Tukio jingine lililonigusa sana week hii...

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Wapendwa wana jamvi la MMU,

Siku ya J3, nilisema kuwa kuna matukio 2 niliyokutana nayo week hii ambayo kwa kweli yamenigusa sana. Tukio la kwanza ni hadithi ya yule bibi kizee wa miaka zaidi ya 100 ambaye alibakwa kwa zaidi ya masaa 8 na bado mbakaji anadunda mtaani.

https://www.jamiiforums.com/mahusia...-miaka-100-abakwa-kwa-zaidi-ya-masaa-8-a.html

Tukio la pili ni story ya kweli ambayo niliisikia kupitia Clouds radio katika kipindi cha michezo siku ya J2. Kuna kijana (22 yrs old) mcheza football ambaye bahati mabaya sikuweza kupata vizuri jina lake, alieleza jinsi aliavyotapeliwa na mapromota wa mpira wa miguu. Alichukuliwa na mawakala matapeli kutoka ZNZ kwa ajili ya kwenda kumtafutia timu SA. Badala yake walimpeleka Comoro na Libya na kisha kumlazimisha afanye kazi ya kusafirisha unga (dawa za kulevya) kwa malipo ya Tshs 140mil! Kijana aligoma kufanya hiyo kazi na baada ya hapo passport yake na hati nyingine za kuwepo Libya walivichoma moto na huyo kijana kufungwa jela miezi 6 (sikumbuki vizuri kama siyo miezi 4). Walimwachia passport ya Burundi ambapo alirejeshwa baada ya kumaliza kifungo. Story ni ndefu ila kijana tayari karudi Bongo na hakuna hatua ambazo zimechukuliwa dhidi ya hao wahalifu!!

Nilisikitishwa sana na hiyo hadithi na especially aliposema kuwa watu hao walimweleza mambo mengi ikiwemo ushiriki wa watu wazito katika biashara hiyo chafu!!
 
Ndo bongo mkuu! ukishangaa unalizwa mchana kweupe

Kuibiwa ni tatizo ila linakuwa tatizo kubwa kama linawahusisha na wakubwa ambao ndio wanaotakiwa kutupatia ulinzi na usalama wa mali zetu na maisha yetu!

Ni sawa na kuwauza watoto wako mwenyewe..Sasa tukimbilie wapi??
 
Hao ni wachache katika ya wengi ambao ukisikiliza stori zao ni huzuni tu kuna wale wanaotoka hapa wakiambiwa kuwa wamepatiwa ajira nzuri huko nchi za watu wakifika huko wanakuwa house girls na house boys, kufanyishwa kazi bila malipo, kufanyishwa biashara ya ukahaba na mengineyo mengi tu
 
Bora alikataa kuliko angekubali either akafa nayo tumboni or akaishia kukamatwa na kula mvua nyingi zaidi. Babu DC, inahuzunisha, lakini hakuna ushahidi wa kutosha kwa sababu walimtelekeza. Alipaswa awaripoti kule kule wakamatwe tena kwa human trafficking na sio madawa kwani ushahidi haukuwepo. Mi simuamini mtanzania yeyote!kha!
 
Utu wake na uaminifu wake ktk maamuz yake umenipa moyo sana. Suala ka kukataa kuuza madawa ya kulevya na kujikuta katupwa jela mi naona ni kitendo cha kishujaa kabisa ambacho kila mwanamapinduzi au mzalendo yeyote anatakiwa kuwa hivi.
Kama tungebahatika kuwa na viongozi wa ngazi za juu wenye UTU kama huyu kijana, neno UFISADi tusingelisikia kamwe na TZ ingekuwa kama SA kwa maendeleo.
Mungu awabariki wenye mioyo kama hii, loooh.
 
Kweli hayo tanafanyika sana TF, tatizo langu ni pale ambapo viongozi wa ngazi za juu katika chama cha soka na labda wengine kutoka serikalini wanakuwa key players katika huu uozo!
 
Bora alikataa kuliko angekubali either akafa nayo tumboni or akaishia kukamatwa na kula mvua nyingi zaidi. Babu DC, inahuzunisha, lakini hakuna ushahidi wa kutosha kwa sababu walimtelekeza. Alipaswa awaripoti kule kule wakamatwe tena kwa human trafficking na sio madawa kwani ushahidi haukuwepo. Mi simuamini mtanzania yeyote!kha!

Kwa nini hutuamini? Tumekufanyia au tumekufanya nini??
 
Utu wake na uaminifu wake ktk maamuz yake umenipa moyo sana. Suala ka kukataa kuuza madawa ya kulevya na kujikuta katupwa jela mi naona ni kitendo cha kishujaa kabisa ambacho kila mwanamapinduzi au mzalendo yeyote anatakiwa kuwa hivi.
Kama tungebahatika kuwa na viongozi wa ngazi za juu wenye UTU kama huyu kijana, neno UFISADi tusingelisikia kamwe na TZ ingekuwa kama SA kwa maendeleo.
Mungu awabariki wenye mioyo kama hii, loooh.

Hata mie nilifurahi sana kwamba kijana alitia msimamo hadi dakika ya mwisho...Ni ushujaa wa aina yake!

Ila sasa hao watu wazito wanaonyemelea wototo na wajukuu zetu kwa nini wanaachwa waendelee kutanua mitaani?
 
Uczoee kila m2 bila kuwa na logic ya mana.ashukuru Mungu ake sana mana cku hz angefanyiwa hata ukamerun,bila kubisha wala maelezo.
 
Uczoee kila m2 bila kuwa na logic ya mana.ashukuru Mungu ake sana mana cku hz angefanyiwa hata ukamerun,bila kubisha wala maelezo.

Mbona sijakuelewa ndugu yangu.

Kama mtu una bidhaa sokoni, utajuaje yupi ni mteja wa kweli na yupi anakuzuga?
 
Back
Top Bottom