Tulichosema kuhusu Kigamboni kimetimia: Tukimbilie wapi?

jamani kweli hata mimi nimesikia hivyo.... mwenye habari atuambie jamani mali zetu wanataka kutuzulumu......
 
Eneo wanalochukua including na lile la mradi wa viwanja 20,000 ? Naomba mtuhabariboshe......Hilo tangazo hamuwezi ku-scan mkatuwekea hapa?
 
Nini malengo ya serikali katika hili? Kwa idadi kubwa ya watu ilivyo sasa (hata kuboresha miundo mbinu inakuwa vigumu), ningetarajia mpango huu wanaotaka kuufanya Kigamboni waufanye Kibaha, Bagamoyo au sehemu nyingine ili kupunguza mwongezeko wa watu wanajazana Dar es Salaam.





.
 
taarifa isiyo rasmi kwa upande wangu ni kwamba serikali itachukua eneo lililo karibu na feri, eneo hili linachukuliwa kwa ajili ya kupanua miundombinu kama vile barabara na uboreshaji wa ramani ya sehemu husika. Hii imelenga kugeuza eneo husika kuwa na mtazamo wa kibiashara zaidi. Hivyo eneo la mradi wa viwanja 20,000 halitahusika katika kurekebisha muenekano wa Kigamboni.

Binafsi sioni kama ni vibaya,iwapo wananchi wanaomiliki maeneo hayo watahusishwa katika zoezi kikamilifu.
 
Maeneo yatakayohusika yako katika Kata za Mjimwema, Kibada, Vijibweni na Kigamboni na itahusu maeneo yafiatayo:

1. Kaskazini kuna Bahari ya Hindi kuanzia Feri ikijumuishwa na visiwa vya Kendwa na Sinda ndani na nje
2. Magharibi kuna bandari ya Dar
3. Kusini magharibi kuna bonde la Mto Mzinga
4. Mashariki eneo la Mwera
5. Kusini kuna mto Kizinga na eneo linalopakama na Wilaya ya Mkuranga

Eneo litakalochukuliwa na Serikali litakuwa na ukubwa wa hekta 5533 (Ekari 13,832.5).

Kwa mujibu wa Tamko uendelezaji wa maeneo yaliyo katika wigo huu umesitishwa, kasoro maeneo yaliyo kwenye mpango wa viwanja 20,000.
 
Tamko hili halitahusu viwanja 20,000.

Duh, mimi nina ka-plot kangu ambako hakajapimwa just nearby eneo la mradi wa viwanja 20,000 pale Mjimwema na nlkuwa nawaza kuanza kujikongoja kujenga hata kibanda sijui itakuwaje maskini.
 
Bunge limeanza kikao chake sasa. Na sisi kwa heshima na taadhima tuansema hivi:

'Tunamtuma mbunge anayehusika na eneo la Kigamboni kwenda kusema wananchi wa Kigamboni wanadai hati zao za ardhi ikiwezekana kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Tumechoka kuibiwa, tumechoka kufisadiwa. Au mnatuona bado tunatabasamu mnadhani tunawapenda.

Wabunge tafadhalini aste aste hao jamaa serikalini hapo Ardhi na wajomba zao wa CCM wasithubutu kututia kidole jichoni eti....'

Mlalahoi Kigamboni
 
Maeneo yatakayohusika yako katika Kata za Mjimwema, Kibada, Vijibweni na Kigamboni na itahusu maeneo yafiatayo:

1. Kaskazini kuna Bahari ya Hindi kuanzia Feri ikijumuishwa na visiwa vya Kendwa na Sinda ndani na nje
2. Magharibi kuna bandari ya Dar
3. Kusini magharibi kuna bonde la Mto Mzinga
4. Mashariki eneo la Mwera
5. Kusini kuna mto Kizinga na eneo linalopakama na Wilaya ya Mkuranga

Eneo litakalochukuliwa na Serikali litakuwa na ukubwa wa hekta 5533 (Ekari 13,832.5).

Kwa mujibu wa Tamko uendelezaji wa maeneo yaliyo katika wigo huu umesitishwa, kasoro maeneo yaliyo kwenye mpango wa viwanja 20,000.

Kibada block '9' iko kwenye huo mradi???? mwenye data
 
Wakuu,
Mtanisamehe sana lakini mimi binafsi nakubaliana na maamuzi ya serikali..Mji wowote ni lazima upimwe na kuweka ramani ya mji mpya iwe kwa matarajio ya mwaka 2050 au zaidi. kama sehemu hizo zimepewa hati ovyo ovyo bila kufuata ramani ya mji ktk mapanuzi yake ni lazima serikali ichukue hatua mara moja kabla ujenzi na kuwagharimu wananchi ktk utapeli uliofanyika..

Nimekuwa nikiutazama mji wa Dar ktk baadhi ya Picha nikaona kwamba mji wetu hakika ni mzuri sana kibiashara isipokuwa tumekuwa kukichuachua kutazama maslahi binafsi..
Na ni katika kutazama mji wetu nikapendekeza hata bandari yetu iondolewe pale na mji upanuke kuelekea Kurasini na kuzunguka hadi pwani ya Mbagala..kwa sababu sioni sababu kabisa ya kuendelea kuboresha bandari ambayo inaweza kuruhusu Meli moja tu kuingia kwa kila msafara.
Ni sawa na kuwa na International Airport ambayo ina runway moja tu.. Upana wa majengo na kadhalika hauwezi kubadilisha ukweli kwamba ni ndege moja tu inayoweza kutua kwa wakati mmoja.

I WISH ningekuwa Mayor wa jiji la Dar...
 
Wakuu,
Mtanisamehe sana lakini mimi binafsi nakubaliana na maamuzi ya serikali..Mji wowote ni lazima upimwe na kuweka ramani ya mji mpya iwe kwa matarajio ya mwaka 2050 au zaidi.kama sehemu hizo zimepewa hati ovyo ovyo bila kufuata ramani ya mji ktk mapanuzi yake ni lazima serikali ichukue hatua mara moja kabla ujenzi na kuwagharimu wananchi ktk utapeli uliofanyika..

Sidhani kama kuna raia yeyote wa Tz ambaye angepinga serikali kuboresha mji (iwe Dar au kwingine) kama kweli nia ya serikali ingekuwa ni kuuweka mji uwe wa kisasa. Kwa hali ilivyo ni kuwa (hata kiwa na nia nzuri tu) hakuna atakayeiamini serikali kwa sababu imeshapoteza imani (credibility) yake kwa wananchi. Kwa hiyo kila kitu kinaonekana ni usanii. Hata hivyo sina shaka kuwa mpango huo (hata kama ni mzuri kiasi gani) ni mwendelezo wa usanii ule ule. Hapa ni kuwapiga wananji changa la macho tu!
 
Dark City,

Kweli kabisa maneno yako lakini pamoja na kuwa na viongozi wabaya huoni kwamba kuna umuhimu wa sehemu hiyo kutojengwa vibanda na kuanzisha biashara haramu za viwanja wakati tuna matatizo mengi..

Mkuu Hata nyumba za Msajili na NHC zinauzwa leo hii kwa mabillioni wakati serikali inapokea vijisenti..Binafsi kama kuna kiongozi ataingilia kati na kusimamisha uuzaji wa nyumba hizi ama ubadilishaji wa mikono ktk nyumba hizi na kutazama upya mpango wa upangishaji na pengine uuzwaji wa nyumba hizi nitapongeza hatua hiyo pamoja na kwamba kuna watu wamekwisha piga mahesabu yao.

Kesho tunaweza kabisa kumweka mtu kiti moto na kumuulizia KULIKONI badala ya kuacha swala zima kila mtu anaingiza mkono wake. Mama Mkapa amekuwa na nguvuna nyumba za serikali kuliko hata Msajili wenyewe.

Kundi dogo la watu ambao hawana hata madaraka serikalini ndio vinara wa uuzaji wa nyumba hizi wakati hawana hata mchango wa senti ktk ujenzi ama sheria andamizi ya Utaifishaji..

Hadi sasa hivi mkuu, viwanja vya Kigamboni vimetolewa kiholela, mimi binafsi niliambiwa nitume dollar 3,000 nipatiwe kiwanja beach nikashtuka kwa sababu sikuamini kabisa kwamba serikali inaweza kutoa viwanja vya beach bila kuona mjengo ama dhumuni la maombi ya kiwanja hicho..Mji haujengwi kwa kutoa vibali na hati bila kufuata ramani iliyopo mezani..Na sidhani kama tunayo ramani ya mji wetu kwa miaka 10 au 20 ijayo!.. hivyo, nilijua kuna namna pamoja na kwamba ningepewa kibali na pengine kuchukua hata Hati ya kumiliki lakini kisheria utaratibu ulotumika unanifungia kanyaboya..

Kweli kabisa toka mwinyi, Mkapa hadi leo Kikwete kumekuwa na utapeli mkubwa toka kwa viongozi wetu lakini kuwepo kwa viwanja hivyo chini ya serikali kunatupa muda na wasaa wa kuwaondoa CCM madarakani na serikali mpya ikaweza kutumia haki hii kuijenga tanzania tunayoitaka badala ya kurudi tena ktk sheria za Utaifishaji baada ya ujenzi mbaya.
 
Nashangaaa katika MJADALA huu bado hamjamtaja yule MHINDI/MWARABU aliamua kuchukua almost vwanja vyote kwa msaada wa yule Jaji pale KISUTU


Kama kuna mtu keshadhulumiwa pale najua mtajua namuongelea nani
 
Back
Top Bottom