MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Baada ya awali kusema kwamba Taliban iliundwa na shirika la ujasusi la Marekani la CIA kwaajili ya faida ya Marekani, rais wa Pakistan ameendelea kutoa vijembe kwa serikali ya Marekani.
Akiongea na televisheni ya NBC ya Marekani, Zardari alisema kwamba Osama bin Laden alikamatwa na majeshi ya Pakistani mwaka 2001 lakini Marekani walimuachia huru.
Zardari alisema kwamba majeshi ya Pakistan kwa kushirikiana na majeshi ya Marekani walishirikiana katika operesheni ya kumsaka Osama bin Laden kwenye milima ya Tora Bora.
Zardari aliendelea kusema kuwa wakati wa operesheni hiyo majeshi ya Pakistan yalimkamata Osama bin Laden na kumkabidhi kwa majeshi ya Marekani lakini majeshi hayo ya Marekani yalimuachia huru.
Zardari alisema pia kwamba haamini kama Osama bin Laden ambaye alikamatwa miezi mitatu baada ya mashambulizi ya septemba 11 yuko hai hadi sasa.
Ni miaka minane sasa CIA haijapata habari zozote kuhusiana na Osama bin Laden na hata hivyo Marekani ilishatupilia mbali mipango yake ya kuishawishi dunia iamini kwamba Osama bin Laden amejificha kwenye milima ya Tora bora.
Pakistan imekuwa kwenye shinikizo kubwa toka kwa Marekani ambayo imeitaka Pakistan itokomeze majeshi ya Taliban ambayo yanajiunga upya kwenye miji iliyopo kwenye mpaka wa Pakistan na Afghanistan.
Source:http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2033078&&Cat=2