Tujiunge na kuanzisha JAMII FARM

Mkuu Malila na wengineo mlioamua kuwa pamoja ktk project hii, kwanza niwape pongezi zenu for daring to act!
pili, naomba kujiunga na kundi hili ktk project hii.
Nipeni taratibu za kufuata.

Asante
 
Hongereni nyote mliothubutu kuanzisha na iwe mfano wa kuigwa mkivuna msiache kutuhabarisha nasisi tule vya nyumbani ..natamani ningekuwepo toka mnaanzisha ilo wazo..keep it up

Naomba nipokee hongera yako kwa niaba ya wenzangu, tutarudisha matokeo hapa jamvini muda si mrefu.
 
lolyz upo dada yangu!!
mambo ya Jamii farm ni bam bam, watu wanapanda miti kama hawana akili nzuri!1
 
Mgombezi uko wapi,

Jamii farm tayari imeshaanza.


Nimeangalia thread za miaka ya nyuma na kugundua kuwa wazo la Jamii Farms lililetwa Jukwaani na Ntareyehirungu June 2, 2010 saa 1450.

Kwa miaka ambayo nimekuwepo hapa JF kama mwanachama, nimeelimika vilivyo, nimeburudika kiasi cha kutosha, nimefarijika na kufaidika na mengi kwa ujumla. Moyo wangu daima unajihisi kukosa fadhira kama sishirikishi au kurejesha hata sememu ya faida hizi kwa wengine au jamii.

Ni usemi wa siku nyingi kuwa "Ndege wenye mabawa yanayofanana.........." na hivyo basi wakati wote mimi huamini kuwa kujificha nyuma ya kompyuta na kuemdeleza matumizi ya majina bandia katika kuchangia mada makini humu ndani kunatakiwa kuwa na kikomo. Nikiazima kaulimbiu ya Invisible "Ficha Upumbavu, Usifiche Hekima" nadhani huu utaratibu wa kujificha inabidi tuuvunje kwa wanachama wenye mawazo sawa, mtazamo unaofanana na kuwajibika kunakoshabihiana kukutana wazi tukiwa na dhamira moja tu; Kuhalisia Fikra Zetu. Nimesoma mahali kuwa baadhi yetu wamewahi/hukutana.
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/39210-project-funding-sources-5.html#post927666 Ni jambo jema na si vibaya wengi zaidi tukajulishwa ni jinsi gani ya kuungana nao.


Najua JF kuna majukwaa mengi. Na watu wanavivutio, hisia, mitazamo na malengo tofauti kulingana na majukwaa wanayopendelea. Binafsi, mie mtoa wito ni mpenzi wa Jukwaa la Biashara na Uchumi. Na wito wangu nautoa kwa Wadau wa Jukwaa la Biashara na Uchumi kukutana na kutengeneza Mpango stahimilivu utakaowezesha kuhalisia mawazo na mitazamo yetu.

Kuna hazina kubwa juu ya Mustakabali wa Biashara na Uchumi imehifadhiwa hapa JF. Rasilimali-Watu na taarifa zilizomo humu ndani juu ya Kilimo, Ufugaji na Biashara kwa ujumla ni LULU huwezi pata bure kokote ufikiliapo. Nimejaribu kujikumbusha nyuzi na michango LULU kama:

https://www.jamiiforums.com/busines...kwa-wanaopenda-ufugaji-mkubwa.html#post908785
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/52203-sirudi-nyuma-3.html#post896885
https://www.jamiiforums.com/busines...biashara-ya-mboga-mboga-ulaya.html#post934969
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/50511-bwawa-la-samaki-2.html#post936693
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/60458-kilimo-cha-milonge.html#post936948
https://www.jamiiforums.com/busines...62-kilimo-cha-mitiki-utaalamu.html#post937049
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-tanzania-ni-nchi-maskini-19.html#post888920
https://www.jamiiforums.com/busines...ieni-5mil-kuanzia-biashara-10.html#post877391
https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/35182-mbuzi-wa-maziwa.html#post565339
https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/33587-nauza-rozera.html#post518819
https://www.jamiiforums.com/busines...isha-biashara-itakayofanikiwa.html#post509060

Shime: Natuone thamani iliyomo katika maandishi haya. Tujithanini kwa kutoa hii michango yenye thamani namna hii. Natujiweke tofauti na Walivyozoeleleka Watanzania: Wajuvi wa kueleza matatizo na kutoa masuluhisho kwa maneno bila vitendo. Na kisha tujipange kukutana kuuunganisha haya mawazo na kujenga umoja/chombo kitakachotoa nafasi kwetu sisi kuyafikia malengo. Chombo hicho yaweza kuwa Kampuni

Naomba kuwakilisha

Entare Yehirungu
Kasindaga.

E-mail: kageratea@gmail.com
Mob: 0762-444-266
 
hahahahah kaazi kweli kweli panapokuwa hamna hot event wanaJF hujiburudisha
 
Nimeangalia thread za miaka ya nyuma na kugundua kuwa wazo la Jamii Farms lililetwa Jukwaani na Ntareyehirungu June 2, 2010 saa 1450.

Kweli mkuu,
Sijui kama jamaa anajua kuwa mchango wake ulizaa matunda na vijukuu? Mambo yanaendelea.
 
Back
Top Bottom