nimekumbuka mbali sana nilikuwa na safari buti nilizivaa kuanzia darasa la pili hadi la nne haziishi siku moja nikavizia madingi wametoka nikaenda kukitupa kimoja katika shimo la maji machafu ili ninunuliwe chachacha za Burundi.
hahahahaha
sio kma nacheka ila nalia kwa sweet memories za shule.
nakumbuka mara ya kwanza kuvaa chupi ilikuwa nikiwa njuka na chupi maarufu ilikuwa VIP ambayo ukiwa unasukuma soka ikakatika basi itapanda hadi kifuani....
nakumbuka pia ile style ya kuzungusha mkono iliniathiri mno hata mie na ingawa nilikomaa nao nikaingia class kinguvu bila kuandikishwa nilisota darasa la kwanza miaka mitatu (lakini bado naipenda Tanzania).
Kwa wale ambao hatukuwa mamonita najua mnakumbuka matumizi ya upupu na maji ya betri.... ila nilikuwa kiongozi bora sekondari walimu walilia tulipokuwa tunawaaga
Nimesoma yoooote na nimefarijika sana kukumbuka enzi hizo. Lakini furaha yangu haitaweza kamilika bila ya kukumbuka kitabu kinachitwa MWANDANI WA MWANAFUNZI. hiki kitabu kilikuwa kiboko. ukiweza ku-solve maswali yake yaaani wewe ni kwenda sekondari tu.
Wewe Ally,acha utani...
Mie nilianza shule nilinununliwa viatu laba fulani ziliandikwa DH nilikua nataniwa "Dingi Hana uwezo"
Enzi hizo nasoma Zanaki Primary school nakaa Sinza,zile laba chini ni plastic.
Saa sita natoka shule nishakula hela yote ya nauli au ninayo ya kupandia pale manzese Msufini tu inabidi nifanye yellow page mpaka Msufini au mpaka nyumabini.
Sasa laba zile na jua hazipatani unaweka mfukoni unaanza kutembea peku.
Kamanda leo nimekumbuka mbali....Ukija Darasa la Nne ndio unakutana na Kibanga Ampiga Mkoloni, Ndoto ya Kimweri (chifu wa Wasambaa), Mkwawa Shujaa, Barua Kwa Mjomba Mndolwa na Siku ya Gulio Katerero (hadithi ya Kiiza).
Shairi la kitabu hiki linaanza hivi:
KAMA MNATAKA MALI
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
Wakataka na kauli iwafae maishani
Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali
Roho naona yachinjwa, Kifo kimenikabili
Kama mnataka mali, mtayapata shambani
........................................>