Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
Dark City,
Kweli kabisa maneno yako lakini pamoja na kuwa na viongozi wabaya huoni kwamba kuna umuhimu wa sehemu hiyo kutojengwa vibanda na kuanzisha biashara haramu za viwanja wakati tuna matatizo mengi..
Mkuu Hata nyumba za Msajili na NHC zinauzwa leo hii kwa mabillioni wakati serikali inapokea vijisenti..Binafsi kama kuna kiongozi ataingilia kati na kusimamisha uuzaji wa nyumba hizi ama ubadilishaji wa mikono ktk nyumba hizi na kutazama upya mpango wa upangishaji na pengine uuzwaji wa nyumba hizi nitapongeza hatua hiyo pamoja na kwamba kuna watu wamekwisha piga mahesabu yao.
Kesho tunaweza kabisa kumweka mtu kiti moto na kumuulizia KULIKONI badala ya kuacha swala zima kila mtu anaingiza mkono wake. Mama Mkapa amekuwa na nguvuna nyumba za serikali kuliko hata Msajili wenyewe.
Kundi dogo la watu ambao hawana hata madaraka serikalini ndio vinara wa uuzaji wa nyumba hizi wakati hawana hata mchango wa senti ktk ujenzi ama sheria andamizi ya Utaifishaji..
Hadi sasa hivi mkuu, viwanja vya Kigamboni vimetolewa kiholela, mimi binafsi niliambiwa nitume dollar 3,000 nipatiwe kiwanja beach nikashtuka kwa sababu sikuamini kabisa kwamba serikali inaweza kutoa viwanja vya beach bila kuona mjengo ama dhumuni la maombi ya kiwanja hicho..Mji haujengwi kwa kutoa vibali na hati bila kufuata ramani iliyopo mezani..Na sidhani kama tunayo ramani ya mji wetu kwa miaka 10 au 20 ijayo!.. hivyo, nilijua kuna namna pamoja na kwamba ningepewa kibali na pengine kuchukua hata Hati ya kumiliki lakini kisheria utaratibu ulotumika unanifungia kanyaboya..
Kweli kabisa toka mwinyi, Mkapa hadi leo Kikwete kumekuwa na utapeli mkubwa toka kwa viongozi wetu lakini kuwepo kwa viwanja hivyo chini ya serikali kunatupa muda na wasaa wa kuwaondoa CCM madarakani na serikali mpya ikaweza kutumia haki hii kuijenga tanzania tunayoitaka badala ya kurudi tena ktk sheria za Utaifishaji baada ya ujenzi mbaya.
Mkuu Mkandara hatutofautiani kitu kuhusu haja ya kuwa na míji iliyotengezwa kwa mpango badala ya kuwa na miji ambayo inakua kama ni ajali ajali vile(unplanned). Ila hatuna watu wakutufanyia kazi hiyo kwa sasa. Kwa sababu hatuna serikali yenye bongo inayoona mbele. Na maadamu hatuna kitu kama hicho (serikali) ambacho ni muhimu katika kubuni mipango na kuisimamia kikiwa na baraka na imani ya wananchi basi tuiache ardhi ikae kama pori. Kwani itaoza?? Mbona Mwalimu JKN aliacha madini yetu kwa sababu kama hizo. Kama isingekuwa hii mibaka uchumi si wangekuja kufaidi wajukuu zetu?? Hata miji itajengwa tu, ama na kizazi chetu au kijacho.
Jambo ambalo sitaki ni kuibiana kimacho macho kama ambavyo wizara ya ardhi (na serikali kwa ujumla) inafanya sasa.