Tukubali yaishe?

I remember this too. Na nimekuwa nikijiuliza ni mwanakijiji yule wa bcs au? Kule nakumbuka kulikuwa na wanachama wawili wa CCM walikokuwa wanabishana juu ya nani anaijua zaidi CCM yaani Manakijiji na Mzee ES, je, unaikumbuka hii Nyani? Lakini sasa nilifikiri sio yule mwanakijiji wa kule. Kwa sababu kule kulikuwa na Mwanakijiji halafu baadaye akaibuka Mzee Mwanakijiji ambaye nafikiri ndiye huyu tuliye naye hapa. Naendelea kuamini kwamba kuna tofauti kati ya Mwanakijiji (kada wa CCM kule bcs) na Mzee Mwanakijiji (Thinker, debator, writer, lover of his country, controversial as he could be) ambaye ndiye huyu tuliye naye hapa.

Mzee Mwanakijiji unaweza kunitegulia hiki kitendawili msee wangu?

Yaa nakumbuka bwana...tena alikuwa anajivunia uchipukizi wake na kukimbiza mbio za mwenge....
 
dadangu we, ni uamuzi wa machozi.. sasa hivi nimeoda kakofia kangu ka kijani kenye nembo ya jembe na nyunzo za rangi ya njano. Halafu shati litakuwa kama lile la Lowassa la rangi ya kijani kibichi (lime) la kumeta meta.. tatizo langu kubwa sijui kama nitapewa nafasi ya kufungua mdomo au ndio nimejikatia leseni ya ukimya..

Yaani it's so funny!

Hilo shati la lime naona limekaa funny tu. Chonde chonde Mkjj, tuna historia ndefu pamoja, naomba uwaombe wakubwa wakuruhusu uvae shati la rangi tofauti.

Yaani wewe na kijani hamuendani kabisaaaa. Afadhali uvae suti ya kijivu kama zile za Nyerere (RIP)

Good luck though! It's sad but what should I say. Kitu kimoja tu kinatia moyo ni kuwa at least ccm watapata mtu mwenye bollz
 
mzee Nyani, ushabiki wangu wa Kikwete haukuwa na kificho na mapenzi yangu kwa CCM sijawahi kuyaficha. Hata hivyo muda huo wote SIKUWA MWANACHAMA nilikuwa shabiki tu hasa ukizingatia nililelewa ndani ya CCM na kunyweshwa maji ya bendera. Na kwa muda wote sijawahi kuwa na kadi yoyote ile isipokuwa ya CCM niliyopewa miaka ileeeeee wakati natakiwa kwenda mafunzo ya Mgambo!(ila ilishaexpire baada ya kuukimbia mwenge 1984).

Niliomba kujiunga na CCM mapema mwaka huu lakini wakanipa masharti magumu gumu hivi ya kucompromise some of principles nikagoma tu. Ila sasa wataka au wasitake nitajiunga nao humo humo... kwani naamini ninatimiza masharti yote ya kuwa mwanachama.

Hreat ! baab kubwa !
 
Yaani it's so funny!

Good luck though! It's sad but what should I say. Kitu kimoja tu kinatia moyo ni kuwa at least ccm watapata mtu mwenye bollz
wewe mwk, usije ukanifanye nami nianze kuamini hii habari, could it be serious? difficult to comprehend hiyo kitu!
 
I remember this too. Na nimekuwa nikijiuliza ni mwanakijiji yule wa bcs au? Kule nakumbuka kulikuwa na wanachama wawili wa CCM walikokuwa wanabishana juu ya nani anaijua zaidi CCM yaani Manakijiji na Mzee ES, je, unaikumbuka hii Nyani? Lakini sasa nilifikiri sio yule mwanakijiji wa kule. Kwa sababu kule kulikuwa na Mwanakijiji halafu baadaye akaibuka Mzee Mwanakijiji ambaye nafikiri ndiye huyu tuliye naye hapa. Naendelea kuamini kwamba kuna tofauti kati ya Mwanakijiji (kada wa CCM kule bcs) na Mzee Mwanakijiji (Thinker, debator, writer, lover of his country, controversial as he could be) ambaye ndiye huyu tuliye naye hapa.

Mzee Mwanakijiji unaweza kunitegulia hiki kitendawili msee wangu?

ndiyo sasa hivi nitakuwa Kada Mwanakijiji... nitajenga hoja za kwanini CCM inastahili kuendelea kuila nchi, na kwanini viongozi wake wametumwa na Mungu kutuongoza kuelekea nchi ya ahadi. Kama Kada mpya wa CCM natatajia kuwaelewesha wapinzani kuwa CCM ndiyo chama kilichobarikiwa na "aliye juu" kututawala na hakuna chama kitakachoweza kututawala kwa amani. Kama Kada mpya wa CCM nitatetea chama changu kwa mabaya au mema ili wapinzani wasipate nafasi yoyote ile. Nitapangua hoja za Buzwagi na Karamagi na kuonesha ni kwanini hazina msingi hasa kwa kutozijibu moja kwa moja isipokuwa kwa kuonesha kuwa ni hoja za wapinzani na kwa vile ni za wapinzani basi hazina muda wa kujibiwa!

kwangu mimi CCM ndiyo alfa na omega! cha kwanza na cha mwisho!
 
MMJ

Kama ni kweli umeamua hivyo nakushauri hili''Kaa nao, kula nao, tembea nao ila usifanane nao''.

Na falsafa ya hoja hujibiwa kwa hoja naona imekushnda tafuta falsafa ingine
 
ndiyo sasa hivi nitakuwa Kada Mwanakijiji... nitajenga hoja za kwanini CCM inastahili kuendelea kuila nchi, na kwanini viongozi wake wametumwa na Mungu kutuongoza kuelekea nchi ya ahadi. Kama Kada mpya wa CCM natatajia kuwaelewesha wapinzani kuwa CCM ndiyo chama kilichobarikiwa na "aliye juu" kututawala na hakuna chama kitakachoweza kututawala kwa amani. Kama Kada mpya wa CCM nitatetea chama changu kwa mabaya au mema ili wapinzani wasipate nafasi yoyote ile. Nitapangua hoja za Buzwagi na Karamagi na kuonesha ni kwanini hazina msingi hasa kwa kutozijibu moja kwa moja isipokuwa kwa kuonesha kuwa ni hoja za wapinzani na kwa vile ni za wapinzani basi hazina muda wa kujibiwa!

kwangu mimi CCM ndiyo alfa na omega! cha kwanza na cha mwisho!

Now you are talking. Tumekuelewa sasa, acha akina kada original waendelee kushangilia ushindi hewa!
 
Mwanakijiji...ungesubiri kuitoa hii April fools day....you've made Kada very excited
 
mwanakijiji usitake watu hapa waanze kuchoma kurasa kama ile ahadi ya picha !!

kwanza wee nshakuona haukwolifai kuwa memba bana ! baki huko huko uliko kwenye kiza !
 
wewe mwk, usije ukanifanye nami nianze kuamini hii habari, could it be serious? difficult to comprehend hiyo kitu!

Kitila,

dont worry! Mwanakijiji ameshakuwa memba wa hii secret society ambayo inapigana kuikomboa Tanzania. Hakuna chochote kibaya zaidi kinachoweza kutokea hapa kwa yeye kujiunga ccm.

Sina hakika kama ni kweli hili maana so far nafuatilia kujua Mwanakijiji alilala wapi jana hadi akaamuka na haya mawazo ya ajabu. Sheria za kazi ziko palepale. Mkjj kwenda CCM will be the best thing to ever happen kwa upinzani.

Subiri tu usikie yatakayotekea huko ingawa so far nimeshavunja mbavu kuimagine Mwanakijiji akiwa in yellow and green!
 
Mwanakijiji...ungesubiri kuitoa hii April fools day....you've made Kada very excited

no no, leo ameamka hakuna nyuzi yoyote, hana kitu cha kuikosoa serikali ilibidi achangamshe baraza, na kwa kuwa wakuu wa barza wapo hapa wakipata gahwa wengine tulishaelewa where the ball was rolling to !
 
Yaani it's so funny!

Hilo shati la lime naona limekaa funny tu. Chonde chonde Mkjj, tuna historia ndefu pamoja, naomba uwaombe wakubwa wakuruhusu uvae shati la rangi tofauti.

Yaani wewe na kijani hamuendani kabisaaaa. Afadhali uvae suti ya kijivu kama zile za Nyerere (RIP)

Good luck though! It's sad but what should I say. Kitu kimoja tu kinatia moyo ni kuwa at least ccm watapata mtu mwenye bollz

you know what.. labda sitovaa hilo kwa heshima yako ila naweza kuweka kitambaa cha kijani kwenye mfuko wa shati just in case nitaulizwa my loyalty to the party? Hili la my bowlz mbona unalirudia rudia wasije wakanihasi wenzao halafu nikawa sina bowls anymore..
 
duh ! subiri nkalale mie ! naona watu washanitayarisha !

kama alivyosema MVIZIBO, sign out, kunywa kikombe cha chai then rudi, thats what i'll do !
 
mwanakijiji usitake watu hapa waanze kuchoma kurasa kama ile ahadi ya picha !!

kwanza wee nshakuona haukwolifai kuwa memba bana ! baki huko huko uliko kwenye kiza !

kada eh!! yaani umenikaribisha kwa mikono miwili halafu hata kurasa moja haijaisha umenitimua? Mbona unaanza kunitisha kwenye chama chetu.. bana miye sirudi huku kwenye "giza" nataka nikae na nyie wenye mwanga bana..!
 
kasungura kapo,kanawasubiri kina Mwanri,makamba na Rostam ..mwanakijiji hakuna share yako,
ndanda akikujua tu,umekwisha
 
Huko wanakula bila kunawa uko tayari kukabiliana na hali mpya ya mfumo wa maisha?

Humo ukienda lazima wakupige japo kapicha kamoja wakaweke kwenye gazeti la uhuru na pia siwezi kuimagine kuwa katibu mkuu wako atakuwa makamba.....
 
Back
Top Bottom