Tukumbushane riwaya za kusisimua

Watoto wa Mama ntilie hakika riwaya hii imekaa na inasisimua kwa sababu imeeleza mazingira halisi ya kitanzania

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hanahela,
mashujaa,
hadithi ya alan quatamani
mashimo ya mfalme suleiman
rosa mistika
kibaraka na nyingeinezo hizi zilikuwa zinapatikana kwenye maktaba ya taifa iliyokuwa inatembea vijijini. Nilikuwa nasoma tu riwaya hizo hadi ninalia kutokana na visa vya wahusika. Aliyeandika na mchapishaji sikuwa nazingatia.
 
Hizi ni baazi tu za riwaya za kitambo sana (Simu ya Kifo,Mizimu ya Watu wa Kale,Cha Mnyonge Utakitapika Hadharani) hiki kimeandikwa na Ephrahim Kezilahabi
 
inspekta fog na kachero haji nliwapenda sana..bado natafuta opereshen sukuma namba nane na simu ya kifo sureish kanji alipokuwa anapiga simu kuwaambia polisi anaenda kuua...kaka umenikumbusha mbali sana. pia nakitafuta kitabu cha SIFI MARA MBILI. OPERESHENI SUKUMA NAMBA NANE,MMEMPA ACHUME, na yule Jambazi aliyeamua kuwaua wanawake wenye majina yaliyoanzia na Z..
 
Kuna kitabu kinaitwa UTOTOLE muandishi simkumbik! Nilikisoma huku ninalia..!

aisee nakikumbuka sana UTOTOLE.. kitabu kina mambo ya uchawi wa kutisha. sijapata kuona kitabu chenye story za kichawi kama kile. duuh! nilikisoma kitambo saaaaaana! nami simkumbuki mtunzi ni nani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom