Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

CLARA OOH MAMA SIKUDHANI KAMA UTANIKATAAAAAAAAAAAAAAAAAA...........!clara ooohh maaaamaaaaaaa!

dah!nilipiga sana keyboard enzi zangu
 
Asha mwanaSeif niambie mpenzi wangu,imekuwaje leo mama uko kimya hivyo,ni lipi jambo limekuudhi nieleze leo,sema Asha seema mpenzi wangu kama mimi nimekuudhi unieleze

Nashukuru mume wangu kwa kuniuliza ooh,unakunywa pombe huonekani mpaka siku tatu,nachekwa na wenzangu,watoto wanateseka,hata huruma huna kwa hawa malaika, nachekwa na wenzangu,watoto wanateseka,hata huruma huna kwa hawa malaika

Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto(mama Maika), Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto

(TX) Aa mama,nimekubali maneno yako mama(ooh mama) wakale walisema mjinga kwa kwenda kwa kurudi anajuaa,pabaya na pazuri lelele

Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto(mama Maika), Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto

(Mbwembwe) Natubu mbele yako hata kwa hawa malaika,unisamehe Duniani hata mbinguni,nasema…

Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto(mama Maika), Ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto

Wewe Mkali........!
 
Kaka unatisha si kidogo,nimekuvulia kofia,au mwenzetu unakachip kwenye head,ha ha ha ha.

Ukweli ni kwamba mimi ni mpenzi sana wa muziki wetu wa Dansi na kwenye Music library yangu nina hazina /miziki si haba..Naisikiliza kila siku hii
 
King Kikiii _ Kitambaa cheupe ( Zipola)
i love this song wapendwa duh
''...nainua mkono mamaaaa.........KITAMBAA CHEUPEEEEEEE
ishara ya mapenzi mamaaaa........OHHHHH ZIBORAAAA

mamaaaa zibo mamaa zibo ZIBORAAAA OOOHHHOO MAMAAAAAAAAA!

CHUNGULIAAAAAAAAAAAAA!...''

dah!:D
 
Ukweli ni kwamba mimi ni mpenzi sana wa muziki wetu wa Dansi na kwenye Music library yangu nina hazina /miziki si haba..Naisikiliza kila siku hii

I can see,mie nilipokuwa o'level nilikuwa nina uhusiano mzuri sana na RTD, baada ya hapo si bongo flevor zikachukua nafasi,siku hizi moja moja sana.Hongera sana.
 
GEORGINA, NEEMA, SIWEMA..TATU BORA..Any ways nyingi ziko bomba.. lol mwanakijiji umefikiri vp huku..could never think of this..nways great idea lol..zingine za enzi mpk leo zimetulia!
 
Mkuu lyrics hizi hapa

1.Sauda

Sauda,Sauda oooh,Sauda dada…
Tangu tuwe wapenzi tumependana kikweli pendo letu la moyoni,
Mioyo tusibadili wangu kipenzi dada tuepuke ushauri
Kwa mahasidi wa penzi ooh Sauda kwa mahasidi wa penzi mama ooh Sauda

Tangu tuwe wapenzi tumependana kikweli pendo letu la moyoni,
Mioyo tusibadili wangu kipenzi dada tuepuke ushauri
Kwa mahasidi wa penzi ooh Sauda kwa mahasidi wa penzi mama ooh Sauda

Sauda ooooh mama,Sauda ooooh mamaaa

Mv Mapenzi meli ya wapendwa nao,moyo kama bahari manahodha mimi na wewe

Mv Mapenzi meli ya wapendwa nao,moyo kama bahari manahodha mimi na wewe

(Gurumo) Duniani kuna mengi sawasawa na bahari,kuna papa na nyangumi tena wale wa hatri,hawapendi kuiona meli yetu baharini watafanya kila njia waifupishe safari

Mv Mapenzi meli ya wapendwa nao,moyo kama bahari manahodha mimi na wewe

Mv Mapenzi meli ya wapendwa nao,moyo kama bahari manahodha mimi na wewe

(Gurumo) Duniani kuna mengi sawasawa na bahari,kuna papa na nyangumi tena wale wa hatri,hawapendi kuiona meli yetu baharini watafanya kila njia waifupishe safari Sauda eeh

2.Kesi ya Khanga(Monica)-ZAITA Musica

Mama nipe nauli nikamfuate Monika ee,amekimbilia Zambia na treni ya mizigo ee,kisa cha kukimbia madeni yamemzidi doti kumi za khanga alizokopa hajalipa ee,anatafutwa na Polisi popote hapatikani,na mimi rafiki yake nipo nje kwa mdhamana ee,nililala rumande siku mbili kituoni,usumbufu nilioupata kwa kweli sina raha ee

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi

Mahakamani wameshapanga siku ya kusikiliza kesi,asipokuja nitapelekwa jela kutumikia kifungo,ee Monika eeeh uko wapi ee,Monika eeh

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi

Naona bora niende Zambia nikamtafute Monika,nimlete Daresalama apambane na kesi yake,e Monika eeh uko wapi eeeeh

Mwaveja sana....mwanawane......! ngoja nianze kuegesha......!
 
[...

Duniani kuna mengi sawa sawa na bahari kuna papa na nyangumi tena wale wa hatari hawapendi kuiona meli yetu bahari[/QUOTE]

Watafanya kila jia waifupishe safari.
Huu wimbo alikuwa naupenda jamaa yangu enzi hizo Kasulu-Kigoma, RTD pekee ukibahatisha KBC kupitia SW 2 unakutana na Katitu.
 
Niko hapa nasikiliza "Christina Moshi" Rudia posti ya mwanzo nitawapatia nilizonazo hapa na kama kuna mtu anazo angependa kushare nitumie kwenye email yenye jina la "mwanakijiji" kwenye anuani hii ya jamiiforums.

"tulipokubaliana kwa hiari, tulikuwa wawili, watatu mungu wetu!!" .. kibwagizo mwah.. silali leo; mtakoma!
 
[...

Duniani kuna mengi sawa sawa na bahari kuna papa na nyangumi tena wale wa hatari hawapendi kuiona meli yetu bahari

Watafanya kila jia waifupishe safari.
Huu wimbo alikuwa naupenda jamaa yangu enzi hizo Kasulu-Kigoma, RTD pekee ukibahatisha KBC kupitia SW 2 unakutana na Katitu.[/QUOTE]

rudi kwenye posti ya kwanza.. ujikumbushie!!
 
asha mwanaseif niambie mpenzi wangu,imekuwaje leo mama uko kimya hivyo,ni lipi jambo limekuudhi nieleze leo,sema asha seema mpenzi wangu kama mimi nimekuudhi unieleze

nashukuru mume wangu kwa kuniuliza ooh,unakunywa pombe huonekani mpaka siku tatu,nachekwa na wenzangu,watoto wanateseka,hata huruma huna kwa hawa malaika, nachekwa na wenzangu,watoto wanateseka,hata huruma huna kwa hawa malaika

ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto(mama maika), ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto

(tx) aa mama,nimekubali maneno yako mama(ooh mama) wakale walisema mjinga kwa kwenda kwa kurudi anajuaa,pabaya na pazuri lelele

ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto(mama maika), ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto

(mbwembwe) natubu mbele yako hata kwa hawa malaika,unisamehe duniani hata mbinguni,nasema…

ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto(mama maika), ulevi ulio nao bwana unanitia aibu,huna mapenzi oo kwangu mimi na watoto

thanks balatanda nimekukubali
 
Salama by Jabali la Muziki

Wapi salama, salama nakuomba
salama nakwita mamaa
umenipa machozi, machozi yasiyokwisha
nifanyeje mwana mamaa

nikilala naota sura yakoo
nikitembea nasikia waniitaa
nageuka sikuoni mwana mamaa
nauliza uko wapi mwana mamaa
 
kumbe kuna wapenzi wa dansi humu.. nilidhani kizazi cha bongo flava ndio kimeshatu waipu auti!? Then there is hope for some old folks! Maana wengine tumezoea minesoneso ya taratibu.. mambo ya kufokeana masikioni hatuwezi..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom