Tukio la Ujambazi lililofanikiwa zaidi, kusisimua na kuushangaza Ulimwengu

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,671
Sasa, unaweza kupata nakala za Kitabu changu cha "NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI".
kitabu kina kurasa 442 na ndani yake kuna makala 17.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 50,000/-

Pia waweza kupata kitabu changu cha "OPARESHENI ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI"
Kitabu hiki kina kurasa 214 na ndani yake nimechambua Oparesheni 6 tofauti.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 15,000/-

Wasiliana nami kwa namba 0759 181 457


Mwaka 2003 lilitokea tukio kubwa zaidi la ujambazi ambalo labda ndio lililotumia akili na maarifa zaidi pengine kushinda tukio lolote la ujambazi kwa miaka 50 iliyopita.. Tukio hili lilishuhudia wahusika wakitokomea na vitu vyenye thamani ya zaidi ya Bilioni 200 (100 mln USD)!
Uthubutu, ubunifu, akili na maarifa yaliyotumika kutekeleza tukio hili limefanya mpaka kampuni ya utengenezaji filamu ya Paramount Pictures kununua haki za hadithi ya tukio hili ili watengeneze filamu itakayo husu mkasa mzima wa tukio hili..

TUKIO LENYEWE

Mwanzoni mwa mwaka 2000 mfanyabiashara wa madini (almasi) Leonardo Natarbartolo alifungua ofisi mjini Antwerp nchini ubelgiji, mji ambao ndio kituo cha biashara ya madini ya almasi ulimwenguni.. Ofisi yake ilikuwa katikati kabisa ya kitovu cha mitaa ambayo ndio hasa biashara ya almasi hufanyika. Natarbartolo alijihusisha hasa katika manunuzi ya kiwangi cha kawaida cha almasi (small deals) lakini jambo ambalo watu hawakulifahamu ni kwamba walikuwa wamemkaribisha moja kati ya manguli wa wizi wa almasi ulimwenguni!
Kutokana na kujitambulisha kama mfanya biashara mwenzao, Natarbartolo alipata fursa ya kuingia katika Kuba (vault) za wafanyabiashara wengine ili aweze kukagua mali kabla ya kuinunua na aliutumia fursa hii kuyasoma mazingira ya Ofisi hizo zilizo hifadhi madini na kuja kufanya uhalifu kesho yake..
Natarbatolo aliishi hivi mjini Antwerp kwa miezi kadhaa kabla hajakutana na mfanyabiashara ya almasi Myahudi ambaye kukutana kwao kulipelekea kufanikisha tukio ambalo liliushangaza ulimwengu na limeendelea kuushangaza ulimwengu mpaka leo hii..



MAANDALIZI

Mwaka mmoja baada ya Natarbatolo kuingia Antwerp, siku hiyo akiwa kwenye mgahawa akinywa kahawa alifuatwa na Mfanyabiashara wa Kiyahudi ambaye alimuomba wazungumze faragha kuhusu biashara muhimu. Baada ya kukaa nae chemba Myahudi akamueleza amza yake kuwa anataka amshirikishe katika tukio la ujambazi na alimuuliza kama anahisi Vault ya Antwerp Diamond Center inaweza kuibiwa... Natarbartolo akamjibu kwa kifupi kuwa atamjibu swali hilo kama yuko tayari kumlipa dola laki moja! Na Myahudi huyo akakubali

Siku mbili baadae Natarbatolo alielekea ilipo Main Vault ya Antwerp Diamond Center (kumbuka kutokana na yeye kujitanabaisha kama mfanyabiashara ya almasi kwa mwaka mmoja aliokaa Antwerp hivyo alifanikiwa kujisajili ili aweze kuhifadhi almasi zake katika Main Vault ya Antwerp)..
Kitu ambacho watu wote wakiwepo walinzi hawakikugundua ni kwamba katika mfuko wa pembeni wa suti yake aliweka peni ambayo inaonekana kama peni ya kawaida lakini ilikuwa ni peni maalumu iliyokuwa na kamera ndogo ya siri.. Kamera hii ilimsaidia Notarbartolo kurekodi mandhali yote ya ndani ya vault na jinsi ulinzi ulivyo...
Kesho akajutana na yule myahudi na kumpa jibu lake kuwa ni immposible kuvunja na kuiba main vault ya Antwerp inayohifadhi almasi zote zilizopo katika mji huo.. Akampa ile peni ambayo imerekodi mandhali ya Vault pia akampa na maelezo ya mdomo kwanini haiwezekani kuiba katika ile vault na akamsisitiza zaidi juu ya matabaka ya ulinzi (security levels) ambayo yana protect vault hiyo. Matabaka hayo yapo kama ifuatavyo..

1) Combination dial ambayo unatakiwa uingize tarakimu nne za siri

2) Sehemu ya kuingiza funguo maalum

3) Sensor ya mitetemo (seismic sensor)

4) geti la Chuma lililo sambamba na mlangi

5) sensor ya sumaku (magnetic sensor)

6) Kamera ya nje ya mlango

7) Keypad ya kuzima alarm

8) sensor ya mwanga (light sensor)

9) Kamera ya ndani ya vault

10) sensor ya joto na mjongeo (heat & motion sensor)

Jumlisha; walinzi na ulinzi unaozunguka jengo hilo.. Natarbartlo akmsisitizia yule myahudi "..it is immposible to rob the Antwerp diamond center vault"..

TUKIO LILIVYOTEKELEZWA

Miezi kama mitano ikapita ndipo Notarbartolo akapokea simu kutoka kwa yule myahudi na safari hii alimuomba wakutane nje kidogo ya mji wa Antwerp... Baada ya kuonana yule myahudi alimchukua Notarbatolo mpaka kwenye nyumba moja inayofanana na ghala kubwa.. Ndani yake Notarbatolo alikuta kitu ambacho hakutegemea kabisa... Yule myahudi alikuwa ametengeneza replica inayofanana kabisa na main vault halisi ya kuhifadhia almasi ya hapo mjini Antwerp.. Pia akamtambulisha kwa watu watatu ambao pia aliwakuta hapo! Natarbartolo amekataa kabisa mpaka leo hii kutoa majina halisi ya watu hawa lakini anawasimulia kwa nicknames walizokuwa wanatumia, kulikuwa na The genius (huyu ni mtaalamu wa mambo ya kidigitali na eletroniki), kulikuwa na The monster ( huyu alikuwa ni mekanika na mtaalamu wa umeme) na kulikuwa na mzee wa makamo ambaye walimuita The King of Keys (huyu ni mtaalamu wa kufungua vitasa na makufuli ya aina zote pamoja na kufoji funguo)..
Yule myahudi aliwaambia kazi ya ile replica ni wao wafanye mazoezi na kuitafiti na hatimae wajue namna gani wataweza kuingia ndani ya vault ya Antwerp pasipo kugundulika..

Iliwachukua miezi mitano Natarbartolo na wenzake kufanya mazoezi na kutengeneza perfect plan itakayowawezesha kuingia katika vault na kuiba pasipo kugundulika..


SIKU YA TUKIO..

Siku moja kabla ya tukio, yaani February 14 2003 Notarbartolo alienda mchana kwenye vault kana kwamba kuna almasi ameenda kuhifadhi lakini akajitahidi akae karibu na kifaa cha kuhisi joto na mjongeo (heat/motion sensor) na kwa kutumia hair spray aliyoificha ndani ya jaketi lake akapulizia juu ya kifaa hicho hivyo kukifanya kisiwe na uwezo wa kuhisi mabadiliko yoyote ya joto au movement ndani ya vault...

Ilipowadia siku ya tukio lenyewe.. February 15
Notarbartolo na wenzake waliendesha gari mpaka karibu kabisa na jengo lenye vault! Jengo lilikuwa na ulinzi mkali kwa mbele lakini nyuma ya jengo hakukuwa na ulinzi mkubwa kwani watu wa ulinzi walikuwa na imani kubwa sana na teknolojia yao inayosaidia kulinda jengo lao..
Wote wakashuka kwenye gari isipokuwa Notarbatolo alibaki kwenye gari! Baada ya kushuka wote wakazunguka nyuma ya jengo ambako walitumia ngazi ambayo The genius alikuwa ameificha hapo mchana wake wakapanda mpaka ghorofa ya pili.. Baada ya wote kupanda katika balcony ya ghorofa ya pili ilibidi wakae mbali na madirisha kwani yote yalifungwa vifaa vya kuhisi joto na movement na vikigundua tu kuwa kuna mabadiliko ya joto au movement basi alarm inalia..
Alichokifanya The genius alichukua kitambaa kirefu kilichotengenezwa kwa polyester kujifunika na kusogolea kifaa kile cha heat and motion sensor.. Kutokana na yeye kujifunika kwa nguo yenye material ya polyester hii ilipelekea kifaa kile kushindwa kudetect kilichokuwa kinatokea na alipokifikia karibu kifaa kile akakifunika kabisa na nguo ile kwahiyo korido ikawa iko salama kwa wao wote kupita.. Wakafungua madirisha wakaingia ndani na kuanza kushuka ngazi kuelekea chini kwenye vault..

Baada ya kufika chini nje ya mlango wa vault ambako kulikuwa na giza kutokana na kuzimwa taa.. Wakatumia fursa hiyo kuzifunga kamera kwa mifuko meusi na kisha wakawasha taa.. Baada ya kuwasha taa ilikuwa sasa ni jaribio la kufungua mlango na hapa ndio wanatakiwa kuwa makini zaidi kwani wakikosea kitu kimoja tu maana yake alarm italia na mchezo utaishia hapo..

Kumbuka kuna matabaka kumi ya ulinzi wanayotakiwa wanayotakiwa kuyavuka mpaka waingie ndani.. Tabaka la kwanza ni lile la combination dial ambapo wanatakiwa waingize tarakimu nne za siri! Kabla ya siku hii ya tukio Natarbartolo alifanikiwa kumshawishi muhudumu wa vault wabadilishe mtungi wa tahadhali ya moto (fire extinguisher) jambo ambalo hawakulifahamu ni kwamba mtungi ule ulikuwa na gas ndio lakini ndani yake Natarbatolo aliweka kifaa maalumu kilichokuwa kinachukua data za kamera ya nje ya mlango wa vault! Kwa kutumia kifaa hicho Natarbartolo alinga'amua tarakimu nne za siri ambazo zilikuwa zinahizatijika kuingizwa... Kwahiyo waliingiza tarakimu nne na wakawa wamefanikiwa kwa hatua hii ya kwanza... Bado hatua tisa ili wafanikishe.!

Hatua ya pili chabgamoto ya pili ilikuwa ni namna gani wangeweza kudiable kifaa cha kuhisi usumaku (magnetic sensor) hii yenyewe ilitengenezwa katika katika hali ya kwamba plate moja ya sumaku iliwekwa kwenye mlango na nyingine ilifungwa kwenye ukuta pembezoni mwa mlango kwa maana ya kwamba mlango ukifungwa kunakuwa na magnetic field inatengenezwa pale katikati kwa maana ya kwamba kama mtu ukifungua mlango unadisturb ili magnetic field na alarm inalia...
Kwahiyo alichokifanya The genius alichukua plate ndogo ya aluminium aliyoitengeneza nyumbani alafu akaifunga na tape ya gundi kali na kunasisha katika zile plate za sumaku huku na huku yaani iliyopo ukutani na mlangoni (ametumia aluminium ili asiweze kudisturb magnetic field).. Baada ya hapo akafungua screw na zile plate na kuziweke pembeni ya mlango! Kwahiyo zile plate mbili bado zilikuwa na magnetic field katikati yake lakini zilikuwa zimewekwa pembeni ya mlango..
Kwahiyo tayari matabaka matatu yalikuwa yameshakuwa disabled bado matabaka saba.. Kumbuka kamera ya nje tayari ilishafungwa na mfuko mweusi.

Hatua ilifuata ilikuwa ni kudisable alarm inayo monitor seismic sensor na geti dogo la ndani. Kifaa hiki kilifungwa kama keypad pembeni kwenye ukuta, kilichokuwa kinatakiwa ni kuingiza tarakimu nne za siri kama pale juu kwenye mlango.. Tarakimu hizi za siri nazo walikuwa wameshazifahamu kwa kutumia kile kifaa kilichopo ndani ya fire extinguisher kwahiyo waliingiza tu tarakimu na tayari wakawa wamefanikiwa kudisable tabaka hili..

Shughuli ikabaki kwenye kufungua mlango kwa kutumia funguo.! Funguo iliyokuwa inatumika hapo sio kama funguo hii ya kuweka mfukoni.. Ilikuwa ni funguo kubwa yenye size sawa na mguu wa binadamu!
Sasa ilikuwa ni zamu ya The king of keys kufanya miujiza yake... Kumbuka kuna kifaa chao kile kilichopo kwenye fire extinguisher kinachorekodi kila kinachoendelea kwenye vault kwahiyo kabla ya siku hii ya tukio walikuwa na Picha halisi ya funguo ya mlango ilikuwa inafananaje.. Kwahiyo alichokifanya The king of chains ni kutengeneza funguo inayofanana kabisa na ile funguo halisi.. Lakini kabla hawajaijaribu hii funguo yao ya bandia The king of keys akawaeleza kuwa kwenye zile Picha za video walizonazo aligundua kitu kuwa kabla mlinzi hajafungua mlango ilikuwa lazima aende kwenye chumba kilichopo karibia na hiyo vault na The king of keys alitaka kujua alikuwa anaenda kufanya nini.. The king of keys alipoenda katika chumba kili hakuamini alichokikuta, ulikuwa ni uzembe wa kiulinzi ambao hakuutegemea utokee Antwerp.. Funguo halisi ya kufungua mlango wa vault ilikuwa imewekwa pale inaning'inia.
The king of keys alichukua funguo halisi akarudi kwenye vault na kuwasisitiza wenzake kuwa angeoenda watumie funguo ile halisi.. Kwahiyo wakachomeka funguo na kuizungusha kisha wakazungusha ringi (usukani) wa mlango wa vault na mlango ukafunguka bila hiyana.. Kwahiyo kwa nje ya vault walikuwa wamepita vizingiti vyote na kikibakia geti la Chuma lililopo baada ya mlango.. Geti hili ni mageti fulani hivi yanayotumika kwenye vault nyingi lenyewe linakuwa lina nondo dizaini kama madirisha yetu uswahilini ya nondo na mbao tofauti tu ni kwamba hili lilikuwa ni nondo na chuma pekee hakuna mbao.. Kwakuwa tayari walikuwa wamedisable kifaa cha kumonitor hili geti (pale ukutani unapoingiza tarakimu nne) kwahiyo hapa wakatumia nguvu tu kuliharibu na kuingia ndani..

Kwahiyo kwa walikuwa wamefanikiwa kupita matabaka yote ya ulinzi nje ya vault na wakibakiwa na matabaka machache ya ulinzi ndani ya vault ambayo ni Kamera ya ulinzi, sensor ya mwanga (light sensor) na sensor ya mjongeo na joto (heat & motion sensor)



#2

NDANI YA VAULT..

Baada ya ya kufanikiwa kufungua mlango wa vault kwa mafanikio kabisa sasa changamoto ilibaki ndani ya vault kukabiliana na matabaka matatu ya ulinzi kabla ya kuanza kufungua visanduku vya vilivyohifadhi almasi ambavyo navyo vilihitaji funguo na namba za siri..

Kumbuka kuwa siku moja kabla Natarbartolo alikuwa amepulizia hair spray kifaa cha kuhisi joto na motion! Lakini ile spray ingesaidia labda kwa dakika tano tu kama mtu angeingia na baada ya hapo ingeweza kuhisi kuna mabadiliko ya joto.. Kwahiyo kama wote watatu wangeingia maana yake labda kwa dakika moja au mbili za mwanzo isingehisi kitu lakini baada ya hapo ingeling'amua kuwa kuna mabadiliko makubwa ya joto.. Hivyo badi ilikuwa inatakwa mtu mmoja tu aingie na aweze kudisable system nzima ya zile alarm na hapo ndipo ilikuwa zamu ya The monster ambaye alikuwa ni mtaalamu wa umeme na mekanika (mechanics) kufanya miujiza yake..

The monster alitembea hatua kumi na moja mpaka katikati ya vault kama ambavyo alikuwa amefanya mazoezi kwa takribani miezi mitank kwenye replica waliyokuwa nayo nyumbani.. Baada ya kufika katikati ya vault aliinua mikono juu kugisa dari la vault ambalo hapo juu kulikuwa na kiboksi cha umeme ambaco chenyewe ndicho kilikuwa kinakusanya electric pulse kutoka kwenye vifaa vyote vya ulinzi ndani ya vault na kupeleka kwenye system ya alarm.. Yaani kwa mfano kama light sensor ikihisi kuna mwanga kwenye vault basi itatuma electric pulse mpaka kwenye kifaa hiki na chenyewe kitatuma taarifa juu kwenye system ya alarm na alarm italia..

Kwahiyo alichokifanya The monster ni kufungua mfuniko wa kifaa hiki kisha akazichuna plastiki ya juu inayofunika nyaya na hatimae zile nyaya zikawa wazi, kisha akachukua kipande cha nyaya alichokuja nacho na kufunga kwa ustadi kuunganisha nyaya hizo na kutengeneza 'bridge' ya umeme (alikuwa anafanya reroute) naamini watu wa umeme na fizikia watelewa vizuri..
Kwahiyo baada ya kufanya hii reroute ilimaanisha kwamba umeme uliokuwa unatoka kwenye alarm system unaishia hapo kwenye 'bridge' na kurudi nyuma na umeme uliokuwa unatoka kwenye vifaa vya ulinzi ulikuwa hauvuki hiyo bridge!! Kwa kifupi ni kwamba mawasiliano kati ya alarm system na vifaa vya ulinzi yalikuwa hayapo hivyo haikujalisha nini kilikuwa kinatokea ndani ya vault, alarm system isingeweza kudetect..

Baada ya hapo wote wakaingia ndani na kuanza kazi ya kufungua visanduku vidogo vilivyopo ukutani vilivyokuwa na almasi.. Walitumia drill ambayo ilitengenezwa na The king of keys nyumbani.! Kwa kila kisanduku walitumia kama dakika tatu kukidrill mpaka kufunguka hivyo mpaka mida ya saa kumi na moja alfajiri walifanikiwa kufungua visanduku 109 kati ya 120 vilivyopo ndani ya ile vault.. Ili kuogopwa kukutwa na watu maana kitongoji cha Antwerp kuanzia majira ya saa kumi na mbili na nusu mitaa inaanza kufurika watu! Kwahiyo wakajiridhisha kuwa wana mali ya kutosha wakabeba mzigo wao wakatokomea..



#3

WIKI CHACHE BAADE..

Natarbatolo alikamatwa wiki chache baadae kwa kuhusika na tukio hili!
Kukamatwa kwake kulikuwa ni kwa kizembe mno, walitupa taka taka za vifaa vyao vya maandalizi nje kidogo ya mji wa Antwerp na walipuuzia kuzichoma moto wakiamini hakuna mtu atakayeziona.. Katika takataka hizo pia kulikwa na kipande cha Sandwich ambacho Natarbartolo alikibakisha alipokuwa anakula.. Polisi walitumia kipande hicho cha sandwich kupima DNA na kukuta inamatch na DNA ya Natarbartlo..


MAMBO YENYE UTATA MPAKA LEO HII

Kuna vitu kadhaa ambavyo mpaka leo havitapata majibu sahihi..

i) yule myahudi aliyempa dili Notarbartolo ni nani?? Kuna watu wanadai kuwa Natarbartolo anajificha identity ya huyu mtu kwasababu inawezekana ni mpwa wake Benedetto Capizzi ambaye mwaka 2003 aliteuliwa kuwa Capo dei capi, ambacho ni cheo cha juu kabisa katika mtandao wa kihalifu wa Sicilian Mafia..
Natarbartolo anakataa kabisa mpwa wake kuhusika katika tukio hili..

ii) Natarbartolo anadai kuwa wao wenyewe waliingizwa mkenge na yule myahudi kwasababu anahisi kuwa yule myahudi na wenzake walitengeneza insurance scum ili waweze kujipatia fedha kutoka kwenye kampuni ya Bima.
Yaani iko hivi, polisi wanadai kuwa almasi iliyoibiwa zilikuwa na thamani ya dola milioni 100 lakini Natarbartolo anadai kuwa viboksi vingi wakivyovifungua ndani vault vilikuwa havuna kitu kana kwamba watu waliambiws wasiweke alamsi siku hiyo.. Natarbartolo anadai kuwa almasi walizozikuta zilikuwa na thamani isiyozidi dola milioni 20.!! Natarbatolo anahisi kuwa yule myahudi alipanga dili na wenzake wamshawishi aende akaibe lakini siku moja kabla yule myahudi na wenzake wengi wakatoa almasi kwenye vault, kwahiyo baada ya tukio lile la wizi watu wote wenye visanduku kwenye vault wataenda kulipwa na kampuni ya bima lakini huku almasi zao zikiwa ziko nyumbani wamezificha kwani walizitoa siku moja kabla ya tukio! Kwahiyo wanakuwa wamepata hela ya bima na almasi zao wanazo..

iii) Hizi almasi zilizoibiwa hazijapatikana mpaka leo, na hazijulikani ziko wapi licha ya Natarbattolo kukamatwa..


MWISHO


Jiunge na Group langu la Whastapp kusoma makala na simulizi zaidi kila siku – 0718 096 811 (kuna malipo ya 5,000/- kwa mwezi)


Natarbartolo alikamatwa na kushtakiwa kwa wizi huu uliotokea! Kutokana na kukosekana ushahidi wa moja kwa moja (almasi zenyewe) ikabidi mahakama itumie ushahidi wa kimazingira (circumstantial evidence) ili kumtia hatiahani na alihukumiwa miaka kumi jela.. Mpaka hivi tunavyoongea Natarbartolo ameshamaliza kutumikia adhabu yake na yuko uraiani na ameingia mkataba na Paramount Pictures ili kutengeneza filamu kuhusu tukio hili na filamu itatengenezwa na Director nguli J. J. Abrams huyu ndiye aliyetengeneza filamu za Lost (series), Armageddon, Star Trek, Star Wars: Force Awaken pamoja na filamu ya Mission Impossible III



The Bold
 
Back
Top Bottom