Tujiunge na kuanzisha JAMII FARM

Naomba tuwasiliane mie ni mtaalamu wa kilimo hili linawezekana kabisa na hasa sasa pamba inalipa mbaya

Tunawahitaji sana wataalamu wa Kilimo katika wakati huu, tunategemea ushiriki na mchango wako.
 
ndugu wanajamii tukubaliane lini tutakuwa na muda wa kufanya mkutano huo ,. then kila mtu aandae elfu kama elfu kumi mpaka 15 kwa ajiili ya gharama za ukumbi (inaweza kupungua au kuongezeka kutegemeana na idadi ya watu).. ukumbi upatikana tu.

Napendekeza tarehe 30 January 2011, vipi wadau mnasemaje. Kanyagio tusaidie kutoa pendekezo la ukumbi mmojawapo na gharama zake ili tuwe na hakika ya gharama. Halafu hiyo 10 - 15 elfu itakuwa ni gharama ya ukumbi tu au ita-include some drinks or anything.
 
Jumapili watu wengi wanakuwa na vikao vya kifamilia na harusi, hatuwezi kufanya Jmosi 29th or 26th sababu ni public holiday
 
Jumapili watu wengi wanakuwa na vikao vya kifamilia na harusi, hatuwezi kufanya Jmosi 29th or 26th sababu ni public holiday

Mkuu Elnino; Ni kweli katika miji mikubwa kama Dar unaweza kujikuta kila Jumapili unahitajika kushiriki kikao cha harusi ya jamaa wa karibu. Tunaweza kukutana 29 Jan 11; hii inaweza kuwa njema zaidi kwa wale watakaotoka nje ya Dar kurejea makwao Jumapili.

Mkuu Kanyagio; unaweza kuangalia ukumbi kwa siku hiyo.

Nawasilisha!
 
Nimependa hii idea, naomba nijulishwe nami nihudhurie tafadhali
 
sawa Mgombezi nitafuatilia,.. kwa sasa nipo nje ya Dar.. nitatoa feedback nikirudi Dar
 
kwa tarehe hizo mimi nitaukosa mkutano wa kwanza. Narudi dar 1february. Nitapata feedback toka kwa kanyagio. Ikikubalika tarehe hiyo basi mkutano ufanyike
 
kwa tarehe hizo mimi nitaukosa mkutano wa kwanza. Narudi dar 1february. Nitapata feedback toka kwa kanyagio. Ikikubalika tarehe hiyo basi mkutano ufanyike

Mkuu Malila;
Nafikiri wadau wengi wangependekeza uwepo wako kutokana na michango yako, ngoja tuwasikilize wadau wengine.
 
WaKUU nashauri kikao Kihairishwe Mpaka baada ya 1February mpaka Mkuu Malila awepo,na atuhakikishie kuwepo,Michango yake ktk hii secta hana mpinzania na ameonyesha a true spirit of the INTERNET.to help and share knowledge freely .
Malila sasa tueleze convenient time and date .
 
Asante,

Mimi nitakuwepo dar kuanzia 1february mpaka 28february. Kwa hiyo siku zote za hapa ktkt nipo huru kabisa kushiriki kikao chetu. Naomba tuchague tarehe ili mimi niingize tarehe hiyo ktk ratiba zangu. Nina kazi ya kuhakikisha miche milioni moja ya miche ya pines/mlingoti inapandwa ktk mashamba ya wadau wenzangu huko Iringa ktk kipindi hicho. Sitawaangusha wakuu. Na mimi pia sipendi kuwaangusha wadau wangu wa misitu huko shamba Iringa.
 
Jumamosi ya 5february tukutane pale Lunch Time Hotel, opposite na Mabibo Hostel Mandela Road, saa kumi na mbili jioni baada ya kazi za mchana kutwa. Pale pana kumbi zaidi ya moja, pana Parking ya kutosha yenye ulinzi mzuri, pana nyama choma kwa watumiaji na rahisi kuingia na kutoka kwa wenye magari na waendao kwa miguu.
 
wakuu.. mimi nakubaliana na Malila kwa tarehe 5 February 2011 ila naomba sana sana tena sana tusianze saa 12 bali tuanze saa 10 juu ya alama . one of the proposal ni kufanyia kikao chetu pale Luch time. napendekeza tufanye yafuatayo.

  • nitaanzisha thread mpya kwa ajili ya maandalizi (nitaiita CHAI Day: Kujadili fursa katika Kilimo 5 Feb 2011 Dar)
  • nitashirikiana na Malila na Mgombezi katika kufanya maandalizi hasa kufinalize ukumbi pamoja na gharama (one option ni Lunch Time, kama kutakuwa na option nyingine nitawaambia). Aidha tutashirikiana katika kutengeneza ajenda
  • Tuhamasishe watu walio serious wa-attend!
  • nitapitia threads zote zinazohusu kilimo ili kubainisha
pamoja na kuwa na wajumbe wa JF napendekeza tuite na watu ambao ni serious katika kilimo. Je mnapendekeza tukaribishe Tanzania Investment Bank (TIB) na Benki ya wanawake ambao nasikia wanatoa mikopo ya kilimo?
 
Ngoja tuone majibu ya wenzetu, kama tutakuwa chini ya washiriki kumi hakuna haja ya ukumbi,ili kupata idadi tarajiwa ni vizuri kwa kupitia hiyo thread mpya watu tujiorodheshe. Lingine ni kwamba, ni mapema mno kuwaalika jamaa zetu wa TIB au wadau wengine kwa sababu, sisi hatuna formal leadership wala jina hatuna na bado misheni/visheni havijawekwa bayana,tunaweza tukawatumia vibaya na ule muda mwafaka wa kuwahitaji wakatuocha hewani kutokana na picha ya nyuma.

Tukutane kwanza,tuweke mambo vizuri na kutengeneza skeleton ya utekelezaji,naamini itafika stage ambayo tutawahitaji tu. Kwa historia tu hata huyo Lunch time mwenyewe tukimwalika ili atuambie kwa nini aliita hotel yake jina hilo na alikotokea,litakuwa somo tosha kwetu.
 
Malila ahsante kwa maoni. nakubaliana na wazo lako la kukutana kwanza sisi kwa sisi kabla ya kualika banks!!. Aidha kikubwa kwa sasa itakuwa ni kupata washiriki wa mkutano. kwa upande wangu sina wasiwasi na idadi ya watu, hata tukikutana watu 10 tunaweza kutoka na kitu cha maana sana kutegemeana na aina ya watu watakaokuwepo na mawazo yatakayotoka!!.

Aidha, nakubaliana na wewe kuwa kama idadi itakuwa ndogo tusikodishe ukumbi bali tutafute sehemu iliyotulia ambayo ni free of charge (mradi unatumia vinywaji vya hapo sehemu) au ambayo wanatoza fee kidogo. sitapendelea waandaaji waingize mfukoni mwao kugharimia mkutano huu (apart from fedha watakayotoa kama washiriki wengine).
 
Asante KANYAGIO na MALILA,

Nilipita kwenye ile thread mpya ya CHAI DAY kabla ya kupita hapa, nakubaliana sasa na wazo la mkuu MALILA kwamba tukutane kwanza sisi wenyewe halafu tutaweza kufahamu uhitaji wetu na kujua tunamhitaji nani wakati mwingine.
 
Mambo yamezaa mambo, thread hii ilipelekea kuzaliwa kwa thread ndogo ya chai day, ambayo nayo ikazaa thread ndogo nyingine na hiyo ndogo nayo imezaa ndogo zaidi kwa maana kwamba sasa tuko ktk utekelezaji.

Ninachotaka kusema hapa, ni kwamba jamii farm ilikubalika,inawezekana wadau wengine wasijue nini kiliendelea baada ya pale, kwa ufupi mambo yanaendelea kimya kimya.
 
Mimi nipo tayari kwa masharti kwamba sehemu litakapoanzishwa Shamba lazima pawe na maji ya uhakika (Mto) ili tutumie kilimo cha umwagiliaji, sitaki kusikia eti Mvua haijanyesha ndio maana tumekosa mazao
 
Maji ya mto usiokauka ni lazima,kinyume na hivyo tunadanganyana. Kipande cha Ikwiriri/Rufiji kinaonekana kimejaa sana, najaribu kuangalia kipande cha Moro upande wa bonde la Kilombero, Dakawa kumejaa na bei ziko juu kidogo. Tunataka eneo kubwa kabisa,sio kidogo.
 
Back
Top Bottom