Tukumbushane: Hivi kwanini Nyerere alikataa J. S. Malecela asigombee urais kupitia CCM

Pamoja na John Samwel Malecela kuwa mwanasiasa mwenye nguvu ndani ya chama cha Mapinduzi CCM na Serikalini lakini juhudi zake za kutafuta kuteuliwa kuwa mgombea urais ziligonga mwamba kwa vipindi vyote viwili vya 1995 na 2005.

Sababu gani zilizofanya ashindwe:

Mbio za Malecela 1995

Ingawa Malecela alikuwa ni mgombea aliyekubalika kati ya wagombea wengine wa CCM lakini Baba wa Taifa JK Nyerere hakufurahishwa na kitendo cha Waziri Mkuu wakati huo Mh. Malecela kuruhusu hoja ya Serikali tatu iletwe bungeni, vile vile hakufurahishwa na kitendo cha yeye kujihusisha na Zanzibar kujiunga na OIC. Kwa hiyo kitendo hicho kilimkera sana Mwalimu hadi akafikia kumtaja Malecela kuwa ni muhuni na mroho wa madaraka. Nanukuu mwandishi mmoja,

"Nyerere saw him as someone who was driven by personal ambition in his quest for the presidency and warned CCM leadership that he would not even attend the party congress if Malecela was on the short list of possible candidates".

Vile vile kulikuwa na hear say kwamba Malecela alikuwa groomed na nchi moja ya kiarabu ili kufanikisha mbio zake za urais na ilisemekana kuwa ilibidi abadili jina(dini) na kujiita Jumanne Samwel Malecela. Kutokana na msimamo wa Mwalimu jina lake halikupendekezwa na Mkapa akaibuka kidedea.

Mbio za Malecela 2005

Baada ya kutofanikiwa lengo lake 1995 Malecela hakukata tamaa alionekana kutokuwa karibu sana na Mwalimu Nyerere na hasira hizo zilienda mbali na kusababisha hadi kwa familia yake imchukie Mwalimu na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM, kiasi kwamba katika kinyang'anyiro cha mwaka 2005 jina lake halikuvuka hata raundi ya kwanza wakati Mh. Kikwete alipoibuka kidedea. Inasemekana kinyongo cha Malecela kukosa urais kwa safari mbili kiliendelea hadi kusababisha makundi ndani ya chama.

Kwa vile wakati ule alikuwa bado na cheo cha Makamu Mwenyekiti rais Kikwete kwa kuona hali ilivyo ndani ya chama ikabidi atafute mbinu ya kumtoa pale, akasema anataka asaidiwe kwenye kiti kile cha M/M/kiti na damu changa lakini matokeo yake mwaka 2007 akateuliwa Pius Msekwa kiasi kwamba watu wakajiuliza damu changa iko wapi. Kwa vile ilionekana Malecela bado ana nguvu ndani ya chama uongozi wa juu wa chama katika kumpunguza nguvu zaidi ukafanya juu chini ili Malecela asishinde kwenye kura za maoni za ubunge jimbo la Mtera.

Mimi binafsi ingawa sikuwa kwenye michakato hii toka 1995 enzi za Mwalimu hadi 2005 enzi za Mkapa/Kikwete lakini nafarijika kwamba huyu Mzee hakupata kutuongoza kwenye nafasi ya urais kwa vile kama alivyosema Mwalimu ni Mbinafsi,Muhuni, roho isiyo na utu'You Can Go to Hell' alitaka kutuingiza OIC, kama si Nyerere kuliona hilo mapema tungejuta.

I say again thank God he is/was not a President of Tanzania.

Mkuu umenena then it simz chuki na kwa Mwl imesharithishwa kwa kizaz chote cha Malecela man hata mkewe willie yupo humu kwa Id ya Field Marshal Es, anamponda sana mwl na kudai mwl alikua anagombea na kivuli,Anamtetea sana mkwewe kwa hasira zao ya kukosa Urais. We ngoja utamuona humu muda si mrefu maadamu thread imemgusa mkwewe so lazima bibie ataingia tu.
 
- Mkuu hakuna mke wa mtu hapa, kama umeshindwa kujadili na wanaume wengine hapa kaa pembeni tu hakuna mke wa mtu hapa, sema hoja yako utajibiwa, lakini hakuna mke wa mtu hapa mbona unatakwia kuwa babu wa kutufundisha mkuu badala yake unakwua kama mtoto mdogo, hivi kweli wewe kuna anayeweza kufikia umri wako humu JF mbona unajidhalilisha sana? Duh!

Willie @ NYC, USA.
 
- JF bin Malecela ha! ha! ha! ha 1 the beat goes on and on and on JF Malecela, saafi sana people, keep it on this is great maaana hili jina Malecela halitapotea never na haya maandishi yasiyofutika, ninawashukuru sana angalau hata Vutukuu watalikuta jina likiwa limesimama that is all you could ask from great thinkers, I mean Malecela JF, Malecela JF! ha! ha!

- Bravo Great Thinkers, Viva Malecela JF! JF Malecela! what a JF Icon, The Retired Malecela JF!

Willie @ NYC, USA
Humu ndio JF home of Great Thinkers! ukijifanya mjuaaji na kuleta zako za kukejeli watu unavuliwa nguo tena sembuse wewe toto la fisadi! hata hiyo tie uliyovaa kuna sumni ya mlipa kodi Mtanzania!
 
Humu ndio JF home of Great Thinkers! ukijifanya mjuaaji na kuleta zako za kukejeli watu unavuliwa nguo tena sembuse wewe toto la fisadi! hata hiyo tie uliyovaa kuna sumni ya mlipa kodi Mtanzania!

- Hapana ni kawaida sana kwa mvuliwa kudai anawavua wengine, kumbe ni yeye aliyevuliwa! ha! ha! maana ni aliyevuliwa ndiye hufungua thread dhidi ya aliyemvua au sio mkuu? ha! ha! ha! ha! ha!

- Halafu I am glad kwamba unaijua JF kuliko mimi, thaanks kwa kunielemisha kuhusu JF maana nilikuwa sijui!

Willie @ NYC, USA.
 
- Mkuu hakuna mke wa mtu hapa, kama umeshindwa kujadili na wanaume wengine hapa kaa pembeni tu hakuna mke wa mtu hapa, sema hoja yako utajibiwa, lakini hakuna mke wa mtu hapa mbona unatakwia kuwa babu wa kutufundisha mkuu badala yake unakwua kama mtoto mdogo, hivi kweli wewe kuna anayeweza kufikia umri wako humu JF mbona unajidhalilisha sana? Duh!

Willie @ NYC, USA.
alaa kumbe na Jumanne Malecela ana ID gani humu kama Mkewe W.J: Malecela ni Field Marshal Es,
 
Yaani Mwalimu Nyerere na ujanja wote ule, alikuwa anamuogopa Malecela?

May be aliona kuwa hawezi kumpelekesha vile angependa...!

I can't believe it's not butter ...ai see
 
- Unasema ni bora kukataliwa na viongozi kuliko wananchi wenyewe wenye taifa, sawa mkuu nimekusikia sana!

Willie @ NYC, USA.
kwa vile unakuwa umebaki na kihoro na simanzi ya kutojua kama wananchi wangekukubali au la? si ndo maana unaona Mh anakata matumaini mapemaa...BTW hali yake inaendeleaje? Ujiheshimu mkuu! unapogusa interest za vijana tuliopinda kama sisi na kumkosea adabu kiongozi wa wananchi Wazalendo (DR wa Ukweli Slaa) ujue watu hawatanyamaza kimya watakuchojoa nguo!
 
Wanafanana kila kitu, hadi sura, wakati ule akijiandaa kuwania Urais Mwanae mmoja pia alikuwa anajikita kutawala UVCCM bahati mbaya akapata ajali na kuaondoka Duniani.

Actully tuna mlaum EL lakini huyu ni zaidi ya EL; wakati ule akiwa M/Mwenyekiti wa Chama alipandikiza wanachama wa Mkutano mkuu wote walikuwa watu wake, ndio maana watu wa UWT wakamwambia Ben kuwa akifanya kosa akaendelea mbele hawatamuweza kwenye vikao vya mbele ikabidi Ben amwambie Towa jina haraka sana unipishe niweze kusimami uchaguzi vizuri, akisita sita Ben akarudia akamwambi tena Mzee Malecele naomba utoe jina lako mwenyewe, ebu ona jinsi alivyo na dhambi kama angekuwa msafi hasinge endelea kuwa CCM maana Ben alimwacha akagawa fedha zake zote kwenye kampeni za chama alafu mwisho wa siku anamwambia atoe jina lake.

Huyu mama wakati ule aliibiwa Laptop na majambazi magumashi! alikuwa tayari anatamba kuwa ni First lady! Maajabu kweli hii nchni bora ya Kikwete mtu watu kazidiwa tu, chama kimeoza chote hana pa kushika, ndio maana kaamua ajikalie kimia hakuna watu wazuri CCM utampa nani Uwazi na uache nani wabunge wa CCM ndio hao Manji, MO, El, RA, Chenge, ni ngumu sana wewe fikiria pamoja na kelele zote tulizopiga hapa JF na Tanzania kwa ujumla bado mtu kama RA anapata kura za Ubunge! Wananchni bado wamelala kuliko tunavyofikiria ndio maana watu kama hawa wanasumbuwa hadi leo.

Kama hakuwa Mroho wa Madara kama Nyerere alivyosema wewe angalia bado alikuwa anagombea Ubunge tu pamoja na kuwa Waziri mkuu Mstaafu, na umri wote huo na kujaribu urais na kukosa mara kadhaa bado alikuwa anawania Ubunge maajabu alizidiwa akili hata na Sumaye sijawai kusikia akifikiria kuwania Ubunge, ubunge wenyewe akisha pata hakuna anachofanya Bungeni!
Asante Arafat;

Tuseme ukweli Malecela alikuwa na nguvu sana serikalini hata kwenye chama kiasi kwamba hata Nyerere alimwogopa, alikuwa amewashika karibu wakuu wote wa mikoa na wilaya na kwa vyovyote vile bila Mwalimu huyu jamaa angekuwa rais hakuna ambaye angemzuia. Ukimtoa Malecela Mwaka 1995 rais alikuwa awe Kikwete ila Mwl hakumtaka kwa sababu zake na endapo Mwl angekuwepo 2005 Kikwete asingekuwa rais leo.

Tofauti ya Kikwete na Malecela, Kikwete ni mjanja baada ya kuukosa kosa urais wa 1995 alijua hawezi kujilinganisha na Malecela kiuwezo (lobbying, pesa you name it) akalazimika kuingia alliance na EL pia akawa mtiifu mzuri kwa Mkapa wakati huo rais ili njia iwe nyepesi come 2005, Malecela akaendelea kujiimarisha kwa watendaji wa mikoa na wilaya akasahau kuwa sauti kubwa iko CC ambayo ilikuwa imekamatwa na Boyz 2 Men mbali ya Malecela kutembeza pesa kwa wajumbe kama ulivyosema lakini akaja kunyang'anywa tonge mdomoni na CC tena kwa aibu.

Tatizo lake lobbying anaijua lakini ni jeuri less care hajui kuinama kwa wadogo he is not flexible rigid alichoamua no one can bend him hilo ndilo haswa tatizo ambalo tungelipata kama angeshika urais sijui kama Mwl naye aliona tatizo hilo kwake maana rais wa aina hiyo ni hatari anaweza kuiingiza nchi kwenye matatizo makubwa ikiwemo vita kama alivyokuwa tayari kuiingiza Tanzania OIC.
 
- JF bin Malecela ha! ha! ha! ha 1 the beat goes on and on and on JF Malecela, saafi sana people, keep it on this is great maaana hili jina Malecela halitapotea never na haya maandishi yasiyofutika, ninawashukuru sana angalau hata Vutukuu watalikuta jina likiwa limesimama that is all you could ask from great thinkers, I mean Malecela JF, Malecela JF! ha! ha!

- Bravo Great Thinkers, Viva Malecela JF! JF Malecela! what a JF Icon, The Retired Malecela JF!

Willie @ NYC, USA
Mkuu, kuna watu wamefanya kazi na Baba yako wako humu JF,hata dili zake, uadilifu wake,mbinu zake,tabia na mwenendo wake wanaujua. Acha hao wamtetee na wewe kaa kimya. Kelele zako ambazo unazipiga zinafanya watu wakudhanie kuwa siku mbili hizi umepiga mitungi sana maana huna hoja kama siku za nyuma ila kubwabwaja na kucheka cheka.
Malecela kama kiongozi ana haki ya kujadiliwa na hajadiliwi kwa vile ni baba yako bali kama kiongozi aliyefanya mazuri na mabaya. Na hayo hayakuhusu kama mtoto bali kama raia wa TZ (kama bado hujaukana uraia wako)
 
- Sasa si wote ni raia tumjadili mbona unanizua na maneno mengi wewe mjadlili na mimi nipe haki kama mwananchi kumjadili, kama ninapomjadili Malecela kwako ninakuwa kama mlevi na wewe usiyekunywa unahangaika na kufungua mi-thread kila kona kunishambulia kwa sababu ya michango yangu, nafikiri inajisema wazi mlevi hasa ni nani kati yetu, au ninakosea?

- Otherwise una hoja nzito sana mkuuu kuliko wengine wengi!

Willie @ NYC, USA.
 
Mkuu, kuna watu wamefanya kazi na Baba yako wako humu JF,hata dili zake, uadilifu wake,mbinu zake,tabia na mwenendo wake wanaujua. Acha hao wamtetee na wewe kaa kimya. Kelele zako ambazo unazipiga zinafanya watu wakudhanie kuwa siku mbili hizi umepiga mitungi sana maana huna hoja kama siku za nyuma ila kubwabwaja na kucheka cheka.
Malecela kama kiongozi ana haki ya kujadiliwa na hajadiliwi kwa vile ni baba yako bali kama kiongozi aliyefanya mazuri na mabaya. Na hayo hayakuhusu kama mtoto bali kama raia wa TZ (kama bado hujaukana uraia wako)

labda ndio kile kiburi cha kusemanitasema lolote,lakini tuna viongozi wengi wastaafu na watoto wao wapo na tunawajua na tunawaheshimu kutokana na mienendo yao kwenye jamii,nafikiri anafanya jambo analochukulia kwa wepesi,maneno yote unayoweka hapa yanaingia ndani ya vichwa vyetu na tunayafanyia kazi,sijui matokeo yake yatakuwaje
 
kwa vile unakuwa umebaki na kihoro na simanzi ya kutojua kama wananchi wangekukubali au la? si ndo maana unaona Mh anakata matumaini mapemaa...BTW hali yake inaendeleaje? Ujiheshimu mkuu! unapogusa interest za vijana tuliopinda kama sisi na kumkosea adabu kiongozi wa wananchi Wazalendo (DR wa Ukweli Slaa) ujue watu hawatanyamaza kimya watakuchojoa nguo!

- Lakini sasa mbona unajichojoa mwenyewe kuliko mimi! ha! ha! ha! ha! unasema uongozi wa wazalendo ni kukwepa kulipa kodi? na posho ya Shillingi Millioni 7.5 kwa mwezi ndio kuongoza wazalendo huko? haya mkuu nimekubali!

Willie @ NYC, USA.
 
labda ndio kile kiburi cha kusemanitasema lolote,lakini tuna viongozi wengi wastaafu na watoto wao wapo na tunawajua na tunawaheshimu kutokana na mienendo yao kwenye jamii,nafikiri anafanya jambo analochukulia kwa wepesi,maneno yote unayoweka hapa yanaingia ndani ya vichwa vyetu na tunayafanyia kazi,sijui matokeo yake yatakuwaje

- Wacha vitisho wewe humliki Tanzania, ni taifa la wananchi Millioni 45, wewe ni mtu mmoja tu kama kweli una huo uwezo kwa nini usimsaidie Dr. Slaa akawa Rais?

Willie @ NYC, USA.
 
nilichoona huu uzi kuna watu wanamfagilia mkapa wengine jk na wengine mwalimu sasa jambo la muhimu nikujua nan yupo right je ni malecela au nyerere...sio tu tunatupa lawama na matokeo yake amjibu hoja mkipigwa ban ooo ma mod hatuwaelewi..
 
William... chill out, si kila ligi lazima ushhiriki

- I am just having fun mkuu leo si unajua US ni a big holiday, anyways wote ni my people kutofautiana ni kawaida sana na pia sometimes kupeana vipande ni kawaida saan kumubuka ni hao hao wanaoniambia mara nyingi hapa kwamba nijiunge na Chadema, so usijali mkuu ni watu wangu sana mimi ni mtu wa kujichanganya hakuna jipya hapa kama wewe ni member wa siku nyingi hapa na besides ni mengi ni mambo ya Territory so relax maan!

Willie @ NYC, USA.
 
William... chill out, si kila ligi lazima ushhiriki
Tatizo lako wakati Saint Ivuga alipoitisha kura ya maoni ya watu wabishi hapa JF hujui nani alishinda, ungemjuwa aliyeshinda wala usingesumbuka.
 
Yaani Mwalimu Nyerere na ujanja wote ule, alikuwa anamuogopa Malecela?

May be aliona kuwa hawezi kumpelekesha vile angependa...!

I can't believe it's not butter ...ai see
yeah it is not butter... it was Jumanne sir

now you believe
 
- Sijazuia anything zaidi ya kutaka kuelimishwa zaidi, kwamba kama unapoamua kuongelea ubaya wa Malecela, ni vyema uokaongelea uzuri wa Mwinyi, Mkapa na JK, ha! ha! ha! ha!

- Sasa mkuu kosa langu lipo wapi hapo au unataka nijitoe kwenye hii thread sema tu mkuu wewe tena mkuu wa JF nitatoka tu ha! ha! ha!

Willie @ NYC, USA.

- Saigon Malecela hafai kwa sababu Mwinyi, Mkapa na JK wanafaa sio ndio argument za kisomi na modern au kwa leo tu iwe Malecela tuu! ha! ha! ha! ha! ha!, Malecela alikosa urais kama Dr. Slaa na Mbowe waliv yokataliwa na wananchi au leo tuongelee Malecela tu? ha! ha! ha!

- Tena Malecela alikataliwa na Viongozi wenziwe, wengine walikataliwa na wananchi au ya Malecela ni mbaya zaidi kuliko ya kukataliwa na wananchi?
ha! ha! ha! ha! ha!, wakuu mnanifurahisha sana maana mnanilazimisha kuandika bila kufiri sana! ha! ha! ha!
Willie @ NYC, USA.
Whats wrong with you kwanini kila sentensi moja unacheka cheka?
 
Back
Top Bottom