Tukumbushane ya Pugu Sekondari

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Si vibaya mtu ukikumbuka ulipotoka.

Nakumbuka siku ya kwanza kukanyaga Pugu ilikuwa tarehe 5 mwezi februari. ilikuwa ni siku ya mapumziko (public holiday), siku ya kuzaliwa CCM(Kwa miaka hiyo tarehe ya kuzaliwa CCM ilikuwa inaadhimishwa kitaifa na inakuwa ni mapumziko).

Nilipangiwa bweni la Maendeleo 2 na baada ya muda nilichaguliwa kuwa dom monitor. Kipindi kile pale Pugu mbele kidogo ya jiko kulikuwa na mradi wa nguruwe ambapo wanafunzi walikuwa wanawahudumia bila kujali wewe ni wa dini gani, mimi na wenzangu tulisimama kidete kupinga mradi ule hadi ukafutwa.

Nakumbuka shida ya maji ya kunywa pale shuleni na ilikuwa inatupasa twende pondi ya mzee wa shamba kuchota maji na kuja kuyafungia katika makabati yetu maarufu kama lockers.

Maisha ya bweni yalikuwa ni mazuri sana, ratiba ya chakula ilikuwa ni kama ifuatavyo: Tulikuwa tunakunywa uji saa 4, saa nane ugali maharage na usiku pia isipokuwa siku ya jumatano usiku ilikuwa ni siku ya wali maharage na alhamisi mchana tunapewa matunda(ndizi) na usiku wa alhamisi ni ugali kwa nyama(kipindi kile nyama tulikuwa tunaita kishoka).

Vyoo vya Pugu maarufu kwa jina la bettle vilikuwa vina harufu kali sana na ilikuwa inatupasa tuvue mashati kabla ya kuingia vinginevyo utanuka mpaka bwenini/darasani kwa harufu.

Pugu!!!!!!! nakumbuka mengi, walimu wangu akina Cobra "hilo ni jina la utani, jina lake halisi silikumbuki", mwl Charwe(huyu aliwahi kuninyang'anya viatu vyangu vya ngozi nilivyokuwa nimepewa na mzee wangu ambaye alikuwa ni afisa wa jeshi), mwl Juma Wasiwasi, Mwl Maliki, Mwl Shangwe, Mwl mukuru, marehemu mwl Swai, mabagala(sijui yupo wapi siku hizi), Mwl Mamilo, huyu alinikamata na "feki" la Physics NECTA na hatimae nikafutiwa matokeo yangu ya NECTA. Nimekumbuka sana shule yangu, ambayo imesaidia kujenga historia yangu.

WANA PUGU, MNAKUMBUKA NINI PUGU!!!! LET'S SHARE
 
Si vibaya mtu ukikumbuka ulipotoka. Nakumbuka siku ya kwanza kukanyaga Pugu ilikuwa tarehe 5 mwezi februari. ilikuwa ni siku ya mapumziko (public holiday), siku ya kuzaliwa CCM(Kwa miaka hiyo tarehe ya kuzaliwa CCM ilikuwa inaadhimishwa kitaifa na inakuwa ni mapumziko). Nilipangiwa bweni la maendeleo 2 na baada ya muda nilichaguliwa kuwa dom monitor. Kipindi kile pale Pugu mbele kidogo ya jiko kulikuwa na mradi wa nguruwe ambapo wanafunzi walikuwa wanawahudumia bila kujali wewe ni wa dini gani, mimi na wenzangu tulisimama kidete kupinga mradi ule hadi ukafutwa.
Nakumbuka shida ya maji ya kunywa pale shuleni na ilikuwa inatupasa twende pondi ya mzee wa shamba kuchota maji na kuja kuyafungia katika makabati yetu maarufu kama lockers. Maisha ya bweni yalikuwa ni mazuri sana, ratiba ya chakula ilikuwa ni kama ifuatavyo: Tulikuwa tunakunywa uji saa 4, saa nane ugali maharage na usiku pia isipokuwa siku ya jumatano usiku ilikuwa ni siku ya wali maharage na alhamisi mchana tunapewa matunda(ndizi) na usiku wa alhamisi ni ugali kwa nyama(kipindi kile nyama tulikuwa tunaita kishoka).

Vyoo vya Pugu maarufu kwa jina la bettle vilikuwa vina harufu kali sana na ilikuwa inatupasa tuvue mashati kabla ya kuingia vinginevyo utanuka mpaka bwenini/darasani kwa harufu. Pugu!!!!!!! nakumbuka mengi, walimu wangu akina Cobra"hilo ni jina la utani, jina lake halisi silikumbuki", mwl Charwe(huyu aliwahi kuninyang'anya viatu vyangu vya ngozi nilivyokuwa nimepewa na mzee wangu ambaye alikuwa ni afisa wa jeshi), mwl Juma Wasiwasi, Mwl Maliki, Mwl Shangwe, Mwl mukuru, marehemu mwl Swai, mabagala(sijui yupo wapi siku hizi), Mwl Mamilo, huyu alinikamata na "feki" la Physics NECTA na hatimae nikafutiwa matokeo yangu ya NECTA. Nimekumbuka sana shule yangu, ambayo imesaidia kujenga historia yangu.

Hivi haya maneno DOCEBIT VOS OMNIA yanamaanisha nini? Yameandikwa kwenye ule ukuta una-oface parade ground, halafu kwa juu yake kuna picha ya Njiwa/Hua
 
Kobra jina lake aliitwa Wajimira,namkumbuka mukuru aliyekuwa akituchezesha kwata uwanja wa mpira ,nakumbuka disko la welcome na graduations ,ruvu girls walikuwepo siku hiyo. Mr malick alikuwa mwalimu wa history ,mabagala kemia ,je wakumbuka uji ulikuwa ukinywewa kweny Tg na maboza? Je wamkumbuka mzee wa shamba aliyekuwa akituuzia mihogo? Je wakumbuka mashamba ya mihogo na minazi na je vipi zamu ya kuchunga ng'ombe . Pugu boys wazee wa ku drop wakati mwingine na vidumu vya kutafuta maji ya kunywa pale gongo la mboto mashine. Credit ziwaendee marehemu Mtera my only headmaster f1 to 4
 
Nusura nihailishe mwaka baada ya kuugua tyford kali wiki kabla ya mtihani. Paper ya Math na Pysics practical nikuwa naharisha vibaya hata matokeo hayakuwa mazuri, nikapiga E Mbili na C moja, sikuweza kwenda chuo direct, nimefurukuta tu baada ya kuingia mtaani. Nakumbumbuka WAJIMIRA(Cobra) alitupa adhabu ya kung'oa visiki kule majohe sababu ya kuchelewa kurudi toka likizo, jamaa alikuwa katili sana sijui yuko wapi siku hizi. Nakumbuka patashika siku ya kishoka, jamani maisha yale du sina hamu, na kibaya zaidi tulikuwa tunachanganywa na watoto wa form one basi patashika tupu.
 
Pugu si mchezo, nakumbuka mabagala asubuhi asubuhi kama hujaenda assemble full kukimbizana, namkumbuka mama P muuza wali, R. I P mama P alifanikisha vya kustosha mimi kuishi Pugu. nakumbuka J3 siku ya nyama watu mapema sana wapo DH, ilikuwa kiambulia mchuzi kitu cha kawaida sana... nakumbuka Pond, nakumbuka battle... nakumbuka ili full kudrop kila ijumaa ikifika... Pugu imesaidia sana kuwa hapo nilipo..
 
Pugu nakumbuka vifuatavyo

  • Kudrop-maana yake kuondoka shuleni kwenda nyumbani bila ruhusa hiki kipindi mpaka naondoka form 4 mwaka 2010 kilikuwa bado kipo sana na kurudi shuleni ni Jumapili jioni sana au JumatatU asubuhi

  • Mwalimu Ogesa(makamu mkuu wa shule) - Wanafunzi walipenda kuiga sauti yake sana na walimpondea mkanda wake kwamba hakuweza kuubadili tangu tunaingia form one mpaka tunaondoka form four.

  • Jeshi la wokovu walikuwepo waalimu wafuatao

  • Mwero[mkuu]
  • Ogesa[msaidizi]
  • Nampanda
  • Angelo
  • Magari
  • Senga[ndo jina la utani tangu nafika form one mpaka naondoka ckujua jina lake kamili]
Kazi ya hili kundi nikuhakikisha kila mtu anaingia darasani sababu utoro ulikuwa umezidi sana yani baada ya break tu watu hawarudi tena darasani wenginewalilala sababu wametoboa wengine uvivu wameshiba maandazi ya mama Mainda au sambusa na chapati za mama Bonge au maandazi ya mama Maqantity walienda Gongo la mboto ,Mwisho wa lami wengine walienda kwenye tarehe zao

  • Mwalimu Magari ni mwalimu wa malezi alikuwa mahahrufu wa kukariri visogo vya watu yani mtu akimuona anakimbia huku akiwa ameficha kichogo badala ya uso sababu alikuwa akiona kichogo bhasi tena ashakujua alikuwa mwalimu wa kipekee sana lakini kabla sijaondoka pale Pugu alienda kuwa mkuu wa shule ya O level ya jirani na Pugu
  • Vurugu za machungwa hapa siku kama sijakosea ilikuwa siku za ugali pia Vurugu za mikate iliyokuwa wanagawa siku za ugali pia ila saa nne ndo walikuwa wagawana mikate midogo super Loaf 5 kwa 25 boys hapa kama hauko chap unaambulia patupu nilikuwa mmoja wao walio ongoza kwa kukosa mikate

  • Kuzamia madish ya watu au Table leader anapochukua dish nakuelekea sehemu ambayo watu hawaijui kisha watu wanamis na kwenda kuzamia kwa madish ya watu wengine sanasana siku za wali na nyama watu walitumia majina kupewa msosi na table leader sababu siku ya J3,J5,Jmoc ni wali Ijumaa ni nyama zilikuwa zinazua hadi ngumi beef nzito matusi ya nguoni na hadi kufichuliana siri coz ya hasira ya kumisishwa msosi.

  • Docebit vos Omnia -- Nilimuuliza head master Mr.Mwero akanijibu ni UJIO WA KRISTO YULE NJIWA NDO KRISTO NDO MAANA ANAKUWA ANAPAA KUELEKEA CHINI TOKEA JUU.
:peace::love::love::love:
 
Docebit vos Omnia = He will teach you everything
 
Boza ,container ya plastic ilitumika kunywea uji,TG, ni kikombe na bakuli zilizotumika kulia chakula na kunywea uji, mzee wa shamba ni mzee aliyekuwa maarufu kuuza mihogo, kobra ni mwalimu maarufu aliyekuwa akifundisha physics na alikuwa mwalimu wa malezi
 
Nakumbuka siku ya kwanza nimeenda kureport form one Pugu baada ya kupatiwa bweni lilikuwa Umoja 2 ile kufika bwenini tu nikaenda chooni kulia. Nilimwaga sana machozi lakini nashukuru nikaja kuzoea shule.. Mwenyeji hadi wa pondi
 
Pugu nakumbuka vifuatavyo

  • Kudrop-maana yake kuondoka shuleni kwenda nyumbani bila ruhusa hiki kipindi mpaka naondoka form 4 mwaka 2010 kilikuwa bado kipo sana na kurudi shuleni ni Jumapili jioni sana au JumatatU asubuhi

  • Mwalimu Ogesa(makamu mkuu wa shule) - Wanafunzi walipenda kuiga sauti yake sana na walimpondea mkanda wake kwamba hakuweza kuubadili tangu tunaingia form one mpaka tunaondoka form four.

  • Jeshi la wokovu walikuwepo waalimu wafuatao

  • Mwero[mkuu]
  • Ogesa[msaidizi]
  • Nampanda
  • Angelo
  • Magari
  • Senga[ndo jina la utani tangu nafika form one mpaka naondoka ckujua jina lake kamili]
Kazi ya hili kundi nikuhakikisha kila mtu anaingia darasani sababu utoro ulikuwa umezidi sana yani baada ya break tu watu hawarudi tena darasani wenginewalilala sababu wametoboa wengine uvivu wameshiba maandazi ya mama Mainda au sambusa na chapati za mama Bonge au maandazi ya mama Maqantity walienda Gongo la mboto ,Mwisho wa lami wengine walienda kwenye tarehe zao

  • Mwalimu Magari ni mwalimu wa malezi alikuwa mahahrufu wa kukariri visogo vya watu yani mtu akimuona anakimbia huku akiwa ameficha kichogo badala ya uso sababu alikuwa akiona kichogo bhasi tena ashakujua alikuwa mwalimu wa kipekee sana lakini kabla sijaondoka pale Pugu alienda kuwa mkuu wa shule ya O level ya jirani na Pugu
  • Vurugu za machungwa hapa siku kama sijakosea ilikuwa siku za ugali pia Vurugu za mikate iliyokuwa wanagawa siku za ugali pia ila saa nne ndo walikuwa wagawana mikate midogo super Loaf 5 kwa 25 boys hapa kama hauko chap unaambulia patupu nilikuwa mmoja wao walio ongoza kwa kukosa mikate

  • Kuzamia madish ya watu au Table leader anapochukua dish nakuelekea sehemu ambayo watu hawaijui kisha watu wanamis na kwenda kuzamia kwa madish ya watu wengine sanasana siku za wali na nyama watu walitumia majina kupewa msosi na table leader sababu siku ya J3,J5,Jmoc ni wali Ijumaa ni nyama zilikuwa zinazua hadi ngumi beef nzito matusi ya nguoni na hadi kufichuliana siri coz ya hasira ya kumisishwa msosi.

  • Docebit vos Omnia -- Nilimuuliza head master Mr.Mwero akanijibu ni UJIO WA KRISTO YULE NJIWA NDO KRISTO NDO MAANA ANAKUWA ANAPAA KUELEKEA CHINI TOKEA JUU.
eace::love::love::love:
Daaah umenikumbusha mbali sana kaka.
 
Nawakumbuka sana teachers wa chemistry Shrondinga jina lake kimili nimelisahau alikuwa mzur sana kwenye organic chemistry
Kiberit..huyu alikuwa mzee daaa kwa practical za chemistry alikuwa njema sana na tulielewana sana maswali ya chemistry nilikuwa nayo niliyasolve yote kwa msaada wake kwahyo students ilikuwa lazma anione akitaka solution za practical aliwaelekeza waje kwangu
Anjelo..mtaalam wa physical chemistry nilifanya mitihan ming kwake
 
Nilikaa bweni la Maendeleo1 na walemavu kulikuwa na chumba cha stafu pale niliwazoea sana wakina KAPETO,,,Edo boy
Bwen la walemavu weng walikuwa wanalitenga flan hv na kuwaogopa
 
Kobra jina lake aliitwa Wajimira,namkumbuka mukuru aliyekuwa akituchezesha kwata uwanja wa mpira ,nakumbuka disko la welcome na graduations ,ruvu girls walikuwepo siku hiyo. Mr malick alikuwa mwalimu wa history ,mabagala kemia ,je wakumbuka uji ulikuwa ukinywewa kweny Tg na maboza? Je wamkumbuka mzee wa shamba aliyekuwa akituuzia mihogo? Je wakumbuka mashamba ya mihogo na minazi na je vipi zamu ya kuchunga ng'ombe . Pugu boys wazee wa ku drop wakati mwingine na vidumu vya kutafuta maji ya kunywa pale gongo la mboto mashine. Credit ziwaendee marehemu Mtera my only headmaster f1 to 4
bad news,head master wetu mwlm Mtera kumbe ni marehemu? alifariki mwaka gani? Mungu amlaze mahali pema peponi.
 
Nawakumbuka sana teachers wa chemistry Shrondinga jina lake kimili nimelisahau alikuwa mzur sana kwenye organic chemistry
Kiberit..huyu alikuwa mzee daaa kwa practical za chemistry alikuwa njema sana na tulielewana sana maswali ya chemistry nilikuwa nayo niliyasolve yote kwa msaada wake kwahyo students ilikuwa lazma anione akitaka solution za practical aliwaelekeza waje kwangu
Anjelo..mtaalam wa physical chemistry nilifanya mitihan ming kwake
Mwlm Mkandawile aka "madam" mwalimu wa chemistry enzi zenu hakuwepo?
 
Si vibaya mtu ukikumbuka ulipotoka. Nakumbuka siku ya kwanza kukanyaga Pugu ilikuwa tarehe 5 mwezi februari. ilikuwa ni siku ya mapumziko (public holiday), siku ya kuzaliwa CCM(Kwa miaka hiyo tarehe ya kuzaliwa CCM ilikuwa inaadhimishwa kitaifa na inakuwa ni mapumziko). Nilipangiwa bweni la maendeleo 2 na baada ya muda nilichaguliwa kuwa dom monitor. Kipindi kile pale Pugu mbele kidogo ya jiko kulikuwa na mradi wa nguruwe ambapo wanafunzi walikuwa wanawahudumia bila kujali wewe ni wa dini gani, mimi na wenzangu tulisimama kidete kupinga mradi ule hadi ukafutwa.
Nakumbuka shida ya maji ya kunywa pale shuleni na ilikuwa inatupasa twende pondi ya mzee wa shamba kuchota maji na kuja kuyafungia katika makabati yetu maarufu kama lockers. Maisha ya bweni yalikuwa ni mazuri sana, ratiba ya chakula ilikuwa ni kama ifuatavyo: Tulikuwa tunakunywa uji saa 4, saa nane ugali maharage na usiku pia isipokuwa siku ya jumatano usiku ilikuwa ni siku ya wali maharage na alhamisi mchana tunapewa matunda(ndizi) na usiku wa alhamisi ni ugali kwa nyama(kipindi kile nyama tulikuwa tunaita kishoka).

Vyoo vya Pugu maarufu kwa jina la bettle vilikuwa vina harufu kali sana na ilikuwa inatupasa tuvue mashati kabla ya kuingia vinginevyo utanuka mpaka bwenini/darasani kwa harufu. Pugu!!!!!!! nakumbuka mengi, walimu wangu akina Cobra"hilo ni jina la utani, jina lake halisi silikumbuki", mwl Charwe(huyu aliwahi kuninyang'anya viatu vyangu vya ngozi nilivyokuwa nimepewa na mzee wangu ambaye alikuwa ni afisa wa jeshi), mwl Juma Wasiwasi, Mwl Maliki, Mwl Shangwe, Mwl mukuru, marehemu mwl Swai, mabagala(sijui yupo wapi siku hizi), Mwl Mamilo, huyu alinikamata na "feki" la Physics NECTA na hatimae nikafutiwa matokeo yangu ya NECTA. Nimekumbuka sana shule yangu, ambayo imesaidia kujenga historia yangu.

WANA PUGU, MNAKUMBUKA NINI PUGU!!!! LET'S SHARE
Mimi nakumbuka sana "battle" nilikuwa naishi "Mapinduzi ",,,nakumbuka pia maisha ya pond,,maisha ya kubeba maji ya kunywa kwenye kidum cha lita tano....zaidi ya yote naikumbuka sana shule yangu Pugu high school ilinilea vizuri sana...wako wapi mkali wa hesabu mwlm Aradai,mkali wa physics mwlm Sarawati?
 
Mwl Sarawati mkali wa physics alihamishiwa Ifunda Tech
 
Back
Top Bottom