Tukio la Arusha ni ishara kuwa busara isipotumika Tz amani itakuwa historia

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
10
Ni bahati mbaya sana kuwa viongozi wetu wa jeshi la polisi pengine wakiagizwa na wakuu wa dola wamekuwa na mtazamo finyu na wa kidikteta katika kushughulikia maswala ya usalma wa wananchi inapokuja kwenye maswala ya kisiasa. Hatua ya mkuu wa jeshi hilo kuzuia maandamano halali kwa kisingizio kuwa kungekuwapo uvunjifu wa amani Arusha ni mfano mmoja kati ya mingi.

Kama wananchi wangeachiwa wakaandamana kusingetokea vurugu. Lililo baya zaidi wamewakamata viongozi wa watu wale wale wanaoandamana. Busara ndogo tu inaonesha kuwa kuwakamata viongozi kama hao mbele ya wafuasi wao kungezaa vurugu. Matumizi ya nguvu kubwa kupita kiasi kwa watu wasio na silaha ni uchochezi wa wazi wa vita kati ya polisi na wananchi. Kule Pemba na unguja ndivyo walivyofanya, Dar kadhalika. Mbona hawajifunzi?

Ni muhimu viongozi wafahamu kuwa vurugu inapotokea wa kuwajibika ni wao sio wananchi. Ni wao wameshindwa jukumu lao la msingi la kutunza amani ya nchi. Hivyo ni vyema viongozi muwajibike na kuanza kutumia busara badala ya maguvu. Badala ya kuwakamata viongozi wa siasa kaeni nao mzungumze, mfikie muafaka kwa maendeleo na utulivu wa watanzania wote. Siasa sio fujo, wala ubabe. Msipoyaangalia haya, hali ya Arusha itatawala nchi nzima. Dawa sio kuzuia maandamano na kuua watu, NI MAZUNGUMZO.
 
Back
Top Bottom