Tuliowapa dhamana acheni kulala jamani watanzania Tunaisha

Jun 17, 2011
20
5
ni lini Tanzania itaweza kukabiliana na majanga?,tuliowapa dhamana mko wapi wakati hayo yote yakitokea,uzembe wenu unatumaliza watanzania,sioni tofauti na nchi inayoweza kuwapa wananchi wake sumu ili wafe.

Basi jamani mmeshindwa kukagua vyombo vya usafiri, najua pia mnakula karibu na wamiliki wa yombo hivyo basi onesheni juudi za makusudi za kukabiliana na majanga, kweli chombo kinazama majira ya saa nane usiku mnaonekana asubuhi,mnashindwa hata na waandishi wa habari wanawahi katika sehemu za matukio ili waweze kutoa taarifa kwa wakati, Lakini nyie mnashindwa kufika ili muokoe maisha ya watu?.

Janga likitokea mnaanza kukaa ikao a wakati watanzania wnaangamia,sio kila kitu mkae vikao na ziundwe tume mnatafta tu ulaji.
 
aahh inasikitisha sana kwa kweli, huwa wanasubiri janga litokee
ili waunde tume ya kuchunguza chanzo cha ajali.
ipo siku mwisho wao utafika tu.
 
Back
Top Bottom