tuliosoma St. Kayumba tujikumbushie enzi zetu

Barbie Maliposa

Senior Member
Feb 9, 2011
153
19
Enzi zile 2likuwa 2nasoma vitabu na hadithi kama:
juma na roza (pipiii,simile nipite na motokaa yangu)
sizitaki mbichi hizi
pamela na kipini
bulicheka
fikiri mimi masikini
edina na bustani

Ongeza vingine unavyokumbuka
 
Ngoswe kitovu cha uzembe,alfu lela ulela au siku elfu moja na moja.safari saba za sindibad,
 
Ukiwa mtoto wa mwalimu, basi shambani huendi, hufagii kama wenzako na ni lazima uwe kiranja.
Nilivaa viatu vinaitwa "gogo", jua likiwaka balaa - alafu ili ucheze na wenzako mpira lazima uvue maana wote wapo peku utawaumiza.
 
Musa, Neema, Baraka;
Mr & Mrs Daudi ...

Nilisoma ngarenaro kanumba school ilikuwa inaaminika kwa kutoa makapurwa waosha magari enzi hizo magari yanaoshewa mtoni na kulikuwa na mto hapo shuleni na waosha magari wakipiga msuba wanafunzi walikuwa wanaona ndio ajira pekee na ilikuwa inawashawishi sana kuacha shule na kuingia kwenye ajira chap, pia ngarenaro primary imetoa vibaka na majambazi wengi sana.

Ashukuriwe mwalimu mkuu mwaipopo ndiye aliyekuja kuitengeneza ile shule maana alipohamia pale hata jeshi halikuwa hivyo kitu cha kwanza alijenga ukuta kwa kila eneo ambalo mwanafuzi angeweza kupita akaweka sehemu moja tu ya kuingilia na kutoke ambayo ipo karibu na ofisi , kwavile ilikuwa ni shule ya makatili walivunja vioo na madirisha hata yalipowekwa ya mbao yalivyunja mwaipopo akasema isiwe taabu akaziba madirisha yote kwa kuyajengea na tofali nafiki mpaka leo ukienda pale utakuta baadhi ya madirisha yakiwa yamejengewa kwa matofali, ukaanzishwa mchakamcha na kushika namba saa 12 mazee mwaipopo alikuwa anapiga balaa ingawa hata mtangulizi wake malisa alikuwa akikucha lazima uumwe wiki mbili mpaka wanafunzi wakawa wanasema ni sababu ya ulemavu wake wa miguu hivyo nguvu zote zimehamia mikononi, sitasahau vidumu vya kunyeshea bustani na fagio siku hizi sioni watoto wakibeba vidumu na mafagia kwanini?

Mwalimu mkita alinisaidia sana kwenye somo la kiingereza.
 
Ah? Shule ya Msingi Msasani, nakumbuka Mwl. Doya alinipa kitabu cha Kisiwa chenye Hazina(R. Stevenson), afta skul nikachikichia nacho maze!
 
jaman,don let people cry,wakat huo,majina ya shule yaliyo kwenye vitabu ni MTAKUJA PRIMARY SCHOOL,MAWENZI,KIBO,oh kwa vitabu vya english,WALIMU WA UPE ndo walitamba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom