Tuliwalinda zaidi CDM - Polisi aliyekuwepo Ndago

Naomba kupima uelewa wako.
Mwiguli nchemba aligawa pikipiki jimboni kawe za nini!!!

Epa gua penaazutyuuswa neelasi ka sika nugunua ne kenaazushanelelia,
munidyoolo nouga "laa uu uluuu uuu"

Uelewa wangu ni mkubwa sana Jogi, just PM me. Kikubwa sikatai kwamba hatakiwi kwenda kule ila kumbuka tayari walishakwaruzana Bungeni na wana kesi tayari sasa ile kwenda kwa Mwigulu kwa wakati huu ni kama kuchochea moto wa ugomvi kwa petroli. Ukweli uliopo ni kweli kabisa polisi walijitahidi sana kuwalinda akina Mnyika, hiyo ni kweli kabisa kwa sababu licha ya kuongea na askari aliyekuwepo pale nimeongea hata na mzee mmoja jirani sana na nyumbani kwa mwl ambapo mauaji yalifanyikia. Ukweli CCM watakuwa wameanzisha fujo za SIKU HIYO, lakini sio kwamba hiyo ilianzia hapo. Mnyika hakutumia hekima, na naamini toke ameshinda ile kesi ya ubunge Mnyika amekuwa na mambo ya juu juu tu, mimi nina marafiki waliompigia kura na wanampenda sana lakini wanakubali kwa sasa anaokesea.
 
Mdwenke hii stori ya kupika,huu ni umbea, acha uzushi, una sema eti hatokubali kulinda mkutano wa chadema, kwa taarifa yako hana ubavu wa kupinga kama atapangiwa kufanya hivyo,
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu ambaye ni polisi aliyeshiriki kulinda mkutano wa CHADEMA Ndago- Singida amelalamikia sana lawama zinazorushwa kwao kuwa hawakuchukua hatua zozote za kuwalinda CHADEMA.

Kwa mujibu wake anasema kazi waliyoifanya ni kubwa kuliko inavyofikiriwa kwani ni kweli walishapata taarifa kuwa CDM wanakwenda kumtukana Mwigulu na vijana wa CCM walikuwa wamejiandaa kwamba matusi yakirushwa tu wangejibu mapigo. Ilivyokuwa ni kweli vijana wa CCM walikuwepo mkutanoni na ilipotokea Mwikabe kuanza kurusha matusi wengi wakachukia sana na kuanza kulalama Kinyiramba "mukue, "mukue", "mukue", "mukue", wakimaanisha "apigwe" "apigwe", "apigwe", "apigwe".

Hivyo polisi walijitahidi sana kuzuia wale vijana wa CCM wasiwadhuru viongozi wa CHADEMA waliokuwepo pale akiwepo Mnyiramba mwenzao Mayu Dr Kitila Mkumbo. Ndugu yangu alishangaa sana baadaye kuona kundi la vijana wa CHADEMA waliokwenda kuwalinda ndiyo wanafanya fujo kwa kuwakimbiza wenzao na kwenda kumwuua mmoja nyumba ya jirani na wengine wawili kujeruhiwa vibaya sana.

Ila sasa kibao kinawarudia wao polisi eti walishindwa kulinda mkutano wa CHADEMA, ukweli anasema wasingefanya kazi yao wale viongozi wa CHADEMA wangedhurika sana. Kwake yeye hatakuwa tayari kulinda mkutano wa CHADEMA tena.

Source: Mawasiliano yangu na askari ndugu yangu aliyekuwepo kulinda mkutano wa CHADEMA Ndago - Singida.

Jibu rahisi kabisa: mweleze huyo ndugu yako kuwa hana sifa za askari na hafai kabisa kuwa askari. Why?
1. Mpaka huyo mtu anauawa walishakamata vijana wangapi wafanya fujo?
2. Kama walikuwa na taarifa za CHADEMA kwenda kurusha matusi dhidi ya Chemba walifanya nini kuzuia jambo hilo lisitokee?
3. Kama walikuwa na taarifa za wana-mabwepande kujipanga kurusha mawe, waluchukua hatua gani kuzuia hali hiyo isitokee?
4. Je, ni vijana wangapi ambao mpaka sasa wameshakamatwa kuhusiana na hizo kauli za uchochezi na kujichukulia sheria mkononi "mukue" kama anavyodai kuzisikia kaka yako kabla ya mawe kuanza kurushwa?
5. Je, ni watu wangapi walikamatwa wakati mkutano ukiendelea kuhusuka na vurugu hizo? Kama kulikuwa na kila sdalili ya uvunjifu wa amani, je ni kwa vipi basi walinzi wa amani wakaruhusu mkutano uendelee mpaka mwisho? Huoni kwamba na wao walikuwa wanafurahia "matusi" dhidi ya Chemba na kwamba ni dalili za kusapoti upinzani?

Ama kweli hatuna polisi, tumebakiwa na filimbi na virungu vya polisi tu.

Nitaendelea.........
 
Hiyo taarifa ya cdm kwenda kumtukana mwigulu huyu askari aliipata kutoka kwa nani?.je ni mtu gani ambae anaweza kutoa taarifa kwa askari kuwa tuna kwenda kumtukana mwigulu wakati akijua kutukana ni kosa na anaweza kushitakiwa kwani hata mtu mpumbavu hawezi kutoa taarifa km hiyo.baada ya askari kupata taarifa kutoka pande zote 2(ccm na cdm) kuwa cdm wamepanga kutumia lugha ya matusi na ccm wamejipanga kujibu. kwa nini askari hawakutoa ulinzi wa kutosha ili kudhibiti hali hiyo au kwanini waliruhusu mkutano uendelee wakati walijuwa kuwa kutakuwepo na uvunjifu wa amani wakati wanauwezo wa kuuzuia.kwani huyo askari ameajiliwa kwa ajili ya kuilinda cdm au ameajiliwa kwa ajili ya kuwalinda raia na mali zao?.
 
sasa mbona waliodhurika ni CCM, hana hoja huyo ndugu yako, kama walitoa ulinzi kwa nini mtu afe?
 
Kwa hiyo hao polisi wanakwenda kwa staili ya kupiga ramli yaani waliamka tu wakajua kuwa Chadema wanakwenda kumtukana Mwigulu, yaani wewe na huyo ndugu yako polisi na huyu Mwigulu wenu bure kabisa, Mwigulu katunga vimeseji vyake vya kipumbavu kabisa anadai kuwa vimetumwa na Mnyika, hivi hamuoni haya kuzungumza upumbavu kama huu?
 
​panadol zinapunguza maumivu kichwa
Hao CDM inaonyesha hawana shukurani ,na hapo hawatoki kama waliwavuka polisi na kuingia majumbani kuanza kuua ,ni bora wanemuua huyo polisi kuliko kuingia majumbani kama wanasaka ndezi ,ni hatari sana kuwa na vyama aina hii ,viongozi wanashindwa kuwadhibiti wanachama wao ,na ukiona hivyo ujue hakuna chama hapo.
 
Uelewa wangu ni mkubwa sana Jogi, just PM me. Kikubwa sikatai kwamba hatakiwi kwenda kule ila kumbuka tayari walishakwaruzana Bungeni na wana kesi tayari sasa ile kwenda kwa Mwigulu kwa wakati huu ni kama kuchochea moto wa ugomvi kwa petroli. Ukweli uliopo ni kweli kabisa polisi walijitahidi sana kuwalinda akina Mnyika, hiyo ni kweli kabisa kwa sababu licha ya kuongea na askari aliyekuwepo pale nimeongea hata na mzee mmoja jirani sana na nyumbani kwa mwl ambapo mauaji yalifanyikia. Ukweli CCM watakuwa wameanzisha fujo za SIKU HIYO, lakini sio kwamba hiyo ilianzia hapo. Mnyika hakutumia hekima, na naamini toke ameshinda ile kesi ya ubunge Mnyika amekuwa na mambo ya juu juu tu, mimi nina marafiki waliompigia kura na wanampenda sana lakini wanakubali kwa sasa anaokesea.

Kwanza tuwe na uelewa Mmoja, mwigulu hana jimbo, wala hamiliki jimbo lolote tanzania, iramba magharibi ni ya wanyiramba/wanairamba na sii vinginevyo, ni kosa la karne kwa mwigulu kuwakaririsha wapiga kura wa iramba kuwa lile ni jimbo lake, akumbuke hata alivyomchezea rafu Juma kilimba wakati wa majumuisho ya kura za wana-ccm ni nini kilifanyika makuunda, juma kilimba alikuwa anaongoza karibu kata zote! Kwa kusaidiwa na makamba seniour wakabandika figure kubwa ya voters kwenye kata yake na kuonyesha amepigiwa kura nyingi kwa uwiano wa kumpiku jk (juma kilimba) ambaye naye alikuwa hakubaliki na majority ya wanairamba/wanyiramba, laiti jk anguwa anakubalika naamini ccm wangetoana macho. Kuweni na hoja mtakazowashawishi watanzania wawaunge mkono kwazo!
Mnataka wanyiramba waonekane ni maadui kama si vituko kwa jamii ya watanzania,

1) mwigulu "eti msomi, hapo ana masters akiwa professor" wakati elimu yake utata from the biginning!! "clasified mwongo, posible mwizi, confirmed mtoa rushwa, rumors killer" ameanza kuzoea kuteta teta na watumishi wa mungu. Chukueni hatua!!!!

2) jairo "no dought rushwa"

3) nalaila kiula (ingawa mahakama ilim-clear)

4) amos makala "huyu sijui kule turiani kama aliondoka salama bila ku-base upande wa wafugaji kwenye ule mgogoro"
 
Vizuri sana, anyway nafikiri unajitengenezea njia wewe, hamna mtu asiye na mapungufu yake. Wakati hujatokeza hatuwezi kujua ulivyo, hebu jaribu kutafuta huo ubunge kama hatutajua mengi kuhusu wewe. Sipingami na wewe yawezekana ni kweli elimu ya Mwigulu ni utata huko mwanzoni lakini hilo haliondoi ubunge wake wa sasa, unless otherwise. Nafikiri pia jukumu la kupata mbunge mzuri sio langu tu bali ni letu wote kama Wanairamba makini, yamkini ungetokeza wewe nafikiri ningeweza kukuunga mkono, lakini pia nadiriki kusema yawezekana wewe ni mzuri zaidi katika kukosoa, Mayu Dr Kitila Mkumbo's type.
 
Maayu, mimi sina hata mzuka wala ndoto za kugombea ubunge, naamini kabisa kuwa tanzania haiwezi kunikubalia kupanga bajeti kulingana na idadi ya watu kwenye eneo husika, kutoelekeza wingi wa fedha mijini bila uwiano sawia na vijijini ambako toka zamani ndiko kwenye wananchi wengi zaidi, nina amini kuwa shule na hospitali za serikali zapaswa kuwa the best kwa mtizamo wa kitaifa, ingekuwa marufuku kuajiri mtumishi wa serikali ambaye hakusomea shule za serikali toka chekechea hadi kidato cha sita, mtaala wa masomo kwa shule za tz lazima uandaliwe na magwiji watanzania ambao utatumika nchi nzima, kama ambavyo hapo zamani kidogo ilivyokuwa (kwa mfano ukianzisha shairi la "karudi baba mmoja . . . . .wanaweza kuimba wote wanaokukabili) hiyo ndiyo picha yenye taathira ya umoja wa kitaifa, tu kwa kutolea mfano (sio umoja kwa mwavuli wa chama, mbaya zaidi chama chenyewe ccm)
Nafurahi pamoja nawe kwa uelewa mmoja juu ya uongozi, kwani hata akosoaye aongoza, inakuwa raha kama akosolewaye anakubali kukosolewa, jambo ambalo Mwigulu ame-prove failue, mpaka sasa hajui adui yake na wananchi anaowawakilisha bungeni ni nani, anadhani na kuwaaminisha wanyiramba kuwa adui yao ni chadema, (kyolo lya mpununu udu paasyo)
amebakia kuwagharimia wanamakunda kufanya mazoezi na kuimba eti hatuwezi kurithiwa (sika kushaalwa . . . . . .lwa munansakanka uluuuu uuu!)

Lae kate mwaazikyelwa uugole ne masalla ne manatuulu!!!!!!
Mwambieni mwigulu aachane na chadema, ajikite kwenye kuielekeza serikali inayoundwa na chama chake (toka bunge limeanza akisimama kuchangia yeye ni chadema tu, kila kitu chadema tu, wanyiramba hawakumtuma kupambana na chadema bungeni) akiisimamia serikali kisawasawa + uchumi anaotuambia anaufahamu atawanyima chadema cha kukosoa, na hapo kwa usimamizi makini wa fedha zipelekwazo halmashauri ya iramba ni lazima wananchi wataona tofauti,
kama tunataka kuwa wanyoofu tutaishi kwa kusaidiwa na mifano, alikwisha futiwa vyeti aliyejulikana kwa kina la "kihiyo" nyakati hizo, kama vipi tuutafute msumeno uliokati mti "kihiyo" tuutumie kwa mwigulu
mkuu ujue hii sheria ya kuzuia kukariri darasa la saba imewatoa nje ya shule watu ambao haiyumkini wao wangekuwa faida kwa nchi, kwa hiyo mwigulu siyo spesho kwa nchi hii, kupata mamlaka makubwa ya kiserikali umepaswa kuwa mkweli kabisa ref. Jackob zuma, ni utumishi tu uliotukuka, huyu mwigulu kama alianza kutudanganya akiwa kinda, hapa ukubwani inakuwaje, tunapona vipi + hatuna elimu ya uchumi aliyonayo.
NDIO MAANA ANAWAPELEKAPEKA MPAKA MNAANZA KUTETEA DHAMBI YAKE YA UUAJI NA DAMU INAYOMLILIA MWIGULU ISIJEWAUNGANISHA NANYI, JITENGENI MBALI NA UOVU HUU.
 
Kuwalaumu polisi ni kuwaonea bure kwa yaliyotokea Iramba. Wakulaumiwa ni wanasiasa na washabiki wao.

Nimefika kijiji cha Ndago ulipofanyika mkutano wa CDM na kutokea mauaji ya Yohana Mpinga baada ya kukimbilia kwenye nymba ya John Chume iliyo kama mita 200 kutoka uwanja wa mkutano.

Ingewezekana vipi askari polisi 7 kuzuia idadi kubwa ya washabiki wa vyama viwili pinzani ambao tayari walishaanza vurugu? Kulikuwa na haja gani ya wana ccm kuvamia mkutano wa cdm? Kulikuwa na haja gani ya kumfukuza marehemu Yohana peke yake kwa lengo la kumuua? N.k.

Polisi walitimiza wajibu wao kama polisi na kama binadamu. Polisi wana haki ya kuishi kama watu wengine, so kitu cha kwanza ni kuhakikisha usalama wao kwanza.

Kila mmoja wetu achukue jukumu la kumuelimisha jirani yake juu ya kuvumiliana katika mambo ambayo tunatofautiana kimtazamo ili kuepusha maafa na lawama zisizokuwa za msingi kwa jeshi la polisi. Hakuna asiyejua kuwa polisi wanafanyakazi katika mazingira magumu na kipato haba.

Una habari wakati huu wewe uko nyumbani kwako unabofya kwa raha mustarehe, polisi wako mitaani kupambana na vibaka na majambazi? Wewe unalala usingizi wenzako wanateswa na baridi ili wewe ulale kwa amani.

Mwengine mwenye mtazamo finyu atauliza y uhalifu unatokea. Inabidi utokee coz polisi ni wachache na hawawezi kuwa kila mahali kila wakati.
 
nyie watu tumieni busara kidogo kabl ya kuandika utumbo hapa kwa sababu tu za kishabiki, huwezi kusema eti polisi walijua CDM watatukana kwenye mkutano wa hadhara, maana CDM wanayo mengi sana ya kusema jukwaani kuhusu udhalimu wa ccm, na ccm kwa kujua hilo ndo maana wakaandaa kikosi cha kuvuruga mkutano ili wananchi wasielezwe ukweli unaowafanya waendelee kuishi maisha hayo magumu wanayoishi sasa na badala yake ni kwamba Polisi walijua kwamba ccm watavuruga mkutano huo na ndio maana waliwalinda hao wavamizi wa mkutano wakifanya vurugu zilizosababisha maafa hayo... wewe unaesimuliwa na eti askari aliyekuwepo hapo mimi nakueleza ukweli nilouona na macho yangu nikiwa kwenye mkutano huo nakiri kuwepo ushirikiano mkubwa kati ya polisi na wavamizi hao wa ccm waliokodiwa kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo dar.
 
nakubaliana nawe kuwa wakulaumiwa ni wanasiasa, lakini kwa hali halisi huwezi kuwakwepa polisi kwa yaliyotokea Ndago siku hiyo, walipewa taarifa na viongozi wa CDM kuwa kuna njama ya kuvuruga mkutano ule,,,na kweli baada ya dakika chache watu wachache wakaanzisha vurugu ambao ilikuwa ni rahisi sana kwao kuwatuliza au kuwaweka ndani ili kuepusha vurugu zaidi, lakini hawakufanya hivyo na kuwapa vichwa wale watu kuendelea na vurugu hizo... kituo cha polisi kipo mita 20 kutoka kwenye eneo la mkutano kitu ambacho kingewarahisishia kazi ya kutuliza ghasia hizo kirahisi... mimi nawalaumu mojakwamoja kwa sababu walifanya kazi za kisiasa badala ya kufanya kazi yao ya kuhakikishia wananchi usalama wao katika mkutano wa hadhara halali.
 
staling kwenye hizi picha za kichina huwa anakufa pia, cdm lazima hili walijue
 
hivi ni kwa nini wanajamii forum most of the time mmekuwa mk-side upande wa cdm hata wakifanya pumba!!!
 
nyie watu tumieni busara kidogo kabl ya kuandika utumbo hapa kwa sababu tu za kishabiki, huwezi kusema eti polisi walijua CDM watatukana kwenye mkutano wa hadhara, maana CDM wanayo mengi sana ya kusema jukwaani kuhusu udhalimu wa ccm, na ccm kwa kujua hilo ndo maana wakaandaa kikosi cha kuvuruga mkutano ili wananchi wasielezwe ukweli unaowafanya waendelee kuishi maisha hayo magumu wanayoishi sasa na badala yake ni kwamba Polisi walijua kwamba ccm watavuruga mkutano huo na ndio maana waliwalinda hao wavamizi wa mkutano wakifanya vurugu zilizosababisha maafa hayo... wewe unaesimuliwa na eti askari aliyekuwepo hapo mimi nakueleza ukweli nilouona na macho yangu nikiwa kwenye mkutano huo nakiri kuwepo ushirikiano mkubwa kati ya polisi na wavamizi hao wa ccm waliokodiwa kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo dar.

Ndg unatakiwa ujifunze busara ni kitu gani. Kama wewe kwa mtazamo wako unaona ni busara kumfukuza mtu mmoja ambae alitahidi kunusuru maisha yake
 
nyie watu tumieni busara kidogo kabl ya kuandika utumbo hapa kwa sababu tu za kishabiki, huwezi kusema eti polisi walijua CDM watatukana kwenye mkutano wa hadhara, maana CDM wanayo mengi sana ya kusema jukwaani kuhusu udhalimu wa ccm, na ccm kwa kujua hilo ndo maana wakaandaa kikosi cha kuvuruga mkutano ili wananchi wasielezwe ukweli unaowafanya waendelee kuishi maisha hayo magumu wanayoishi sasa na badala yake ni kwamba Polisi walijua kwamba ccm watavuruga mkutano huo na ndio maana waliwalinda hao wavamizi wa mkutano wakifanya vurugu zilizosababisha maafa hayo... wewe unaesimuliwa na eti askari aliyekuwepo hapo mimi nakueleza ukweli nilouona na macho yangu nikiwa kwenye mkutano huo nakiri kuwepo ushirikiano mkubwa kati ya polisi na wavamizi hao wa ccm waliokodiwa kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo dar.

Ndg unatakiwa ujifunze busara ni kitu gani. Kama wewe kwa mtazamo wako unaona ni busara kumfukuza mtu mmoja ambae alijitahidi kunusuru maisha yake kwa kukimbilia nyumba kiasi cha mita 200 na kujificha kwenye nyumba, lakini bado akaingiliwa huko huko na kupigwa mawe hadi kukata roho kikatili, kama hiyo kwako unaona ni busara, basi taifa hili liko kwenye hatari kubwa!!! Kwa hilo polisi hawana lawama, waliosababisha kifo hicho watakua na dhima ya kujibu kama sio hapa duniani basi mbele ya Mungu Muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.

Si busara kwa mwenye akili na anaeheshimu utu, na haki za wengine kuhalalisha mauaji ya kijana yule kwa kisingizio cha aina yeyote ile. Damu yake haijapotea bure. Mtawatupia lawama polisi, but remember sio polisi walliompiga mawe na kumuua yule kijana.
 
Back
Top Bottom