Tujuzeni matokeo : Cameroon vs manyara stars....mliopo uwanjani

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
...WanaJF tupeni updates za game la Cameroon na Manyara Stars... wengine presha inapanda na kushuka....
 
Jeshi la Julio laivaa Cameroon Send to a friend Saturday, 09 April 2011 09:56 0diggsdigg

jeshjulio.jpg
Mshambuliaji wa timu ya taifa U/23 Mrisho Ngasa akipita katikati ya mabeki wa timu hiyo wakati wa mazoezi jana jioni kwenye Uwanja ea Karume jijini Dar es salaam

Sosthenes Nyoni
TIMU ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 23, leo inatarajia kushusha ama kupandisha presha za Watanzania pale itakapovaana na Cameroon katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Olimpiki utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kushusha ama kupanda kwa presha za Watanzania kutategemeana na matokeo ya mchezo huo yatakayoamua timu hiyo kusonga mbele au kubaki.

Tanzania inashuka dimbani ikiwa na deni la bao moja tu baada ya ule wa awali ulifanyika nchini Cameroon kukubali kipigo cha mabao 2-1kutoka kwa wenyeji.

Tayari kocha Jamhuri Kihwelo'Julio' ameongeza baadhi ya wachezaji katika kikosi chake kitakachoikabili Camoroon leo akiwemo nyota wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mrisho Ngassa akisaidiana na washambuliaji chipukizi wenye kasi Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu.

Hata hivyo vijana hao watamkosa nahodha wake Salum Telela aliyeonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa awali na tayari nafasi yake amepewa kipa Shaaban Kado akisaidiwa na Himid Mao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Julio alisema kuwa watalazimika kupigana kufa au kupona ili waweze kushinda mpambano huo huku akiwataka wachezaji wake wacheze kwa tahadhari.

"Tuna bao moja la ugenini, lakini hii haitoshi na kujiona tumeshinda kwa vile tunacheza nyumbani, zinahitajika jitihada za dhati ili tuwewe kupata mabao ikiwezekana mengi,"alisema Julio.

Kwa upande wa Ngasa mwenye thamani ya Sh 54m, alisema atajituma kwa uwezo wake wote kwa kushirikiana na wachezaji wenzake ili waweze kushinda mchezo huo dhidi ya Cameroon.

"Nipo hakuhakikisha tunaipeperusha vema bendera yetu, ni matumaini yangu kwa kushirikia wote na mashabiki wetu basi tutashinda na kusonga mbele."Naye kocha wa Cameroon, Dieudonne Nke alisema kuwa wamejiandaa vya kutosha kwaajili ya kukabiliana na wapinzania wao.

"Tuko vizuri sasa, hali ya hewa ya hapa haitusumbui kwasababu inafanana na ya kule kwetu hivyo kilichobaki ni kupigana uwanjani tu na nina hakika tutashinda,"alisema Nke.
 
Tunawashambulia sana Cameroon tatizo ni umliziaji tu.....Pia mabeki wamefanya uzembe wa hali ya juu sana kuruhusu goli hili moja.....

Mrisho Ngasa hayupo hata kwenye subs(safi sana hii,naona TFF wamestuka)
 
Tunawashambulia sana Cameroon tatizo ni umliziaji tu.....Pia mabeki wamefanya uzembe wa hali ya juu sana kuruhusu goli hili moja.....

Mrisho Ngasa hayupo hata kwenye subs(safi sana hii,naona TFF wamestuka)

natumai tutashinda , naomba gundu lisiwepo ili haya mashambulizi yazae matunda
 
Half time score 1-1, umaliziaji bado ni issue, samatta na ulimwengu wanapoteza nafasi kibao za wanahitaji kutulia 2nd hafu, kwenye kiungo kigi makassy na abubakari salumu 'sure boy' bado hawajakaa vizuri. HIVI BAADA YA MECHI YA LEO TUKISHINDA NDIO TUMEFUZU AU BADO MECHI NGAPI?
 
tafadhali naomba kujuwa wafungaji(mfungaji wa goli la manyara)na lango kasimama nani?
 
Half time score 1-1, umaliziaji bado ni issue, samatta na ulimwengu wanapoteza nafasi kibao za wanahitaji kutulia 2nd hafu, kwenye kiungo kigi makassy na abubakari salumu 'sure boy' bado hawajakaa vizuri. HIVI BAADA YA MECHI YA LEO TUKISHINDA NDIO TUMEFUZU AU BADO MECHI NGAPI?

bado kuna raundi ya pili,vp maudhulio?
 
Nani alitangulia kufunga? na mfungaji wa Manyara Stars ni nani? Na mazingira ya goli ilikuwa vipi? Ni penati, kona, shuti au....?
 
Back
Top Bottom