Tukio la Morogoro: ITV imeitendea haki CHADEMA, POLISI na Watanzania!

Kama hujui suti ya kuvaa ukiwa TBC, kamuulize Tido Mhando. Ukitaka kudumu ndani ya TBC, basi uwe tayari kuwa kibaraka.
 
Jeshi la Polisi limeendeleza mauaji ya raia wasio na hatia katika kudhibiti ushiriki wa Wananchi kwenye siasa za vyama vingi. Leo tarehe 27/08/2012 Jeshi hilo limemuua raia mmoja kwa kumpiga risasi ya kichwa. CHADEMA walitaka kufanya mkutano tarehe 8 wakazuiwa kwa sababu ya sikukuu ya nane nane, tarehe 26 pia wakaahirisha ili kupisha sensa. Leo tena RPC anaweka vikwazo visivyo na msingi na vya uonevu


Hisani ya chadematv ya youtube
 
Last edited by a moderator:
Nimeipenda sana ITV tena wameonyesha mara tatu kwa heading tofauti lakini zote zikihusu yaliyotokea moro.reporter amekwenda mbali zaidi kwa kusema Cdm walikuwa wakifanya maandamano ya amani.
Hongera sana ITV
 
lkn hawa tbc wanaishi kwa PAYE zetu nawashangaa sana ccm! Ipo siku tutajikomboa kutoka kwa hawa wakoloni weusi
 
ivi ni kipi hasa kinachofanya polisi wa nchi hii kutokutoa kibali cha maandamano ya vyama vingine vya siasa?ivi ccm labda hawajawai kundamana au walishawahi kunyimwa kibali cha maandamano?

kwakweli binafsi hainiingii akilini kila chama mbadala kinanyimwa kibali hiki,au kuna vigezo/masharti maalumu hawatimizi ndo mana wananyimwa?
nimemsikiliza sijui nani yule wa polisi-moro alipoojiwa ktk redio sababu aloitoa nikaishia kufoka kwa hasira sababu ya kipumbavu na uwendawazimu kabisa.....

kweli polisi hatuna magarasa kabisa haya!!
 
Pia ITV wamesema hatimaye polisi walizidiwa nguvu pamoja na kutumia risasi lkn watu walirudi barabarani,vile vile RPC alionekana kuwa mstari wa mbele katika vurugu hizo.

My take:nguvu ya dora haijawahi kushinda nguvu ya uma kote duniani.viva forever
 
Nashukuru kwa kuwa nilishaacha kuangalia taarifa za tbc1 muda sana, yanini kupata presha na taarifa zilizojaa hujuma dhidi ya matarajio wa watazamaji? ndugu zangu tubadilike, kupinga udhalimu achana na tbc, iliwahi kuwa na maana kipindi cha muhando tu baada ya hapo wiiizi mtupu
 
Nashukuru kwa kuwa nilishaacha kuangalia taarifa za tbc1 muda sana, yanini kupata presha na taarifa zilizojaa hujuma dhidi ya matarajio wa watazamaji? ndugu zangu tubadilike, kupinga udhalimu achana na tbc, iliwahi kuwa na maana kipindi cha muhando tu baada ya hapo wiiizi mtupu
TBC ni janga la taifa. Sijui nitumie neno gani kuielezea TBC.
 
nimeona hiyo taarifa utube, iko very elaborative na aliyeuwawa ni muuza magazeti. jk say or do something kuhusu haya mauaji ya raia yanayofanywa na polisi, hata kama wengi hawakupendi lakini jukumu la kutulinda sisi 'wanao' ni lako kwa sasa.. halafu mwisho wa taarifa wamesema eti jeshi la polisi linafanya uchunguzi zaidi... sielewi mwenzeni. hivi mnataka tuelewe kuwa jeahi la polisi halina mbinu za ku manage crisis waliyosababisha wenyewe zaidi ya kuuwa?
 
TBC mbuzi kabisaaaa! yaani hata main news za leo wao hawaoni umuhimu wa kutaja jambo hili la kihuni linalofanywa na serikali.

TBC Uchafu kabisa!!

katika kifupisho cha TBC hebu ondoa ile herufi ya mwisho......umenifahamu eh! unapata TB (=tuberculosis "Kifuakikuu" gonjwa hilo) LAKINI ukichukua ITV ukitoa herufi V unapata IT (= Information and Technology) Umenifahamu hapo!
 
katika kifupisho cha TBC hebu ondoa ile herufi ya mwisho......umenifahamu eh! unapata TB (=tuberculosis) LAKINI ukichukua ITV ukitoa herufi V unapata IT (= Information and Technology) Umenifahamu hapo!

uko fasta!
 
Yani TBC siku hizi limekuwa nilichannel la hovyo sijapata ona.hata kuonyesha hiyo habari kwa kuwapendelea polisi tu wameshindwa?dah!sijuhi ntafanyaje hapa nilipo kesho nisiangalie hii channel takataka kabisa
 
Back
Top Bottom