Tuko wangapi ya mastaa bongo!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
. Chalz na Anti


WAKATI kampeni ya kupinga mapenzi ya mnyororo kwa wapenzi wengi inayoitwa Tuko Wangapi? Tulizana ikiendelea, utafiti uliofanywa umeonesha kuwa baadhi ya wasanii na mastaa Bongo, si mfano wa kuigwa kwani ndiyo wanaoongoza kwa kuwa na ‘mabebi’ wengi wakibadilishana mithili ya siti za daladala, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.
Utafiti wa gazeti hili umefumua mnyororo wa kila mmoja na hapa linauachia ili wahusika wajirekebishe:

WEMA
Wema Isaac Sepetu alitajwa mara nyingi zaidi akihusishwa kuunganishwa kwenye minyororo kuanzia kwa marehemu Steven Kanumba, Jumbe Yusuf Jumbe, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’, Hartmann Mbilinyi, Charles Baba ‘Chaz’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambao nao walikuwa na wapenzi wengine, utawaona chini.

DIAMOND
Jamaa alianzia kwa Rehema Fabian, wakafuatia Pendo Mushi wa Maisha Plus, Jacqueline Wolper, Natasha, Wema, Jokate Mwegelo na sasa yupo kwa Wema tena. Watajwa wote hao nao walikuwa au wapo na wapenzi wengine.

MAREHEMU
Kanumba alitajwa na Wema, Nargis Mohamed, Sylvia Shally, Shalz na baadaye Elizabeth Michael ‘Lulu’. Nao walikuwa au wana wapenzi wengine.

JOKATE
Alitajwa na Hasheem Thabeet, Mbongo Fleva, Padri na Diamond. Nao wapo na wapenzi wengine baada ya Diamond kuunganishwa tena kwenye ule mnyororo wa Wema.
AUNT
Kwa upande wake, Aunt Ezekiel alianzia kwa Jack Pemba (mume wa mwanamke Mzungu), Hartmann (mume wa mtu), Mwilu Mwilola ‘Silva’ (mume wa Sarah Mwakapala ‘Bukabi’ ambaye naye (huyo Sarah) alikuwa na Mzungu wake), akaenda kwa Geofrey ‘Jeff’ na sasa Sunday Demonte. Wote hao walikuwa au wana wapenzi wengine.

WOLPER
Alitajwa kutoka na Diamond, Mjomba na sasa yupo kwa Dallas. Kwa Diamond ndipo alipounganishwa na watu wengi zaidi wakiwamo Wema, Jokate, Rehema Fabian, Natasha na Pendo.

CHAZ BABA
Jamaa aliunganishwa kwenye mnyororo wa Wema uliokuwa na akina Jumbe, Kanumba, Hartmann na Diamond lakini kabla ya hapo alikuwa mwandani wa Husna Iddi ‘Sajenti’, marehemu na sasa yupo na kifaa kingine.

MR CHUZ
Kazi kwelikweli, hapa pakawa mwisho wa matatizo, wakatajwa Leila Ismail ‘LiLy wa Mambo Hayo’, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’, Rose Michael ‘Rose wa Chuz’ na sasa ana demu mpya. Hao wote, nao walikuwa au wapo na wapenzi wengine.

LULU
Kwa Elizabeth Michal ‘Kalulu Kadogo’, walitajwatajwa watu lakini mbali na Kanumba aliunganishwa kwa Ali Kiba ambaye naye alikuwa na Devotha wake.

JINI KABULA
Kutoka kwa Mr Chuz alikoacha mtoto, Jini Kabula akamvaa Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ (aliyekuwa na Lulu John na Rehema Fabian baada ya yule marehemu), akatajwa na msagaji Waukweli na sasa kabeba mimba ya msanii wa siku nyingi wa Bongo Fleva.

JACK CHUZ
Kutoka kwa Mr Chuz wa Lily, Jini Kabula, Wema, Rose na demu mpya, Jack Chuz akatua kwa Ally Timbulo ambaye naye alishatajwa na Isabella Francis ‘Vai’.

TULIZANA
Ijumaa Wikienda halina nia ya kumhukumu mtu isipokuwa linaunga mkono kampeni ya kuteketeza tabia ya watu kuwa na wapenzi wengi inayoongeza maambukizi mapya ya Ukimwi, iliyoratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na PSI TANZANIA, USAID, TACAIDS na KFW. Tupo Wangapi? Tulizana!
TUKO WANGAPI YA MASTAA BONGO! - Global Publishers
 

Attachments

  • TUKO.jpg
    TUKO.jpg
    96.5 KB · Views: 136
  • chuzijack.jpg
    chuzijack.jpg
    30.7 KB · Views: 82
  • diamond.jpg
    diamond.jpg
    34.1 KB · Views: 97
  • woperlulu.jpg
    woperlulu.jpg
    34.2 KB · Views: 89
Diamond hajawahi kuwa na J.Wolper(in his dreams i'm not sure though) but in this 3D real world never, alianza kuzusha ye mwenyewe ili apate tittle mpaka plan zilipo back fire akaambulia ma2si ya nguoni. Check ur sources
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom