Tuliwalinda zaidi CDM - Polisi aliyekuwepo Ndago

Mdwenke

Member
Jul 16, 2012
78
55
Ndugu yangu ambaye ni polisi aliyeshiriki kulinda mkutano wa CHADEMA Ndago- Singida amelalamikia sana lawama zinazorushwa kwao kuwa hawakuchukua hatua zozote za kuwalinda CHADEMA.

Kwa mujibu wake anasema kazi waliyoifanya ni kubwa kuliko inavyofikiriwa kwani ni kweli walishapata taarifa kuwa CDM wanakwenda kumtukana Mwigulu na vijana wa CCM walikuwa wamejiandaa kwamba matusi yakirushwa tu wangejibu mapigo. Ilivyokuwa ni kweli vijana wa CCM walikuwepo mkutanoni na ilipotokea Mwikabe kuanza kurusha matusi wengi wakachukia sana na kuanza kulalama Kinyiramba "mukue, "mukue", "mukue", "mukue", wakimaanisha "apigwe" "apigwe", "apigwe", "apigwe".

Hivyo polisi walijitahidi sana kuzuia wale vijana wa CCM wasiwadhuru viongozi wa CHADEMA waliokuwepo pale akiwepo Mnyiramba mwenzao Mayu Dr Kitila Mkumbo. Ndugu yangu alishangaa sana baadaye kuona kundi la vijana wa CHADEMA waliokwenda kuwalinda ndiyo wanafanya fujo kwa kuwakimbiza wenzao na kwenda kumwuua mmoja nyumba ya jirani na wengine wawili kujeruhiwa vibaya sana.

Ila sasa kibao kinawarudia wao polisi eti walishindwa kulinda mkutano wa CHADEMA, ukweli anasema wasingefanya kazi yao wale viongozi wa CHADEMA wangedhurika sana. Kwake yeye hatakuwa tayari kulinda mkutano wa CHADEMA tena.

Source: Mawasiliano yangu na askari ndugu yangu aliyekuwepo kulinda mkutano wa CHADEMA Ndago - Singida.
 
Hao CDM inaonyesha hawana shukurani ,na hapo hawatoki kama waliwavuka polisi na kuingia majumbani kuanza kuua ,ni bora wanemuua huyo polisi kuliko kuingia majumbani kama wanasaka ndezi ,ni hatari sana kuwa na vyama aina hii ,viongozi wanashindwa kuwadhibiti wanachama wao ,na ukiona hivyo ujue hakuna chama hapo.
 
Ndugu yangu ambaye ni polisi aliyeshiriki kulinda mkutano wa CDM Ndago- Singida amelalamikia sana lawama zinazorushwa kwao kuwa hawakuchukua hatua zozote za kuwalinda CDM. Kwa mujibu wake anasema kazi waliyoifanya ni kubwa kuliko inavyofikiriwa kwani ni kweli walishapata taarifa kuwa CDM wanakwenda kumtukana Mwigulu na vijana wa CCM walikuwa wamejiandaa kwamba matusi yakirushwa tu wangejibu mapigo......
Wangedhurika kivipi wakati umesema kulikuwa na kundi la vijana wa CDM waliokuwa wanawalinda viongozi wao?
 
Hao CDM inaonyesha hawana shukurani ,na hapo hawatoki kama waliwavuka polisi na kuingia majumbani kuanza kuua ,ni bora wanemuua huyo polisi kuliko kuingia majumbani kama wanasaka ndezi ,ni hatari sana kuwa na vyama aina hii ,viongozi wanashindwa kuwadhibiti wanachama wao ,na ukiona hivyo ujue hakuna chama hapo.
ila kuna nini ??
jenga hoja acha kulalama kama mtoto. Wasinge hongwa ili kuvuruga mkutano haya yangetokea sema umaskini unatusumbua ndiyo maana watu wanakufa kwa vijisenti vidogo
 
Hao CDM inaonyesha hawana shukurani ,na hapo hawatoki kama waliwavuka polisi na kuingia majumbani kuanza kuua ,ni bora wanemuua huyo polisi kuliko kuingia majumbani kama wanasaka ndezi ,ni hatari sana kuwa na vyama aina hii ,viongozi wanashindwa kuwadhibiti wanachama wao ,na ukiona hivyo ujue hakuna chama hapo.
Tokea Umeamka Asubuhi unakuja na vithread vya ajabu ajabu kwaajili ya kutafuta vihela vya futari kwa nape lakini mpaka sasa hivi naona bado unahangaika
 
Hiyo ndiyo kazi yake, na alitakiwa kuwazuia wale vijana wa CCM kurusha mawe mbona hawajamkamata hata mmoja? mwambie aeleze vizuri bado hajatukonvince hata kidogo
 
Huyo ndugu yako askari ulitegemea aseme kwamba hawakuwalinda CDM eti?
 
Hiyo ndiyo kazi yake, na alitakiwa kuwazuia wale vijana wa CCM kurusha mawe mbona hawajamkamata hata mmoja? mwambie aeleze vizuri bado hajatukonvince hata kidogo
Mkuu Twigwe mleta thread katumwa na CCM wala hamna polisi aliyelalamika kwasababu wanajua ujinga walioufanya
 
CDM kirekebishe mwenendo wake,laa sivyo kinajipaka kinyesi kwa watanzania ambao walishaanza kukiamini
 
Inaonekana na wewe una akili za polisi uliyeongea naye!
 
Ndugu yangu ambaye ni polisi aliyeshiriki kulinda mkutano wa CHADEMA Ndago- Singida amelalamikia sana lawama zinazorushwa kwao kuwa hawakuchukua hatua zozote za kuwalinda CHADEMA.

Kwa mujibu wake anasema kazi waliyoifanya ni kubwa kuliko inavyofikiriwa kwani ni kweli walishapata taarifa kuwa CDM wanakwenda kumtukana Mwigulu na vijana wa CCM walikuwa wamejiandaa kwamba matusi yakirushwa tu wangejibu mapigo...
...nenda Dar ukasaidiane na Kova kurekebisha hile filamu ya dr Ulimboka alfu ndo mtengeneza hii ya Singida...
 
Kama anayosema ni ya kweli, basi tunategemea kumsikia kuwa ndiye shahidi namaba moja wa sakata hili.
 
Join Date : 16th July 2012
Posts : 10
Rep Power : 303
Likes Received0
Likes Given17
Ndugu yangu ambaye ni polisi aliyeshiriki kulinda mkutano wa CHADEMA Ndago- Singida amelalamikia sana lawama zinazorushwa kwao kuwa hawakuchukua hatua zozote za kuwalinda CHADEMA.

Kwa mujibu wake anasema kazi waliyoifanya ni kubwa kuliko inavyofikiriwa kwani ni kweli walishapata taarifa kuwa CDM wanakwenda kumtukana Mwigulu na vijana wa CCM walikuwa wamejiandaa kwamba matusi yakirushwa tu wangejibu mapigo. Ilivyokuwa ni kweli vijana wa CCM walikuwepo mkutanoni na ilipotokea Mwikabe kuanza kurusha matusi wengi wakachukia sana na kuanza kulalama Kinyiramba "mukue, "mukue", "mukue", "mukue", wakimaanisha "apigwe" "apigwe", "apigwe", "apigwe"....
 
Kauli zake sio za kuaminika kwa sababu inasemekana nao walilipwa ili kuhakikisha mkutano haufanyiki.

Hata hivyo haiingii akilini kusema walikua na taarifa kuwa Mwigulu atatukanwa kwenye mkutano huo.

Kwa namna tunavyolifahamu jeshi la polisi, lingekua na taarifa kama hizo ni wazi wangezuia mkutano huo kufanyika.

Waliruhusu kwa sababu hawakua na taarifa hizo na ndo mana walitumia mbinu nyingne iliyosababisha mauaji!!
 
Goodluck Mwangomango
Natangaza nia mapema: Baada ya kufanya utafiti wa kina na kujiridhisha nimeamua kutangaza nia mapema kwa wanaTunuru wenzangu na kuwa sasa nimejipanga kugombea Ubunge jimbo la Ubungo kupitia Chama CHa Mapinduzi.

Naamini Chama kitaniamini na naami ntashinda kwa kuwa Mbunge aliyeko sasa kashindwa kumaliza na kufanya kazi kama alivyotuaidi na kauli mbiu yake ya "AMUA".

Naamini Mnyika ndiye mbunge dhaifu kuliko wabunge woote wa Upinzani hivyo nguvu kubwa ntaiweka kuhakikisha chama kinaniami na kwenda kuangusha chelewa iliyoegeshwa ukutani(John Mnyika).

Natangaza rasmi kuwa John Mnyika ni Chelewa iliyoegeshwa ukutani, ntamuangusha 2015. Mungu nisaidie

Back
Top Bottom