Tukipiga marufuku majenereta na matanki ya "SIMS", tutatatua tatio la umeme na maji

Nasikita sana ninaposikia citizen wakii blame Tanesco kwa mgao wa dharura uliotangazwa hivi karibuni. Mimi na suggest tuangalie kwa undani matatizo yanayolikabili shirika hili. wana vyanzo vile vile 5 vya kuzalisha umeme (Pangani, mtera, kihansi, kidatu & nyumba ya mungu - vinategemea standard ya ujazo wa maji kuweza kuoperate) pamoja na mtambo wa thermal hapo ubungo, huku mahitaji yakiwa yameongezeka maradufu kwa wateja wa nyumbani, viwanda, mashirika/makampuni, miradi, migodi etc. uwezo wao wa kuzalisha hauwiyani hata kidogo na mahitaji ya sasa. nadhani wanahitaji kuanzisha vyanzo vingine ambavyo ni huge investment (monetary) je watawezeshwaje? kama sikosei mashirika binafsi yamesharuhusiwa kuingia kwenye biashara ya umeme, sasa wako wapi?? please MM naomba tujadili kwa undani zaidi
 
Mnafikiri ni kwa haraka kiasi gani watawala wetu watajaribu kutatua tatizo la umeme na maji endapo majenereta na matanki ya maji yatapigwa marufuku mijini? I bet you very soon...wouldn't you agree?

Niliwai kuwa na wazo hizi nyumba za watendaji wa serikali zingejengwa sehemu mbali mbali. hata haya matatizo ya maji na umeme yasingekuwa sugu kama sasa hivi. OK mawaziri wakae masaki. Nyumba a makatibu , wakurugenzi na wengineo kwa nini sizijengwee chache chace maeneo tofauti ya jiji. Sinza,tandika Mbagala, ubungo kinondoni Kawe,etc

huu Mchezo wa kukusanya nyumba zote sehemu moja ni chanzo cha upendeleo Ubaguzi na kukwepa majukumu kwa watendaji
 
Ni kufikiria jinsi gani jamii hasa watendaji wetu wakubwa wa serikali ambao kwao umeme siyo tatizo wala maji siyo tatizo wataona umuhimu wa kutafuta suluhisho? Watu binafsi sina tatizo kabisa wao wanapata vipi umeme lakini watendaji wa serikali (nafikiria wale wa Tanesco) hili kweli hawana majenereta majumbani kwao na hivyo umeme unapokatika wao wenyewe haiwagusi?

Nasikita sana ninaposikia citizen wakii blame Tanesco kwa mgao wa dharura uliotangazwa hivi karibuni. Mimi na suggest tuangalie kwa undani matatizo yanayolikabili shirika hili. wana vyanzo vile vile 5 vya kuzalisha umeme (Pangani, mtera, kihansi, kidatu & nyumba ya mungu - vinategemea standard ya ujazo wa maji kuweza kuoperate) pamoja na mtambo wa thermal hapo ubungo, huku mahitaji yakiwa yameongezeka maradufu kwa wateja wa nyumbani, viwanda, mashirika/makampuni, miradi, migodi etc. uwezo wao wa kuzalisha hauwiyani hata kidogo na mahitaji ya sasa. nadhani wanahitaji kuanzisha vyanzo vingine ambavyo ni huge investment (monetary) je watawezeshwaje? kama sikosei mashirika binafsi yamesharuhusiwa kuingia kwenye biashara ya umeme, sasa wako wapi?? please MM naomba tujadili kwa undani zaidi
 
Naungana nawe Chapakazi, dawa ni kuishinikiza Serikali iache ukiritimba kwenye huduma hii, iruhusu makampuni binafsi yaingie, yazalishe na kusambaza umeme kama zilivyo kampuni za simu! Haja jeuri ya TANESCO itakwisha kama TTCL!

Umechangia kama ABUNUWASI vile! Labda kama kuna umeme wa kusafirisha bila kutumia nyaya ilo litawezekana. Ipo ARTMUS wapo uko Mtwara.
 
Ah, sidhani kama kupiga majenereta/matanki ya maji marufuku bila kwanza kutafuta alternative, itakuwa njia nzuri ya kumaliza hili tatizo.Nadhani tunachotakiwa kufanya ni kui-push serikali itafute alternative ya kutatua tatizo hili once and for all.
 
Kama wakipiga marufuku majenereta na matanki kwa sasa ni wazi watakwamisha shughuli nyingi sana,mkumbuke hayo majenereta yamegaramiwa na yanachangia katika uzalishaji hasa ukizingatia nishati hapa kwetu ni jambo tata sana.Umeme na maji ni vitu muhimu sana,vinahitaji sera na mipango imara ya muda mrefu,embu fikiria wakati wa shida ya umeme 2006 ikaletwa richmond kwa dharura baada ya mvua kunyesha hakukuwa na mpango wowote endelevu wa kukabiliana na tatizo lisitokee tena.Kama mmemsikiliza Badra Masoud sababu za mgao ni zile zile za kila siku hivyo ni wazi matatizo yanatatuliwa on subsistence basis na si kwa kufocus mbele.Pia sector hii ina matatizo mengi sana toka huko nyuma ikiwemo uendeshaji mbovu,mikataba mibovu,ubadhirifu na serekali kutolipia huduma hiyo.Mpaka hapo serekali itakapoyarekebisha matatizo yaliyopo na kupanga mipango endelevu na usimamiaji thabiti ukawepo ndipo nuru ya matumaini itakuwepo.Halafu tz ukiiangalia kwa ujimla wake inakuwa kama tunarudi nyuma,kuna vitu vingi sana tumekuwa navyo kutoka kwa wakoloni na pale vilipochakaa au mahitaji kuongezeka tukashindwa kufanya replacement,mfano miundo mbinu jijini dar ni ile ile ya mkoloni wakati idadi ya wakazi na shughuli zilizopo zimezidi hata mara kumi ya matarajio yaliyokuwepo wakati mji unajengwa kwa mara ya kwanza.Inatakiwa serekali makini na yenye dhamira kuyafikia haya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom