tuliosoma St. Kayumba tujikumbushie enzi zetu

Mr & Mrs Daudi, Musa, Neema and Baraka

Nakumbuka kitabu cha malenga wapya kuna shairi linaitwa ua

Nakumbuka shairi la sizitaki mbichi hiz

Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
Alitokatoka siku moja..........................
 
andunje na maajabu ya wadudu, sayyid said, kinjektile ngwaru, siku ya gulio katelelo :msela:
 
Mr & Mrs Daudi, Musa, Neema and Baraka

Nakumbuka kitabu cha malenga wapya kuna shairi linaitwa ua

Nakumbuka shairi la sizitaki mbichi hiz

Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
Alitokatoka siku moja..........................

Njaa aliposikia,
Njaa aliposikia,
Sungura nakuambia.
siku hiyo akaenda,
Porini kutembelea,
Akayaona matunda,
mtini yameenea.
Sungura akayapenda,
Mtini akasogea,
Mtini akasogea,
Sungura nakuambia.
malizia hizo beti......
 
zile story za mr&mrs daudi musa, neema, na baraka zilikuwa nzuri saana coz zulikuwa na muendelezo vp story ka kibanga ampiga mkoloni, manenge na madawa , au ile ya babu kunywa chai ya moto wewee ni mtoto mtukufuuu!siafuuu! Wanakusfuuuu dah it was very very fun to read them books
 
Ile story ya yule dogo anayewabeba kuku vichwa chini miguu juu inakumbusha mbali sana halafu walimu wenyewe walikuwa wanakuja wamevaa na sare zao za JKT.

Kabisa hakuna ujinga kabisa gwaride mtindo mmoja! Jamani wale wa Tambaza iliyofungwa tukapotezewa mpo humu ndani.
 
Ile story ya yule dogo anayewabeba kuku vichwa chini miguu juu inakumbusha mbali sana halafu walimu wenyewe walikuwa wanakuja wamevaa na sare zao za JKT. Kabisa hakuna ujinga kabisa gwaride mtindo mmoja! Jamani wale wa Tambaza iliyofungwa tukapotezewa mpo humu ndani.

Yule dogo jina lake anaitwa PAZI
'NAUMIA NAUMIA'
'NIHURUMIE NIHURUMIE'
 
Waliosoma rumuli primary school pale bk watakuwa wanmkumbuka mwal haruna?
 
Me nakumbuka ule wimbo wa saa nne 'wa saa nne makombo wa asubuhi oye oye' halafu inaanza vita ya kutoka arasani kuwapisha wengine. Hii ilikuwa ni kwa darasa la kwanza, pili na la tatu
 
Nilisoma ngarenaro kanumba school ilikuwa inaaminika kwa kutoa makapurwa waosha magari enzi hizo magari yanaoshewa mtoni na kulikuwa na mto hapo shuleni na waosha magari wakipiga msuba wanafunzi walikuwa wanaona ndio ajira pekee na ilikuwa inawashawishi sana kuacha shule na kuingia kwenye ajira chap, pia ngarenaro primary imetoa vibaka na majambazi wengi sana. Ashukuriwe mwalimu mkuu mwaipopo ndiye aliyekuja kuitengeneza ile shule maana alipohamia pale hata jeshi halikuwa hivyo kitu cha kwanza alijenga ukuta kwa kila eneo ambalo mwanafuzi angeweza kupita akaweka sehemu moja tu ya kuingilia na kutoke ambayo ipo karibu na ofisi , kwavile ilikuwa ni shule ya makatili walivunja vioo na madirisha hata yalipowekwa ya mbao yalivyunja mwaipopo akasema isiwe taabu akaziba madirisha yote kwa kuyajengea na tofali nafiki mpaka leo ukienda pale utakuta baadhi ya madirisha yakiwa yamejengewa kwa matofali, ukaanzishwa mchakamcha na kushika namba saa 12 mazee mwaipopo alikuwa anapiga balaa ingawa hata mtangulizi wake malisa alikuwa akikucha lazima uumwe wiki mbili mpaka wanafunzi wakawa wanasema ni sababu ya ulemavu wake wa miguu hivyo nguvu zote zimehamia mikononi, sitasahau vidumu vya kunyeshea bustani na fagio siku hizi sioni watoto wakibeba vidumu na mafagia kwanini? Mwalimu mkita alinisaidia sana kwenye somo la kiingereza.

kama sikosei tiliskuli wote hapo Ngarenaro, hivi ulikuwa A au B?
 
zile story za mr&mrs daudi musa, neema, na baraka zilikuwa nzuri saana coz zulikuwa na muendelezo vp story ka kibanga ampiga mkoloni, manenge na madawa , au ile ya babu kunywa chai ya moto wewee ni mtoto mtukufuuu!siafuuu! Wanakusfuuuu dah it was very very fun to read them books

hahahahaha,nakumbuka aiseee
 
Mr & Mrs Daudi, Musa, Neema and Baraka

Nakumbuka kitabu cha malenga wapya kuna shairi linaitwa ua

Nakumbuka shairi la sizitaki mbichi hiz

Hadithi inayokuja ni ya sungura sikia
Alitokatoka siku moja..........................
kwanza unakuwa umekremisha beti kabla,kwahiyo siku ya siku ikifika unashusha tu mabeti.Mnakuwa tu mnahesabu topics ngapi bado kufikia sizitaki mbichi hizi,ikifika weeee furaha
 
Nakumbuka Masasi mwenzetu mmoja alikuwa hapendi kiingereza na hasa utaratibu wa mwalimu wa somo lenyewe, kila siku kabla ya kuanza somo ni lazima kuanza na imla (dictation) ya maneno kumi, kila kosa moja fimbo moja na bakora yenyewe ina mapanda kwa hiyo two in one mgongoni.

shosti wetu akawa anapandisha mashetani feki kila muda wa kipindi tukiambiwa tumsindikize kwao kila mtu anagombea kwenda ili kupumzikia vipigo. Lakini aaaah kama unajali unamaliza LY yako na cha kuombea maji kidogo kipo.

asante mwl John Chanai aka JC, mwl Maduhu, HR Mtaba, Said Rashid, Mwl Alibu na wengine kibao. Ndwika ya wakati huoooooo.
 
Dah, hii imenikumbusha mbali sana!!! wakija walimu wa upe shule inageuka kambi ya jeshi! Mtawahi namba kwa kengele 3,ya kwanza saa 12 kamili,ya pili 12.15 na ya tatu 12.30.

Ukaguzi wa kidumu cha maji,mfagio na wakati mwingine kuni,mbolea,au maua.
Long time kitambo.....
 
mpiga filimbi wa hamelini, Juma na Roza, hawala ya fedha, Ngoswe... penzi kitovu cha uzembe!
 
Msisahau Kula mbakishie Baba, mnajaza kifusi cha mchanga mnaweka kijiti ktk kimesimama, halafu mnaaza kupunguza mchanga atakae angusha kijiti kichapo cha kufa Mtu!

Nilkula kichjapo kitakatifu Maticher ndio waliniokoa....kwa wadada rede ( Its ready but as you know kayumbas they call it rede....hahahaha!!!!)

Bila kusahau macheck Bobusssss....unaweka handkerchief unaaacha inaning`inia kwa mfuko......raba mtoni....
 
Msisahau Kula mbakishie Baba, mnajaza kifusi cha mchanga mnaweka kijiti ktk kimesimama, halafu mnaaza kupunguza mchanga atakae angusha kijiti kichapo cha kufa Mtu!!! Nilkula kichjapo kitakatifu Maticher ndio waliniokoa....kwa wadada rede ( Its ready but as you know kayumbas they call it rede....hahahaha!!!!) Bila kusahau macheck Bobusssss....unaweka handkerchief unaaacha inaning`inia kwa mfuko......raba mtoni....[/QUOTE]

Umenikumbusha kijana mmoja alikuwa ananipenda mie simpendi kabisa yeye alikuwa ananing'iniza kitambaa kimechorwa chorwa mapicha picha ya kijani njano na nyekundu dahh umenikumbusha mbali nimecheka kweli leo u made my day
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom