; ni mwaka wa uchaguzi wetu. Tusiwaache wanasiasa watuamulie tunachotaka ili tuwachague; tuwaamulie kile tunachotaka ili wakikubali tuwachague!!

Nakubaliana na wewe kabisa, shime watanzania tuzingatie ushauri huu na tuufanyie kazi ipasavyo.
 
Salaam,

Kwanza naomba niwatulize mioyo wale ambao kwa namna moja au nyingine wanajisikia kukwazika na kile kilichoendelea Bungeni leo hii na hasa suala la Richmond. Ninafahamu watu wengi wangependa kuona mambo makubwa yanatokea tena na watu wanatimuana na hata ikibidi kupeana mipasho ya papo kwa papo. Wengine wangetamani kuona wale ambao walijitangaza kuwa ni wapiganaji wanachukua msimamo mkali zaidi na kutokubali kwa namna yoyote ile kulimaliza suala hili kimya kimya.

Hata mimi ningependa hivyo.

Hata hivyo, inaposemwa kuwa "siasa ni mchezo mchafu" siyo suala la utani ni suala la ukweli. Wakati wowote unaposhughulika na wanasiasa ni lazima utarajie mambo kama haya kama gharama ya wanasiasa. Lakini zaidi pia ni lazima tuzingatie kuwa wanasiasa wote (na hapa naamanisha wote duniani) wanafanya mambo wakiongozwa na kanuni kubwa tatu duniani:

a. Watafanya jambo lolote ili wachaguliwe kushika madaraka
b. Wanataka wachaguliwe tena kushika madaraka (re-election)
c. Endapo kuna uwezekano wa wao kutochaguliwa, angalia kanuni "a".

Hivyo, yaliyotokea Bungenii leo na yatakayotokea kwenye suala la Kamati ya Mwinyi na hata baadaye kabla ya kuvunjwa kwa Bunge katikati ya mwaka huu ni LAZIMA yaangaliwe kwa mwanga huo.

Kwa maneno mengine msipate matumaini ya uongo kusikia wanasiasa wanaanza kujitokeza kuwa wapiganaji ufisadi kweli kweli baadaye mwaka huu huku miongoni mwao wakiwa ni wale waliokuwa mawaziri.

Hawa mtawasikia wakijitetea kuwa wakiwa mawaziri wanatakiwa kusimamia maamuzi ya serikali n.k na wengine watasema walichukua maamuzi mbalimbali ili kuonesha umoja ndani ya chama na siyo kwa sababu walikuwa ni dhaifu! Yote ni katika kufanya kazi kwa kanuni "a".

Ninachosema ni kuwa tusiwaangalie wanasiasa kama chanzo cha matumaini yetu ya kulibadilisha taifa letu! Tusiweke imani yetu yote kwa wanaotaka madaraka kwa namna yoyote ile kwani uwezekano wa wao kutuangusha ni mkubwa mno kama tulivyoona. Wakati umefika sisi wananchi wenyewe tuamue kumshika ng'ombe mapembe yake na kumuongoza tunakotaka.

Hii ina maana gani? Maana yake ni kwamba bila ya sisi wananchi kusimama pamoja na kusema nini tunachotaka (siyo kukubali kile ambacho wao wanasema nini tunataka" basi hatuwezi kupata mabadiliko tunayoyataka.

Naomba niwatie shime enyi wana na mabinti wa taifa langu; msikate tamaa kwa kukatishwa tamaa na wanasiasa! Msiinamishe vichwa vyenu kwa masikitiko kwa sababu hawajakidhi mahitaji yenu! La hasha! Tuinue vichwa vyetu juu na kusema "tunawaelewa" na kwa sababu hiyo hatuwataki tena.

Muda unakuja ambapo Watanzania wataitwa wachukue msimamo dhidi ya wanasiasa wao; msimamo ambao utalitikisa taifa letu. Tumeanza kuona dalili zake toka mbali (CCJ na sasa "Tamko").. kama Moshi uliofichwa nyuma ya kilima tunaweza kusema kwa uhakika mahali fulani kuna moto; kama mwangaza wa jua linavyopambazuka tunaona nuru yake kabla hata halijatoka, lakini tuna uhakika kuwa nyuma yake lipo jua!

Mwaka huu ni mwaka wa Uamuzi wetu; ni mwaka wa uchaguzi wetu. Tusiwaache wanasiasa watuamulie tunachotaka ili tuwachague; tuwaamulie kile tunachotaka ili wakikubali tuwachague!!

Ni mimi ndugu yenu,
Mwenzenu,
rafiki yenu,
Na wengine adui yenu wa kudumu

Mpaka msalimu amri!!

M. M. Mwanakijiji

NB: Tutaanza matangazo yangu ya audio wiki ijayo inshallah.. mwendo mdundo mpaka kampeni.. zikiiva..tutaonana majukwaani!!

Wenye uwezo wa kurekodi CDs (downloads) tutakuwa na option ya kudownload episodes za "kijijini leo hii" na mnaruhusiwa kuzicheza na kuzisambaza mahali popote!!




Ahsante sana mwanakijiji maana nilikuwa nashindwa kuendelea na kazi asubuhi hii,baada ya kuona yaliyotokea mjengoni.
 


Hawa kondooo wako far better. Wana mchungaji, tena mzuri na mwenye kuwahurumia/kuwathamini. Kawawekea uzio ili kuwalinda na mwivi, majani ili washibe na mengine walalie. Hawajaachwa yatima. Sisi ni kondoo tunaotangatanga wakati chui na mafisi wameshaingia na kuzingira siyo nyika tu bali hata zizi. Yuko wapi wa kutuoakoa? Musa wetu atawahi kabla ya mafisi hayajatumalizia mbali? We are desperate na hilo tumaini linaweza lisiwepo tena. Tungetamani kuona kipenga cha dakika ya 90 na siyo ya 45! Inavunja mioyo kwani hatuoni hata malaika kilimani akija kutunyakua:confused::confused::confused::confused:
 
Tuache utamaduni wa kupenda rahisi na vya dezo. Tuanze kuwa makini na kuchapa kazi kwa bidii.

Tukifanya hivi, "ma-Richmonduli" yatatoweka yenyewe na neema itakuja. Bila hivyo, status quo itaendelea milele. Majina tu ndo yatakua yanabadilika.
 
Nilibahatika kuwaona "live" wachangiaji wa jioni ya jana akina Kilimba, Dr Slaa, Sendeka, Mawaziri Ngeleja na Marmo pamoja na WM mwenyewe. Ungedhani wote hawajawahi kuwepo Bungeni tangu sakata la Richmond lilipoanza isipokuwa Dr Slaa.
Wametupotezea muda wetu Watanzania. Fedha za walipa kodi wa nchi hii zimetumika nyingi kwenye sakata hili. Binafsi nilitegemea WM ndiye angetoa taarifa ya utekelezaji wa maazimio yale ya Bunge. Badala yake ikaachiwa kamati ijikaange na kula matapishi yake yenyewe. Tanzania hii sio yao wanasiasa wetu.
 
Ikawa usiku ikawa mchana, wakafunika kombe! Dhoruba ikatulia, tazama sasa wanajipanga kupangua na mengine kwenye mlolongo wa machafu yao. Saa ya mageuzi ndio sasa. Mwambie huyo, yule na wale pia, kuwa ule muda wa ukombozi ndio huu. Jikomboe Mtanzania
 
Niko busy naandaa 40 ya TZ japo imekufa siku nyingi si vibaya kufanya 40 yake.
 
katika mtatiziko mkubwa wa kisiasa kama uliotokea jana, hakika lipo jambo la kujifunza kinagaubaga kuwa, hii vita ya ufisadi haipaswi kupiganwa na wapiganaji waoga, wanaoanzisha vita wanaogopa matokeo yake, kweli leo Eng.Stella Manyanya wakusimama nakuisifia Serikali kuwa imetimiza wajibu wake ktk yale maazimio ya Bunge la kutaka serikali kuwafuta kazi baadhi ya watendaji, aibu kwake.
wamepoteza raslimali za taifa bila sababu, wameshindwa vita, mafisadi wanakenua, Mkuu wa TAKUKURU anawacheka, Mwanyika anawashangaa, Lowassa anapata sababu yakurejea tena ktk harakati ili kutimiza ndoto yake.
Naungana na MWANAKIJIJI kuwa Tusivunjike moyo, tusonge mbele, ili hali tukijua kuwa vita hii si lelemama, ni mpambano wa uzito wajuu.
 
msiumie sana jamani.. katika siasa.. you win some, you lose some.. and some hurt more too!! But as long as you have another day to fight.. pick yourself up, jipanguse vumbi na machozi, futa makamasi.. inua kichwa na mabega yako.. angalia mbele.. move!!!
 
Duh! Ama kwa Hakika niko Kizani tena Kiza Kinene, sijui hata wa Kumwamini LoL!
 
Hata wale walioapa kwamba Mjengoni hakutakalika sikusikia hata Miguno yao LoL!
 
Kwa yaliyojiri jana Bungeni naamini aina ya viongozi kama Lowassa ni muhimu ili demokrasia isonge mbele.Uthubutu, ujasiri na uzalendo wake leo hii uliwezesha hoja ya Richmond kuwa kubwa na yenye historia ya kukua kwa demokrasia yetu.

Wapambanaji wa ufisadi wa CCM leo wametuonyeshaaa kuwa kwao masilahi ya umma sio muhimu kama nafsi zao.

Alunta kontinua...
 
Kwa yaliyojiri jana Bungeni naamini aina ya viongozi kama Lowassa ni muhimu ili demokrasia isonge mbele.Uthubutu, ujasiri na uzalendo wake leo hii uliwezesha hoja ya Richmond kuwa kubwa na yenye historia ya kukua kwa demokrasia yetu.

Wapambanaji wa ufisadi wa CCM leo wametuonyeshaaa kuwa kwao masilahi ya umma sio muhimu kama nafsi zao.

Alunta kontinua...

inabidi kwa kweli Lowassa ajengewe madhabau ili watu wazunguke na uvumba!!
 
Mimi hata sikutegemea chochote from the get go, kwa hiyo nimejiepushia disappointment.

Mama yangu Tanzania;

Nakuonea huruma jinsi amabvyo mijibwa imekurarua na bila hata ya aibu inaendelea kukurarua!

Ole wao mijibwa; siku yao yaja amabapo itafungwa kwenye minyororo mikubwa na itoswe ziwa Tanganyika!:mad:
 
inabidi kwa kweli Lowassa ajengewe madhabau ili watu wazunguke na uvumba!!
MM, vyovyote iwavyo, naamini kupitia Lowassa ukombozi utapatikana, najua jana usiku yeye na Rostam Aziz waligonga glass kuashiria ushindi wao, hii ni kitambo tu.
Naamini Lowassa atatamani kurejea kwenye mamlaka za utawala hapa TZ, HUO sasa utakua wakati mwafaka kufanya mageuzi maana , ipo kasoro moja ya mapambano anayoyafanya, naamini kwa muda mfupi ameshinda vita ila inlong run ni looser tu.
 
msiumie sana jamani.. katika siasa.. you win some, you lose some.. and some hurt more too!! But as long as you have another day to fight.. pick yourself up, jipanguse vumbi na machozi, futa makamasi.. inua kichwa na mabega yako.. angalia mbele.. move!!!
Mi wala sijaumia, chembe ya hasira sina,
Matokeo nilijua, tangia awali sana,
We kweli litegemea, nini kitokee jana?
Waumbuane wenyewe, na ulaji upotee?

Badala yake nasema, kwetu ni motivesheni,
Mwiko kutazama nyuma, tuangalie usoni,
Oktoba ni kiama, swali je tufanye nini?
Tuwarudishe Ikulu, au sasa tufanyeje???

Tanzania tuamke, kweli jama tuamke,
Tusi-think kikekike, tusifanye kikekike, - (sorry ladies, ni mambo ya vina tu haya!)
Kamwe tusitetereke, sitirategi tuweke,
Haya mapambano yetu, siishie hapa JF.

Shalom!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom