Tulipokuwa primary,unakumbuka?

mimi nakumbuka wali na maharagwe wakati wa kufunga shule hasa miditerm.

Halafu kule primary tulikuwa na shemba letu la shule ambapo mahindi na viazi vilikuwa kwa wingi, na sio mbali sana ni pale pale jijini dar. ila sasa nikipita shule ile hakuna kitu zaidi ya uzio wa matofali na watoto waliochoka kisaikolojia.

MUNGAI MUST GO
 
Je Mnakumbuka Mwagano,siku Ya Kufunga Shule,kila Mtu Na Bakora Yake Yaani Ile Kulia Na Kushoto Tawanyika .hapo Basi Mguu Niponye.
 
Duh, Wabongo kwa kumbukumbu siwawezi.
Uliyesema kuhusu mashamba ya shule umenikumbusha miradi ya Elimu ya Kujitegemea (EK), sijui kama mashamba haya yapo hadi leo, maana Kapuya na Mungai wametuvurugia sana shule zetu hizi.

@Katibu Tarafa
Nakumbuka wakati wa kufunga shule tuoikuwa tunadundana sana mangumi, hata bakora sometimes. Yaani ilikuwa noma sana, kiasi kwamba kuna baadhi ya jamaa zangu walikuwa hawafiki shule siku ya kufunga, kwa kuhofia bifu za namna hii. Mambo ya LY yameniacha hoi!

@Msanii
Ni kweli enzi zetu kulikuwa na utaratibu kwa shule kuwapa msosi wanafunzi, sijui sasa. Hata hivyo nakupa pole kwa kusikitikia shule yako, kwamba miradi ya mashamba imekufa na kilichobaki ni uzio wa matofali. Nakuunga mkono katika kumtimua Mungai, na Kapuya pia. Hawa wawili ndio wameua kila kitu wizarani pale, we fikiria mtu na akili zake timamu anafuta UMISHUMTA/UMITASHUMTA. huku ndio kulikuwa na vipaji haswa vya kila kitu, iwe riadha, mpira, kwaya, utamaduni, kuruka viunzi, kurusha mikuki na kisahani nk.

@Gamba
Mchakamchaka upo kwa baadhi ya shule za vijijini, mie nilishuhudia mnamo mwaka 2005 watoto wakikimbia na kuimba nyimbo za Azimio la Arusha (kama lipo), na "Jua Lile Literemke".
Tunatoka mbali.
 
Primary school kabla ya ukaguzi utasikia kiranja akisema

.......Mikono mbele, juu, kando, chini.

.......Shoto kulia shoto kulia, nyumaaaaaaaaaa geuka

......Mguu pandee, mguu sawa,legeza mwili (ukikosea, AJUWA)

......Walio mbele, nyumaaaaaaaaa geukaaaaaa

......Mstariiiiiiiiiiii nyoosha (hapo kila mwanafunzi anajificha mgongoni kwa mwenzie bila kutokeza kichwa)
 
Mguu pandee, mguu sawa,legeza mwili (ukikosea, AJUWA)

Hahahahahaha aiseee umenivunja mbavu na neno "AJUWA"....

Vijijini unaambiwa kuna viranja walikuwa na uwezo wa kumuadhibu mwanafunzi mwenzao kwa bakora, sijui kama bado ipo hii style.
 
Hahahahahaha aiseee umenivunja mbavu na neno "AJUWA"....

Vijijini unaambiwa kuna viranja walikuwa na uwezo wa kumuadhibu mwanafunzi mwenzao kwa bakora, sijui kama bado ipo hii style.

hehehehe, hiyo iliisha siku nyingi mana viranja waliokuwa wanawapa mboko wanafunzi walijikuta wakishindwa kujibu mawe na maembe mabichi yaliyokuwa yanavurumishwa kwao wakati wa weekends.

Ati neno ajuwa linatokana na neno "as you were"
 
Primary school kabla ya ukaguzi utasikia kiranja akisema

.......Mikono mbele, juu, kando, chini.

.......Shoto kulia shoto kulia, nyumaaaaaaaaaa geuka

......Mguu pandee, mguu sawa,legeza mwili (ukikosea, AJUWA)

......Walio mbele, nyumaaaaaaaaa geukaaaaaa

......Mstariiiiiiiiiiii nyoosha (hapo kila mwanafunzi anajificha mgongoni kwa mwenzie bila kutokeza kichwa)
Mkuu umenivunja mbavu sana.nakumbuka kuna kiranja alikuwa ananionea sana kila nikimuona nakosa raha
 
Mie nakumbuka wimbo wa kutoka shule darasa la kwanza na la pili........."sasa, saa ya kwenda kwetu. kwaheri mwalimu kwaheri, tutaonana keshoooooo." Hapo mzee lazima utoke nduki kubwa, ama sivyo yule mtoto gangwe uliyepiga tobo kwenye mpira wakati wa mapumziko lazima atakufanyia.
Pia nakumbuka majina ya walimu mengi yalikuwa ya kidizaini sana kama, Mwl Kazimoto, Mwl Mchele Mahela, Mwl Kagari Kamutuka n.k.
Shule zisokuwa na madawati, basi watoto wanacheza mpira wa kitenesi kwa vichwa ubao ndio goli. Hapo msee "ashikilimu" ice cream ya kwenye kifuko cha plastick ndio dili wakti wa mapumziko.
Asubuhi kunakuwa na bendi ya shule inapiga wakati wa kugaliwa usafi na kwenda darasani basi kama haupo makini kila siku utatolewa mbele aidha kucha ndefu, hujapiga pasi au kola ni nyeusi. Lakini ilikuwa inapendeza sana na wazee shukrani kwa kumbukumbu!!!.
 
Nyie wote mnaonekana kweli ni watoto wa juzi. Mwenzenu nimeenda shule kipindi cha mkoloni mjerumani. Enzi zetu tulikuwa tunafundishwa nyimbo za kijerumani:

Eins,Zwei,Papagei
drei,vier,Grenadier
funf,sechs,alte Hex'
sieben,acht,kaffee,gemacht
neunmzehnm weiter geh'n
elf,zwolf,jungle Wolf
dreizehn,vierzehn,Haselnuss
funfzehn,sechzehn,du bist duss

It's a joke yoh!
Gademu
 
Umenikumbusha ukaguzi, bendi ya shule inapiga na uku kale kawimbo ka "maisha marefu sana, mungu awape ninyi, viongozi tanzania, uhuru mudumishe" kanaimba.

Kudadeki nikisikia ka wimbo haka, naanza kutafuna kucha haraka haraka, wakati mwingine ndo nimetoka haja kubwa sekunde chache tu bila hata kunawa mikono, lakini natafuna kucha kama kawa. duh, maisha safari ndefu!!
 
Someni bila shida................wagagagigikoko na Mfalme Huhihuhihuhi
 
Enzi hizo baada ya kusoma wiki nzima, unatamani jumamosi ifike haraka ili usikilize kipindi cha MAMA NA MWANA, hapo unamkuta yule mama deborah Mwenda akikuleteeni hadithi kemkem.moja ya hadithi iliyokuwa inanikosha ni ile ya IMANI na kaka zake wameambiwa watafute wake, kila mtu katupa mkuki,mwanamke atakayeokota ule mkuki ndo anakuwa mke wako, looh salaale mkuki wa IMANI ukaokotwa na chura. Ilikuwa kimbembe hapo!....
 
Unakumbuka Hadithi ya ua jekundu, unyoya wa kipanga azizi na ile ya mfalme juu aliyetaka kushonewa nguo isio onekana!?....siku hizi NADHANI watoto wapo kwenye luninga wanaangalia cartoons imported toka Hollywood!!!!.
 
Nakumbuka tulipofika darsa la tano tulikuwa kama wanafunzi 12 tulikuwa ni wanachama katika mama na mwana club yetu ilikuwa inaitwa Mwenge club. Hivi hiki kipindi ch mama na mwana bado kipo kweli?.

Elimu ya kujitegemea bwana! (EK)pale shuleni kwetu kila mwanafunzi ilikuwa ni lazima uwe na tuta moja either la mchicha au nyanya,mazao yakikomaa inabidi wewe mwenyewe ununue

Shule yetu ilikuwa iko mjinimjini kidogo lakini nakumbuka tulivyokuwa tukitumwa vitu, Utamsikia mwalimu wa zamu akisema kesho mnatakiwa mje na maua, dumu la maji, jiwe mojamoja, jembe, mfagio, mbolea. Hapo hujabeba begi lako la madaftari. Ole wako usije na hivyo vitu, utakavyochapwa! manake enzi zile kuchapwa ilikuwa njenje siku ukitoka shule hujachapwa, basi siku hiyo utakuwa na bahati kweli

Mnakumbuka wakati wa mapumziko, ukinunua kitu unawahi kusema CHAMKONONI! ili wenzako wasikuombe.

Mi bwana nilikaa kwenye dawati darasa la nne na la saba tu, madarasa mengine yote nimekaa kwenye jiwe au tofali, asubuhi mkiingia darasni unakuta yule njemba mwenye nguvu amechukua jiwe lako, huthubutu hata kusema kitu,inabidi uende kutafuta kiti kingine, jamani nie acheni tu tunatoka mbali.
 
nikianzia darasa la tano, mwalimu wetu wa hisabati akiingia darasani alikuwa akisalimiwa kwa tebe (table) ya tatu hadi ya tisa.

Kuna kile kipindi cha mwisho kujiandaa na mtihani wa darasa la saba, tulikuwa tunahangaika na JIANDAE VEMA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI, tulikuwa tuinaita 'JIANDAE'
 
Apo juu quickmover umeniacha hoi na hicho kijerumani! Hivi wangapi hapa wamejua kama hizo ni namba kuanzia moja kuendelea?

Yaani mpaka machozi yananitoka...ninapoona jinzi elimu ya sasa ilivobakwa...sijui vile vitabu vya mitaala ya zamani vipo wapi....ningekuwa na uwezo ningevirudisha vyote mashuleni!

Siku hizi ndo hakuna EK, michezo ndo wanabeep, matokeo yake watoto wao kwenye TV mchna kutwa! daamn.

Wakuu hamjakumbusha ilivokuwa kazi mkweli kutongozana huko madarasani...hahahah~
 
Mkuu Kasana umenikumbusha mbali sana maana ishu ya tebo ilikuwa soo hasa pale wale walimu wanoko waliokuwa wanavuka hataile tebo ya 12 na kwenda mpaka ya ishirini, maana tebo ya saba, tisa ni noma sasa huko kwenye 13, 17, 19 je?. Oyaa mnakumbuka sayansi kimu, ile ya kutengeneza maakuli skuli halafu mnapata maksi. Pia kun ishu moja huwa inaniboa nikikumbuka mpaka leo; NAMBA Yaani mtu unawahi shule kinoma ili uwe namba moja. Mnakumbuka tobo bao, usiombe hiyo ichezwe darasani wakati nje mvua inanyesha! Mnakumbuka mtihani wa mwisho wa darasa la saba, pale ambapo mnaanza say na hisabati baada ya hapo mnaenda kucheza mpaka mnajisahau mnakuja kuitwa mtihaniiiiiiiiii!!! mnaenda tena mkimaliza the same. HALAFU MWISHO KABISA MNAVUNJA PENI, KALAMU N.K
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom