Tukiwa na viongozi wasiojiamini

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
522
239
Watanzania wengi sana leo wajiuliza: Hivi katika uongozi wa mwalimu haya tunayo yaona sasa yalikuwepo? Mfano, sehemu ya nchi kuamua kujiita ni nchi kwa kuvunja katiba kwa wazi kabisa na kuachwa bila kuchukuliwa hatua.

Watu wa kikundi fulani kuamua kuharibu mali za watu wa kikundi kingine na kuambiwa tu waache hayo mambo bila kuchukuliwa hatua inayoonekana. Viongozi kuiba mali ya umma na kuishia kuwabembeleza kuachia nyadhifa eti uchunguzi wa kishikaji ufanyike.

Ujambazi kukithiri hata mchana kweupe watu kunyang'anyawa mali zao. Watu kuuawa na kuacha mambo yapite kana kwamba ameuawa nzi na si binadamu!

Hivi mwalimu angekuwepo haya yangetokea? Hivi kweli mwalimu angekuwepo watu wangepewa adhabu eti kosa kuzaliwa katika eneo lenye dhahabu kama kule Mara? Hivi mwalimu angekuwepo watu wangefukuzwa kutoka maeneo walozaliwa eti kupisha wanyama pori waendelee kujitanua ili wazungu waje kufurahi? Kufukuza bila fidia! Hivi kweli kungekuwa kuna mtu hajalipwa fidia ya mabomu Gongo la Mboto?
 
Back
Top Bottom