Tukio la Walimu wa Mwaka jana kuajiriwa tena (wahitimu wa MUCE)- Serikali iko makini?

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Wakuu kama wote tunavyofahamu, juzi Jumatano majira ya saa 3 hivi usiku Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitoa orodha ya Walimu waliopangiwa kwenye vituo vipya vya kazi. Ni jambo jema sana kwa wale waliobahatika kupangiwa vituo.

Hata hivyo kuna jambo lisilo la kawaida limejitokeza. Ni kwamba Wahitimu wengi kama sio wote wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) wa mwaka 2010/2011 hawajapangiwa vituo vya kazi. Badala yake waliopangwa ni wale wa 2009/2010 yaani ambao tayri wapo kazini tangu Januari mwaka 2011. Nina wafahamu kwa majina, sura, vitu vyao vya kazi na Chuo walichosoma (MUCE) watu kama 6 hivi ambao tena wamepangiwa upya vituo mbali mbali vya kazi.
Ninayo Maswali hapa kwa Wizara zote zilizohusika na mchakato huo yaani TAMISEMI, MOEVT, PO-PSM na MOF..
1. Muda wote toka wahitimu hawa walipojaza fomu zao serikali haikugundua tatizo hilo?
2. Kama zoezi rahisi tu hili limeshindikana, itawezekana vipi kuondoa hicho kinachitwa watumishi hewa?
3. Je, huu sio mwanay wa Wakurugenzi wa Halmashauri kula fedha za serikali pale ambapo walimu hawa hawataripoti kwenye vituo vyao vya kazi?
4. Tumeambiwa kuwa majina yote ya walimu wenye shahada yanarekebishwa leo ili kuondoa huo utata, je huo sio mwanya wa kukaribisha mazingira ya rushwa/
5. Kuna njia zipi zilizowekwa kuhakikisha kwamba zoezi hili linakamilika kwa wakati li walimu watakaoajiriwa wapate haki yao kwa wakati?
6. Serikali ipo tayari kueleza nini kilipelekea hali hii?

Na mengine mengi
 
Watu uwa wanaomba tena,we jaribu mwaka huu,utaona mambo yanakua poua,kama vp ichunie tu,
 
Ni haki yako kulalamika mkuu ila kumbuka wao pia ni wanadamu wanafanya makosa, makosa hutokea mkuu hasa pale ambapo wanakuwa under pressure.Mimi nafikiri Serikali kwenye hili imejitahidi jamani hayo matatizo hehu tuwape muda wajirekebishe, tukiwa watu wa kulaumu tu haipendezi.
 
Haipendezi kulalamika na kukosoa? Au unategemea tusifie uzembe kama huu? Maana kungekuwa na taratibu za kuwajibishana uzembe kama huu kamwe hautorudia wala kujitokeza tena
 
Hawa si bin adam so makosa ni sehemu ya maisha ye2.

Embu serikali ifanye kuwe na utaratibu wa kuwajibishana tuone kama makosa haya mnayodai ni ya kibinadamu yatajitokeza tena
 
kwanini tuitetee serikali??? Makosa ya kibinadamu yanatoka wapi?? Wametumia muda mrefu kupangia watu vituo tofauti na miaka mingine.. Mbaya zaidi wanawapanga tena wa2 walio kazini wakati wahusika kibao wameachwa bila kazi /case study makumira + mkwawa...
HATUWEZI TETEA WAPUMBAVU SISI
 
wadau wa jamii forum kuna vyuo kama makumira tawi la tumaini wamepangiwa watu sita tu kati ya watu mi 400 kweli serikali aipo makini
 
Ni haki yako kulalamika mkuu ila kumbuka wao pia ni wanadamu wanafanya makosa, makosa hutokea mkuu hasa pale ambapo wanakuwa under pressure.Mimi nafikiri Serikali kwenye hili imejitahidi jamani hayo matatizo hehu tuwape muda wajirekebishe, tukiwa watu wa kulaumu tu haipendezi.
Kwanza niweke wazi mimi sio Mwalimu wala sina tatizo la ajira as already nipo kazini. Pili nakupongeza sana kwa kuwa na imani iliyovuka mipaka. Hivi kosa la wazi kama hilo na watu walikuwa na muda mrefu tangu Mei mwaka uliopita utasemaje walikuwa under pressure? Kweli Mtanzania hata ukiingilia ndoa yake hawezi kuingia mtaani
 
hao wamehonga wapangwe upya kwenye vituo vya kazi vizuri.this goverment is full of crap
 
ata mwaka juzi ilikuwa hivi then wanajidai waalimu wameripoti na kukimbia baada ya kuchukua pesa ya kujikimu,kumbe ni mbinu yako.mi najua watu 6 ambao waliajiri mara ya pili,hawakwenda ila majina yao yametoka kwny magazeti eti wamekwenda wakachukua pesa ya kujikimu na kuondoka,wakifutia wanaambiwa ni makosa ya uandishi then mwaka huu wamerudia yale yale
 
Duh kweli mwalimu ni mwalimu..mjaasili aachi asili(unoko)..sasa labda mtu alipangiwa mara ya kwanza hakuenda na sasa kaomba tena kapata,shida iko wapi?au ao watu sita ndio wamezibia nafasi za watu buku4??..ila jamani tunapoelekea kiukweri sio pazuri,juzi juzi tu apa walimu walikuwa wanabembelezwa,leo wao ndio wanatoana ngeu kugombea nafasi tena bado wanapotezewa...smthing must be done kwa kweli,la sivyo nchi itayumba.
 
Hata hujaeleweka!!! Issue sio watu 6. Nilikuwa najaribu kutoa mfano, hao 6 wapo kazini tena wamepangiwa vituo vizuri vya kazi. Ukweli ni kwamba Wahitimu wa MUCE wa mwaka huu hawajaariwa na badal yake wakaajiriwa ambao tayari wapo kazini? Au kwako wewe hilo ni tatizo dogo? Nisisitize hapa Mimi sio Mwalimu na wala sina mdogo wangu, ndugu au jamaa aliyekosa post ila najiuliza tu zoezi lililofanywa kwa siku zote hizi linakuwaje na dosari kubwa hivi?
 
Wanajua kabisa wanachofanya hii yote ni kujitengenezea namna ya kuwezan kujiongezea pesa chafu kupitia majina ya wengine halafu wanakuja kupata tabu walipa kodi kwa watu wachache tena walafi zaidi. Tunaomba serikali iwe korofi tena sana bila kuonesha jino nje maana walaji wanapongezwa na kuchekelewa wakati wafanya kazi wanatishiwa kazi zao na hata wakitaka kuandamana wanaambiwa watapigwa viboko kama sio kupigwa na risasi.
 
Back
Top Bottom