Tukumbushane: Nyimbo bora zenye majina ya kiume...II

Hivi Skassy Kasambula aliishia wapi huyu..Nakumbuka mara ya mwisho kumuona alikuwa na Bendi ya Ngorongoro akiwa pamoja na Shabani Yohana 'Wanted'

...Huyu Bwana sijui aliishia wapi. lakini nakumbuka alipokuwa Ngorongoro Heroes band na akina Kalodji, Kasaloo kyanga, Kyanga Songa, Shabaan Yohana Wanted, Muharami Seseme na wengineo na mtindo wao wa Sukuma Push waliachia kibao cha 'Kambwembwe' na 'Naachia Ngazi'.

Huu hapa ni Naachia Ngazi:

Unipe pendo lako oo mamaa,
Unipe penzi lako nijisikie eee x2


Mwenzio napata tabu kaa ujue,
Kwa ajili yako x2


Nitazame ninavyodhoofika sanaa,
Niitazame ninavyodhoofika sanaa x 2,

Bora niachie ngazi ee nipate kupumzika x 4


Halafu huu hapa Kambwembwe:

Kambwembwe iyoo lele mama,
Kambwembwe iyoo lele mamaa x 2


Nilikuwa nakupenda iyo lele mama,
Nakataa majivuno mama kambwembwe x 2


Kambwembwe iyo lele mama,
kambwembwe iyo lele mama x 2


Uzuri wako wa sura iyo lele mama,
tabia yako mubaya iyo lele mama x 2


zilikuwa nyimbo fupi kwa maneno lakini mdundo wake wa Sukuma Push ulikuwa ni moto wa kuotea mbali!
 
Mmesahau " Mume wangu Jerry"
..nimechoka na visa vyako..nimevumilia kutokana na mwenendo wakooooo - Mlimani Park orchestrar

halafu "Salehe"huu ni wa Marquis du zaire kam sikosei

"Takadiri" -wa OSS
"Mario" -Lwambo Luanzo Makiadi
 
Gama -DDC ,Tafadhali ungeniambia makosa niliyokutendea wee Gamae
Mfaume - DDC , Mfaume wanilizae, we waniambia nende kwetu
Rehani - DDC , Homa imenizidia mie ooh
Isa - DDC , Mnatusema sisi wanawake wabaya, shemeji yangu Isa
Haruna - OSS , Haruna kaka ee, Haruna kaka ooh
Maburuki - OSS ,Tabia na vitendo vyako vyanikera babu ee, sheri ee
 
Nimekumbuka wimbo wa "Rama". Sikumbuki bendi iliyoupiga wimbo huu. Una kibwagizo kifuatacho:
...Matatizo yatakaponizidia ...oh oh oh Rama... sintovumilia....x2

Pesa ulizoniachiaaaa
Zimekwisha Rama
Kwa kuuguza watoto wetu
Mume wangu....

Dah hilo ni Nginde na hicho kipande anakiimba Benovilla Antony.
 
Zomboko -ioss
Ford- ioss
Masudi- marijani



Sent from my iPad using Tapatalk HD
 
Zomboko -ioss
Ford- ioss
Masudi- marijani



Sent from my iPad using Tapatalk HD


Huyo Masudi alikuwa ni ngoma ngumu kweli kweli yani.
Kwa mfano ndio ukutane nae ukiwa umeishika hiyo IPad yako ni lazima useme nae...
 
Kibwe Mutondo - Marquis Original
Takadiri - ioss ( Ndala Kasheba)


Sent from my iPad using Tapatalk HD
 
Mi nakumbuka kitu kimoja cha Biashara Jazz Band Kinaitwa Wivu ukizidi--Wivu ukizidi nyumbani
Mapenzi yapungua
Wivu USIO NA MAANA waleta hasara,
Umepatwa kitu gani,
Bibi umekataza kufanya kazi,
Ati sababu achelewa nyumbani.
 
Back
Top Bottom