Tukikuze kiswahili

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,835
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 29, ninaipenda sana nchi yangu na vitu vake vilivyomo. Ninajisifu kwa kuwa na nchi yenye lugha yake yenyewe tofauti na nchi zingine zilizo kubali kurith lugha za kikoloni.

KISWAHILI KINA SEHEMU GANI KWA MTANZANIA

Pomoja na kwamba watanzania wengi hawapendi lugha yao ya kiswahili, mimi nimejikuta nikipenda lugha yangu ya Taifa. Ni kutokana na sababu zifuatazo.

1. Nchi nyingi za kiafrika zime rithi lugha za kikoloni, na kama hiyo haitoshi zimekuwa na lugha zaidi ya moja. Lakini nchi yetu ya Tanzania pekee hapa Africa imakuwa na lugha yake yenyewe. Ukiangalia nchi nyingi za africa zimekuwa zikisifu lugha za kikoloni, hii inamaanisha kuwa nchi hizo zimetawaliwa bado katika mambo ya kiutamaduni hususani katika mambo ya lugha.

2. Kiswahili ni lugha yenye sifa kuliko lugha zingine za kiafrica. Hii ni kutoakana na kwamba kiswahili ni lugha rahisi kujifunza mtu yeyote anaweza akajifunza na kuelewa kwa mda mfupi. pili lugha ya kiswahili ni lugha pekee inayo weza kubeba jukumu la misamiati ya kisayansi tofauti na lugha zote za kiafrica.

3. Vilevile lugha ya kiswahili inaweza kutamkika pasipo kuwa mawimbi ya neno, yaani sauti ya moja kwa moja.

4. Tukiangalia katika nchi nyingi za kiafrica kumekuwa na kutoelewana baina ya makabila hii ni kutokana na kwamba wamekuwa na lugha mchanganyiko na kila mmoja anataka lugha yake iwe ya taifa. sasa imesababisha tofauti katika jamii hizo.

5. Kiswahili kimetuunganisha kama ndugu wa mzazi mmoja, ni sifa kubwa kwa wa tanzania japo wanaona kama vibaya.

6. Kiswahili kinasehemu kubwa sana hapa afrika kupitishwa kuwa lugha ya nchi mbali mbali, moja wapo Nigeria.

7. Kiswahili ni moja ya lugha za umoja wa africa.

8. Wageni kutoka nje kama uingereza, marekani, china na kwingineko wanatamani sana kujua kiswahili





MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom