Tulifanya kosa kumpa urais Mkapa

Ukweli ni huo kuwa ilikuwa makosa makubwa kuirudisha ccm madarakani wakati kulikuwa na fursa ya kuiweka pembeni... Na kwa nchi hii uchaguzi wowote unaoirudisha ccm madarakani itaendelea kuwa kitanzi bila kujali nani ni rais.Siku watanganyika watakapouweka madarakani utawala tofauti na ccm ndiyo siku watakuwa wamerudisha mikononi mwao madaraka ya kubadilisha serikali yoyote itakayoleta uhuni au itakayoshindwa kufikia matarajio ya wananchi. Raia wakiwa na uelewa/uwezo wa kuiweka ccm pembeni, serikali zote zitakazofata zitashika adabu na zitawajibika kwa wananchi.
 
- Eti did I read it right, kwamba tulifanya makosa kumpa urais ni kweli wewe na mimi ndio tuliompa huo urais? Just curious!

Es!

Swali lako zuri mimi nadhani na wewe hatukumpigia kura aliwekwa na system, ilikuwa si kura ilikuwa beyond kura
 
Urais kapa mlipa nyinyi? kwanini mleta mada unatafuna maneno? sema tu "aliyefanya Makosa aliyempa Urais Mkapa" si inamjuwa aliyempa Urais ni nani? au ulikuwa bado una nyonya?

Nyerere!
 
Ndugu,

Lyatonga alipewa ila kura hazikulindwa. Sio tu mimi peke yangu hata wewe ulaumiwe kwanini hukulinga kura yako.
 
Mkapa alianza na kuuza mashirika ya umma kwa shilingi moja na kusababisha ajira kupungua kwa kiasi kikubwa.
Kiongozi bora ni yule anayeongeza ajira na kujenga viwanda zaidi. Aliwachukia wafanyakazi wa mashirika ya umma na kuyaacha mashirika yajifie yenyewe bila kujali namna watu wachache walivyoharibu miundo mbinu ya mashirika hayo kwa kuiba.
Alikuwa sawa na mtoto aliyerithi mali nyingi toka kwa marehemu baba yake ambaye badala ya kuziendeleza mali zile aliona ni upuuzi mtupu kuwa nazo na badala yake alianza kuziuza ovyo.
Alileta madhara makubwa sana hasa kwa wafanyakazi waliofukuzwa kazi wangali vijana kwa baada ya mashirika yao kuuzwa.
 
Kosa lile lilikuwa kubwa sana ambalo madhara yake yatalikabili Taifa hili kwa muda mrefu. Mrema angechukua nchi wakati ule hali ya uchumi, utamaduni, uzalendo na uwajibikaji vingekuwa vya juu sana kulinganisha na sasa ambapo hali ni mdembwedo!
 
Mtoa mada wait please; Ni lini sisi wadanganyika tumewahi kumchagua rais?. Maraisi wote tumekuwa tukichaguliwa. Tulipojaribu kuchagua mzee wa kichaga na Dr. tukasikia kura zimeibiwa. Katiba inasema hakuna kuhoji matokeo ya raisi. Sisi bado tupende tusipende bado tunatawaliwa mpaka hapo ukombozi kamili wa mtanzania utakapokuja.
 
He wasn't, sera yake ya ubinafsishaji imekuwa ni kichaka cha ufisadi tz. Alijinufaisha yeye na sumaye tu unakumbuka wananchi walikuwa hawamtaki sumaye kwa kuwa hakuwa muadilifu lakini alimg'ang'ania mpaka mwisho na yeye akaja akajichafua. leo hii ukienda mtibwa na turiani mkapa na rafiki yake sumaye wana mashamba kama vijiji
....Eeee! si ndio waliosema kua waTanzania tutakula majani lakini ndege ya Rais ni lazima inunuliwe?
 
Nyerere ndio alisababisha haya!

well said....alikuwa ni chaguo la mwalimu na alipigiwa kampeni na mwalimu

che Nkapa was nobody back in 1995 na kama isingekuwa nguvu na ushawishi wa mwalimu...leo tungekuwa na historia tofauti na hii ya akina ANBEM, KIWIRA, ALEX STEWART, NET GROUP etc.
 
Hembu advise mlitaka afanyeje??

Alitakiwa ayafanye haya anayoyapigia kelele saiv (rejea hotuba yake ya kwenye Kigoda cha mwalimu)

Alitakiwa ajenge uwezo wa Watanzania badala yake akabeba bango kuwatukana.

Alitakiwa kuwajengea Watanzania morali kwa kuwashehenesha na maono yake, badala yake hadi leo hamna mtanzania masikini aliyependa na kunufaika na utandawazi.

Tuache kulewa na ujasiri wa simba katika kuunguruma wakati katafuna watoto wake, watu wengi "makini" wanayumba na ujasiri wa Mkapa katika kujenga hoja na kuchambua current issues matokeo yake wanabebwa na huruma katika kuchambua Uongozi wake!
Ila sio Mimi.
Kwangu Mkapa ataendelea kuwa Mpuuzi fisadi kama walivyo mafisadi wengine tu tena ye namtunukia ukinara na uasisi wa ufisadi mkuu wa pili wa taifa hili (ukiwaondoa wale wa kwanza walioua Azimio la Arusha)....

Nyie mnaobeba bango la Mkapa mtuambie ni kwa kiasi gani amejenga taifa la "JUJITEGEMEA"?! (achilia mbali ujamaa)

Je mnakumbuka kuwa alikiri kwa kinywa chake kuwa "alikisahau kilimo"??
Sasa tumuweke wapi huyu mtu??
Nini yalikuwa maono yake juu ya hili Taifa??

Mnaomtetea kuhusu ubinafsishaji ila ye kashindwa kujibu maswali ya Shivji kuwa ubinafsishaji wa njia kuu za uchumi kama BIMA na BANKS ilikuwa ni kulipeleka taifa golgota!!

Namalizia kwa kusema kuwa tusijipe moyo kwa kuangalia matapishi yaliyo na afadhali, matapishi ni matapishi tu sababu yote ni najisi kwa utakatifu wa Taifa,
hili taifa halijawahi kuwa na KIONGOZI toka mwaka 1985!
 
Mkapa hakustahili kuwa Rais wa Taifa la wapumbavu kama hili huyu ****** ndo stahili ya watu nyie mnaopenda kufanya SIASA kama burudani,kwani kwenye CABINET ya Mkapa JK ndo alikuwa best wao? even LYATONGA mlimkataa kwa chuki za kijinga,akitoka huyu mpeni MEMBE mpaka mtie akili!
 
Ndiye baba wa ufisadi huu tulionao tokana na malezi yake.

Utakuwaje baba wa mafisadi kama wewe si fisadi? Tafakari. Hivi majambazi yanapokamatwa wazazi wao ndio wanaolaumiwa kwa kuwa watoto wamegeuka kuwa majambazi?
 
Mkapa hakushinda uchaguzi wa 1995. Hata yeye analijua hilo. Uchakachuzi wa NEC haukuanza 2005.
 
Nadhani sehemu kubwa ya watanzania tuna matatizo makubwa sana! No wonder hadi leo yaani miaka 50 baada ya uhuru bado tunamlaumu mkoloni kwa kutufikisha hapa tulipo, haya Mkoloni akaondoka akaja Mwalimu J.K.Nyerere nae ameendelea kulaumiwa na baadhi ya watu; Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa mkawaungisha tela hilo hilo na sasa Mko na Mh. Dr. Kikwete! Cha ajabu hakuna hatua zozote madhubuti zilizokwishawahi kuchukuliwa ili kumaliza hayo mnayoyazungumza.

Kama tunataka kuleta mabadiliko tuyafanye kwa vitendo full stop sio kulalamika tu miaka inakwenda, Nyumba za Serikali zikauzwa (to me it was a deadly mistake) sasa tufanye nini, Tuzirudishe kwa namna yoyote ile la kama hatuwezi (kitu ambacho siamini) tujipange upya tujenge zingine, hayo mashirika tunayolalamikia kugawawiwa bure tuchukue hatua na kufunga huo ukurasa! Kwa utamaduni huu wa kulalama bila kuchukua hatu No wonder in the next 50 yrs utakuta vitukuu na vilebwe vyetu vikaendelea kumlaumu mkoloni na hao wengine huku nchi inaendelea kuoza. Tuamke, Tuchukue hatua za kukomesha upuuzi wa ajabu ajabu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom