Elections 2010 Tujiweke karibu na Mungu ili atupatie yaliyofichika katika akili zatu za kibinadamu!

rubymbuya

New Member
Sep 14, 2010
1
0
Hivi umewahi kujiuliza ni kwa sababu gani nchi ya Tanzania inazidi kudoroda katika nyanja zote za kijamii-kimaadili, kiuchumi, kiteknolojia, n.k?

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tutambue kuwa kila jambo linalotendeka katika ulimwengu huu, lina mahusianoa makubwa na ya moja kwa moja na ulimwengu wa kiroho. Hivyo basi, tutafute hayo yaliyofichika na kupumbaza ufahamu wetu kushindwa kujitambua na hali ya umasikini unaotawala nchi hii ya Tanzania ambayo Mungu ameijalia kuwa na maliasili pekee na kwa wingi karibu ka siyo zaidi ya mataifa mengi makubwa.

Tujiulize, ni kwa nini tumekuwa madaraja wa mataifa makubwa kutajirikia katika ardhi yetu huku wakiwezeshwa na baadhi ya Watanzania wenzetu?

Ni wakati muafaka sasa kujitafakari na kubadilika kiroho kwanza.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom