Tulikwenda kupigana msumbiji kama nani!!

Hata nami pia hapo nilipashangaa kidogo.Sijapata kuona askali anahoji kamanda wake. Huyu labda alikuwa mgambo wa jiji wale wanaonyang'anya akinamama vitumbua na chai kisha wanakula wao.

Nafikiri huyu alikuwa "TUSAMINIWE" (Wa magwanda ya kijani na michirizi miyekundu
 
quote_icon.png
Originally Posted by Amiliki
Mwaka 1975 Baada ya kurudi kutoka katika Vita vilivyomwondoa Mreno Msumbiji tulikusanyika pale Lugalo Jeshini ambapo Mwalimu JK Nyerere alikuja kutupongeza kwa Ushujaa uliomwondoa Mreno .
Katika Hitimisho lake Mwalimu akasema, Mashujaa Mmerejea tunawapokea kwa Shangwe na
HATUNA CHA KUWAPA, CHA KUWAPA NI ASANTE

Nakumbuka yule kijana aliyesimama na kumuuliza Mwalimu akitaka kujua kama tulienda kupigana Msumbiji kama Askari wa Kukodiwa na kama ni Askari wa kukodiwa tulipaswa kulipwa au tulienda kupigana Msumbiji kama ni Sehemu ya Tanzania, basi Tuonyeshwe mipaka ya Tanzania!

Huo ndio ulikuwa mwisho wa kumwona yule kijana mpaka leo na Wanajeshi wengine wakafyata japokuwa hakuwa amepanga peke yake kuuliza maswali yale!




Si hayo yameandikwa hapo? Ama kweli wewe Bujibuji. Mwandishi alikuweko kwenye tukio, si kasema "tulikusanyika", "Nyerere kaja kutupongeza", "nakumbuka yule kijana"? Ujinga ni kukataa ukweli ulio dhahiri !

Kama kuandika hapa tu kunamfanya mtu awe mkweli then na mimi ngoja niandike.

Na mimi nilikuwepo, hilo halikutokea!

Sasa niambie, nani kati yetu kasema ukweli? (Na kumbuka WEWE binafsi hukuwepo)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom