Tukubaliane na kuacha Uswahili: Democracy at its Best!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Kwa miaka karibu 20, Tanzania imekuwa katika mchakato wa siasa za vyama vingi. Katika miaka hii 20, damu imemwagika, dhuluma imetokea, uonevu na unyanyasaji umeendelezwa, kauli za kudai haki na usawa zimeendelea kupuuzwa kila mwaka na CCM kimeendeleza utawala wa kibabe kwa kukataa kuanzisha mchakato wa kuundwa kwa Katiba mpya na hata kupuuzia kabis akilio cha kuwa na tume huru ya Uchaguzi.

Zaidi ya hayo, Serikali ya CCM imetumia vyombo vyake vya Serikali kama TISS, Polisi, Jeshi, Mamlaka ya Kodi na taasisi nyingine kisiasa na kwa manufaa yake kwa kudhibiti na kuunyanyasa ule msukumo na wimbi la mfumo wa vyama vingi vya kisiasa na demokrasia.

CCM wamehakikisha kuwa wanapanda mbegu chafu ya kuuonyesha Upinzani kama ni ushetani an udhalimu wa hali ya juu, kiasi cha kuwatishia Watanzania kuwa wapinzani wakipewa dhamana ya kuongoza Tanzania, yaliyotokea Rwanda, Congo, Somalia na kwingineko kuliko na machafuko yatatokea Tanzania.

Watazania walichosahau kuwauliza CCM ni hili, ikiwa Upinzani wa leo iwe CUF, Chadema, TLP, NCCR au chama kingine ambacho si CCM kikawa madarakani kuongoza Taifa letu, ni nani basi ambaye atachukua upanga na majambia kuhatarisha amani yetu na kuleta vita vya ndani? Je hili haliashirii kwamiaka yote kuimbwa wimbo huu kuwa CCM kamwe haitakuwa tayari kukubali kauli za Wananchi kuikataa na kuinyima dhamana ya kuongoza Tanzania?

Je ni sababu hii ya kung'ang'ania madaraka na uchu wa madaraka imefiikia CCM kutafuta mbinu za kila aina katika kila uchaguzi kuhakikisha kuwa inatabngazwa mshindi kwa hali na mali au kama kule Mwanza walikodai "kaza buti hata kwa nguvu" ni lazima CCM ishinde?

Ni kutokana na fikira hizi potofu za kung'angania madaraka na kujiopna kuwa wao CCM ndio Alpha na Omega wa siasa za Tanzania ndipo palipofikia Mwenyekiti wake ambaye alitangazwa kuwa mshindi wa kugombea Urais, Bwana Jakaya Kikwete kutangaza wakati wa kampeni kuwa Upinzani ni nakala.

Haiyumikiniki kuwa juzi wakati wabunge wa Chadema waliposimama na kutoka nje ya Bunge wakati akihutubia, Bwana Kikwete alithubutu kutoa kauli ambayo ni wazi ya kitisho kwa Upinzani.

Nanukuu na kumnukuu kauli yake
Rais Kikwete alikatiza hotuba yake, akanyamaza huku uso wake ukisononeka; akawa ameduwaa, akakohoa kidogo, huku wabunge wa CCM wakipiga makofi kuwazomea CHADEMA; na baadaye alitoa kauli ya kejeli akisema, “Hata wasionichagua hawana serikali nyingine ni hiihii. Watakwenda, watarudi, hawana mwingine wa kumwomba yao yatimie zaidi ya serikali ya CCM ambayo mie ndiye rais wake.”

Ili kuonyesha uroho wao wa madaraka na hata kutokujali maslahi ya Taifa zima na kwa manufaa ya wote, Chiligati amefikia kutoa kauli kama hii ambayo inaashiria wazi kuwa CCM haiko tayari kukaa chini na kufanya haki na kukaa na wenzao kuunda katiba mpya. Nikimnukuu Chiligati amesema hivi
“Waangalizi wa uchaguzi walishatoa taarifa kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki, sasa iweje CHADEMA peke yao kutotambua matokeo kama si uchochezi unaoweza kusababisha uvunjaji wa amani na kuleta vurugu nchini?” alihoji Chiligati katika taarifa hiyo.
Alisema kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi, matokeo ya Rais yakiwa yametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hayapaswi kuhojiwa na mahakama wala chombo chochote, hivyo rais yuko madarakani kwa matakwa ya Katiba hiyo. “Sasa madai ya CHADEMA kwamba iundwe Tume Huru ya Uchaguzi ichunguze nini?....Nia yao wanataka tuache kazi ya kushughulikia maendeleo ya wananchi ili tuingie katika mgogoro wa Kikatiba utakaodumu kwa muda mrefu na kuiingiza nchi katika misuguano na mzozo wa kisiasa?” aliuliza.

Alichokificha kukisema Chiligati na hata Kikwete an Makamba ni kuwa Uchaguzi ulikuwa na madoa na hivyo uhalali wa Serikali yake ni wa mashaka. Wanachokificha ni kuwa haki ilikanyagwa na kufumbwa mdomo kwa kigezo cha Katiba na Tume zimesema hivyo hakuna cha kubadilisha.

Na ndio maana kitendo cha Chadema kutoka nje ya hotuba ya Kikwete kama Rais akihutubia Bunge kimewashitua sana na kila mtu anatafuka kuleta ujuzi wa kisheria au kikatiba kulaani kitendo cha Chadema huku wakisahau kuwa hakuna mahali popote kwenye Katiba au Sheria panaposema ukipingana na Rais au ukatoka nje ya mkutano wake kama kitendo cha kumpinga ni ukosefu wa nidhamu, uvunjaji wa sheria au kuidharau Kariba.

Kwa haki waliodharau Katiba ni CCM kwa kuipuuzia pale inaposema wazi kuwa haki lazima iwe sawa kwa kila Mtanzania na Serikali imepewa dhamana ya kutengeza mazingira sawa kwa kila mtu bila kujali dini, elimu, jinsia, umri au utashi na itikadi ya siasa.

Kwa kuwa ni utamaduni wa Mwenyekiti kushika hatamu, hata yale makombo ya Zidumu Fikra za mwenyekiti, leo hii Makamba anadiriki kuwakoromea Chadema, Chiligati anawakebehi na kudai ni ukosefu wa nidhamu, mbona hawakusema lolote pale Wajumbe wa NEC na CC kutoka Zanzibar alipogomea kikao kule Butiama mwaka jana?

Na hao wote wanojiita Wasomi na wataalamu wa Sheria ambao wanakilaani kitendo cha Chadema, je wanalaani kwa misingi ipi?

Je wao hawatampa hifadhi mtoto au mke anayenyanyaswa na kupigwa na Baba Mume mwenye nyumba?

Kama ni kutaka suluhisho na kuepusha mgogoro wa kisiasa na kikatiba, basi CCM ingefanyia kazi mabadiliko haya miaka 150iliyopita na isingejilazimisha kushinda kuule Zanzibar au huku Bara. Ama isingelitumia Polisi, TISS, TRA, Msajili wa Vyama au Tume ya Uchaguzi kuendeleza mfume wake dume wa kuongoza kwa mabavu.

Kama Uchaguzi huu haukutoa mwangaza kwa CCM kubadilika na kufanya kama walilofanya kwa CUF kule Zanzibar, basi kitendo cha Chadema kuondoka Bungeni kinawapa Watanzani amatumaini kuwa CCM na Rais wa Jamhuri ni watu wa kawadia na si Miungu ya kuogopewa.

CCM wamelewa Madaraka na wanajiona Miungu waabudiwe na kunyenyekewa. Ndugu Mtanzania, kura yako ya hapana na Chadema kutoka nje ya Bunge wakati Rais akihutubia Bunge ni jambo la kawaida na ni demokrasia ya kweli.

Wapimeni Chadema kwa uwezo wao wa kazi na si kusikiliza kejeli, vijembe na vitisho kutoka CCM.
 
Well said Rev,

CCM ni wakoloni kama wengine waliopita, ni jukumu letu kutafuta uhuru wa kweli! sio wa bendera na nyimbo za taifa tu!

Nchi inahitaji kukombolewa, wakoloni hawa weusi, wametuua, wametunyanyasa, wametunyima haki zetu, wamegawana mali zetu, wametugawa watanzania, wamenyima na kuzima wale wote wenye ndoto njema na nchi yao.

Parapanda imeanza kulia, chadema wameanza, moto huu hawataweza kuuzima, hata kama chadema watakaa kimya, maadamu wameanza,moto umeanza kusambaa kama vile nyika ya majani makavu, walio lala wanaamka, waliokuwa waoga wa kupiga kura watapiga, waliosema CCM itashinda tu nyimbo zao hizi zitakoma, mara baad aya kupata tume huru ya uchaguzi na katiba mpya.

Though chadema may think their move was just to 'walk out' OMG that is a walk out from oppresive, from this long awating freedom

Hofu ya mgawanyiko wa dini na makabila hautakuwepo, tutakuwa na katiba moja, nchi moja,watu wamoja, serikali moja the guess what... one heart, to make our beloved country a place to live, grow, produce, and make our dreams come true!

chadema not turning back, if you will then others will rise,plase we trust you go..go..go !!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna Hoja alishaitoa Mwanakijiji Humu (JF) ikiulizia kama sekta mbalimbali za kiserikali na idara mbalimbali za kiserikali kama ziko tayari kupokea mabadiliko? kama zinakubali kuwa chini ya chama kipya (Nje ya CCM)

Mimi nilivyoupima uchaguzi wa Mwaka huu, Tatizo kubwa halikuwa sana kutoka CCM, CCM walipambana na walipata changamoto Kubwa kutoka upinzani Hasa Chadema na Ugumu wa Kampeni waliuona katika miji Mikuu, kuna sehemu Dr Slaa wala Hakufika, na wala Chadema hawakuwa na wawakilishi kwenye hivyo vituo lakini alipata kura nyingi ambazo Hazikutegemewa,

Tatizo kubwa la Uchaguzi wa mwaka huu ni watu ambao ni Teuzi za Rais, hawa ndio walivuruga uchaguzi mwaka huu
1) Msajiri wa vyama vya siasa-(Tendwa) na Mkurugenzi wa NEC (Makame), hawa walikuwa na kauli za kupingana na ikafikia point hataTendwa akawa anaingilia kazi za Makame

2) Tido Muhando na Mkurugenzi wa mawasilianao, naweza sema kwa kiasi kikubwa hawa jamaa walishiriki kuvuruga uchaguzi kwa kukubali kukipendelea CCM kuliko vyama vyote, kibaya zaidi ni kwa mkurugenzi wa mawasiliano, alikubali SMS za ujinga zisambae bila kuichukulia hatua Vodacom na wa kina Shamte, alikaa kimya kwa yale magazeti yaliyokuwa yanaongelea Udini, chuki, Ukabila na vitu kama hivyo

3) Vyombo vya Usalama, Mkurugenzi wa Usalama, JWTZ (Shimbo), Police (Mwema, Kova), Mara nyingi tunajua police ndio huwa wanatumika sana kwenye kampeni za CCM , lakini kwa mwaka huu tumeshuhudia mpaka Mnadhimu wa Jeshi na makamu wa salama wakiingia kwenye siasa

4) Wakurugenzi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, hawa nao walishiriki kikamilifu katika kampeni za mwaka huu, pesa nyingi zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali ilibidi wazitoe ili kufanikisha kampeni, mfano ni mradi wa upanuzi wa Barabara ya Kahama-Rwanda, huo mradi sasa umesimama na watu wa karibu wanasema fedha zote zimeishia kwenye Kampeni

Kwa mtazamo wangu hao Wateule wa Rais ndio kilikuwa Chanzo kikuu cha Uaribifu wa Uchaguzi na Demokrasia nchini
 
Wakuu nashukuru sana kwa ujumbe na elimu hii mliyoitoa hapa.Tayari nadownload ili nikayasambaze Kyela naelekea wiki ijayo.
 
Well said Rev,

Nimeingalia ile scene kupitia Star TV leo asubuhi wakati wabunge wa CHADEMA wakitoka ukumbini, ni kweli kabisa mkulu alikuwa puzzled na hakuamini kile kilichokuwa kinaendelea. CCM wanaweza kuibaraguza tu lakini kiukweli lile tukio tena mbele ya mabalozi na wahisani limewashake ile mbaya.

Hata kama watakuja na kauli gani, ila message has been deliverd already. Na kadri mjadala unavyorefuka ndio wanazidi kuipublicize CDM
 
ni bora kuchagua chama cha wachaga chadema ili waje watutawale kikabila,
maana cc ndo tunataka, kama ingekuwa sio wachaga zitto angeendelea kuwa kiongozi wa upinzani bungeni!!
 
ni bora kuchagua chama cha wachaga chadema ili waje watutawale kikabila,
maana cc ndo tunataka, kama ingekuwa sio wachaga zitto angeendelea kuwa kiongozi wa upinzani bungeni!!

Ndugu yangu nakuomba uwe Mstaharabu kidogo, hii mada ni very serious na wala sio mada ya utani na utoto, kama unaona hauna cha kuweka kinachoendana na hii mada, sio lazima uandike kitu we pita ukishasoma nenda unakoweza kuchangia
ni wapi mtoa mada kaongelea mambo ya Uchaga wa Chadema ama Ukabila wa CCM

acha utoto bwana
 
Minyororo na Pingu za utumwa wa mawazo, kunyimwa haki na kutawaliwa kwa matakwa ya CCM imevunjwa, ndio maana Kikwete hakuamini kilichotokea!
 
Ni kweli kua democracy ni bora kuliko uswahili lakin ni bora zaidi tukaielewa democracy kwanza ndio tukazungumza. Hao wanaoaminika kua ni wazee wa democracy pia wanafanya maamuzi ambayo yanapingana saa nyingine waziwaziwazi na democracy yenyewe kwa mfano ni juzi tu mmoja kati ya washauri wa waziri mkuu wa UK alibidi ajiunzulu kwa kua na mawazo tofauti na bwana mkubwa.

"David Cameron's enterprise adviser Lord Young resigns after being given an "almighty roasting" by the Prime Minister over his remarks about the recession, writes Political Correspondent Cathy Newman" Sasa hiyo ndio democracy unayoitaka?
 
4) Wakurugenzi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, hawa nao walishiriki kikamilifu katika kampeni za mwaka huu, pesa nyingi zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali ilibidi wazitoe ili kufanikisha kampeni, mfano ni mradi wa upanuzi wa Barabara ya Kahama-Rwanda, huo mradi sasa umesimama na watu wa karibu wanasema fedha zote zimeishia kwenye Kampeni

Kwa mtazamo wangu hao Wateule wa Rais ndio kilikuwa Chanzo kikuu cha Uaribifu wa Uchaguzi na Demokrasia nchini

Je hawa Wakuu walioamua kutumia fedha za maendeleo kwa kazi nyingine na hasa kampeni za uchaguzi wa CCM, walipewa idhini hiyo na nani?Je Bunge lilikaa na kusema wakati wa kampeni ni Ruksa kutumia fedha za bajeti kwa kampeni?

Je kwenye hili jambo la hawa Wateule, linatupa picha gani ikiwa maamuzi yao yalikuwa ni kulinda madaraka yao kwa kuhakikisha CCM kinachaguliwa tena kwa ule woga wa kupoteza kazi akija mtu mwingine iwe CUF au CCM?

Je hatuoni sasa kuwa kuna baadhi ya Teuzi zinazofanywa na Rais zinaingilia utendaji wa kiserikali na kufanya mambo kisiasa zaidi na ni lazima tubadilishe huo mfumo ili nafasi nyeti kama hizi zianze kuwatumikia Watanzania na si CCM?
 
Minyororo na Pingu za utumwa wa mawazo, kunyimwa haki na kutawaliwa kwa matakwa ya CCM imevunjwa, ndio maana Kikwete hakuamini kilichotokea!

Ingawaje kwa sasa, kitendo kile kinachukuliwa kama jambo la juu juu tu!

Lakini;

Baada ya muda na tathimini kufanywa ... Itakubalika kwa Watanzania wengi kuwa Ile ni mbegu ya Uhuru na ukombozi wa Tanzania kwa ujio wa mara ya pili ...baada ya ule wa 1961. Ni Ujumbe wenye kina na unaofikirisha wakati wote bila kikomo...na ujembe murua kwa Rais ukiwa haufutiki wala kupungua kila muda unavyozidi kupita... Ni kazi nzuri kwa kweli!!
 
Mkavirondo siyo mswahili kama ambavyo mswahili siyo mkavirondo. Ebo! tuache uswahili maana yake nini? Yaani wote tuwe wakavirondo kama wewe? Mimi ni mswahili na nitaendelea kubakia kuwa mswahili.
 
Ingawaje kwa sasa, kitendo kile kinachukuliwa kama jambo la juu juu tu!

Lakini;

Baada ya muda na tathimini kufanywa ... Itakubalika kwa Watanzania wengi kuwa Ile ni mbegu ya Uhuru na ukombozi wa Tanzania kwa ujio wa mara ya pili ...baada ya ule wa 1961. Ni Ujumbe wenye kina na unaofikirisha wakati wote bila kikomo...na ujembe murua kwa Rais ukiwa haufutiki wala kupungua kila muda unavyozidi kupita... Ni kazi nzuri kwa kweli!!

Azimio,

Kila kazi ina gharama yake. Tulipogombea uhuru, kina Nyerere na wengine waligoma, mkoloni akawafukuza kazi, polisi wakanyanyasa watu lakini pamoja na yote hata kama kulikuwa na mapungufu, Uhuru ulipatikana disemba 9, 1961.

Hatya kama Chadema watu watadai ni kosa la ki-strategy au political suicide, lakini kitendo kina symbolism kubwa.
 
Rev.
Kabla sijajadili maada naomba nipate ufumbuzi kuhusu kichwa cha habari; unaposema "kuacha uswahili" unamaanisha nini?
Msingi wa swali langu ni kwamba, hatuwezi kupinga propaganda kwa kutumia propaganda.
 
Rev.
Kabla sijajadili maada naomba nipate ufumbuzi kuhusu kichwa cha habari; unaposema "kuacha uswahili" unamaanisha nini?
Msingi wa swali langu ni kwamba, hatuwezi kupinga propaganda kwa kutumia propaganda.

ZeMarco,

What is your take of Uswahili and how it was used?
 
ZeMarco,

What is your take of Uswahili and how it was used?

Rev.
Samahani kama swali limekukwaza.
Nimeuliza hivyo kwa sababu neno "uswahili" limetumiwa mara nyingi kipropaganda kuonyesha kuwa watu wa maeneo ya pwani (ambao huitwa waswahili) siyo watu makini na kwamba wamejaa mzaha mzaha tu. Sijafahamu wewe umelitumia kwa mantiki ipi.

Kiongozi,
Si lengo langu kutoka nje ya maada kuu uiyoileta.
 
ni bora kuchagua chama cha wachaga chadema ili waje watutawale kikabila,
maana cc ndo tunataka, kama ingekuwa sio wachaga zitto angeendelea kuwa kiongozi wa upinzani bungeni!!

Mwana JF, unaetegemewa kuwa muungwana, mbona unapotosha hoja ya msingi katika uzi huu? Mambo ya ukabila yametokea wapi Emma. Acha tabia hiyo muungwana. Kama unania njema jadili hoja iliyopo tujenge chama na hatimaye nchi yetu iwe nzuri. Haifai Emma, ACHA!
 
Rev.
Samahani kama swali limekukwaza.
Nimeuliza hivyo kwa sababu neno "uswahili" limetumiwa mara nyingi kipropaganda kuonyesha kuwa watu wa maeneo ya pwani (ambao huitwa waswahili) siyo watu makini na kwamba wamejaa mzaha mzaha tu. Sijafahamu wewe umelitumia kwa mantiki ipi.

Kiongozi,
Si lengo langu kutoka nje ya maada kuu uiyoileta.

ZeMarcopolo,

Tafsiri ya kuwasanifu watu wa pwani si sahihi maana uswahili ni wetu sote Watanzania. Hakuna tofauti kati ya Mkaguru, Muha, Mnyaturu au Mzaramo na Mndengereko au hata Mkwere.

Ni tabia yetu sisi kama Taifa na ni makosa kuifanya ni eneo la ukanda wa pwani pekee.

Sas nikirudi kwenye hoja, ninachozungumzia ni ukosefu wa umakini na ni kuhusu Watazania na hapa nalenga kwa watu wa CCM an sina maana ya kuwasanifu au kuwadharau watu wa pwani. Hata mimi ni Mswahili, naongea lugha kiswahili, lakini Uswahili kama tabia ya kukosa umakini si haiba yangu.
 
Minyororo na Pingu za utumwa wa mawazo, kunyimwa haki na kutawaliwa kwa matakwa ya CCM imevunjwa, ndio maana Kikwete hakuamini kilichotokea!

Sidhani kama Rais Kikwete hakuamini kilichotokea kwani siamini kuwa alikuwa hajui kuwa hicho kitatokea.......System yetu ina mapungufu lakini sio kiasi hicho cha kushindwa kudetect ama kujua hilo na kumuarifu Rais...na kama ni hivyo basi ni lazima watu wawajibishwe hata kabla hatujaingia hiyo hatua ya kumfungulia jini kutoka kwenye kibuyu......Mabadiliko ya Katiba...

By the way, madai ni katiba mpya ama mabadiliko ya katiba?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom