tujikumbushie orodha ya mafisadi ya mwaka 2007 iliyotajwa na shujaa Slaa

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
Orodha ya Mafisadi (List of Shame)
KANUNI/ VIGEZO VILIVYOTUMIKA

A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi
ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na
umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI
Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma
wamefanya maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/
au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba
mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na
jamii ya Watanzania.

MISINGI YA KISHERIA/KISIASA YA ORODHA YA MAFISADI
A. KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sura ya 2 ya Sheria za Tanzania imeweka ‘Malengo Muhimu na
Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali’ kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:[1]
a. Kwamba “wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka
kwa wananchi….”;
b. Kwamba “lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi”; na
c. Kwamba “Serikali itawajibika kwa wananchi….”
d. ….”
Katika kutekeleza malengo na misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali iliyotajwa, “… Mamlaka ya Nchi na vyombo
vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
a. …
b. Kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
c. Kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba wa Taifa unaendelezwa,
unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu
mwingine;
d. Kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
a. …
b. …
c. …
d. Kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
e. Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa
kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;
f. Kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za
uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
g. ….” [2]
Ibara ya 7(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeamuru kuwa “… Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote na
mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki,
watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii …” ya Katiba.
Katiba pia imewapa viongozi wa umma “… wajibu wa kufuata na kuitii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya
Muungano.”[3] Aidha, viongozi wa umma wamepewa “… wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya
Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi….”[4] Vile vile viongozi wote wa umma
“watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi nay a pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na
ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa
lao.”[5]
Licha ya masharti ya kikatiba yaliyotajwa hapo juu, viongozi wa umma waliotajwa katika Orodha hii ya Mafisadi
walikuwa wanabanwa na masharti ya sheria nyingine za nchi yetu kama ifuatavyo:

B. SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA, 1995
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga
maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani
ya Serikali na katika sekta ya umma. Katika kutekeleza wajibu wake, Rais anatakiwa kuweka taratibu thabiti za maadili
katika utumishi wa umma ambazo:
a. Zitahakikisha kwamba kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na
wajibu wake kama kiongozi wa umma;
b. …
c. Zitaweka taratibu za wazi za maadili kuhusu migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wa kuchaguliwa na
wa kuteuliwa;
d. Zitapunguza uwezekano wa migongano inayotokana na maslahi binafsi kuingiliana na shughuli za umma za
viongozi wa umma na kuweka taratibu za utatuzi wa migongano hiyo inapotokea.
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa
umma:
a.
kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na
watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa
Serikali;
b. kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na
kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na
haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu;
c. kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa
maslahi ya umma;
d. kuhusiana na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa
na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya;
e. kuhusiana na maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma watapanga masuala
yao kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale
ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia
zaidi maslahi ya umma;
f. kuhusiana na zawadi, viongozi wa umma hawatadai au kupokea manufaa ya kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo
ndogo, ukarimu wa jadi/takrima au manufaa mengine yenye thamani ishara, isipokuwa tu kama manufaa hayo
yatatokana na mkataba au mali ya kiongozi wa umma;
g. kuhusiana na upendeleo, viongozi wa umma hawatatumia vyeo vyao rasmi katika kusaidia taasisi au watu
binafsi katika mahusiano yao na serikali iwapo kufanya hivyo kutasababisha upendeleo kwa mtu yeyote;
h. …
i. Kuhusiana na mali ya serikali ambayo viongozi wa umma hawatatumia ama moja kwa moja ama kisiri siri, au
kuruhusu kutumiwa kwa mali ya serikali ya aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mali ya serikali iliyokodishwa kwa
ajili ya kumnufaisha kiongozi wa umma;
j. Kuhusiana na ajira baada ya utumishi wa umma, viongozi wa umma hawatafanya vitendo vitakavyoshusha
hadhi na heshima ya utumishi wa umma baada ya kuondoka katika utumishi ili kupunguza uwezekano wa
matarajio ya ajira kuleta migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wanapokuwa katika utumishi wa
umma; kupata upendeleo baada ya kuondoka katika utumishi wa umma; kutumia taarifa zinazopatikana
kutokana na utumishi wa umma kwa maslahi binafsi; na kutumia utumishi wa umma kwa ajili ya kupatia nafasi
za ajira nje ya utumishi wa umma.

VIONGOZI WA UMMA WALIOKO KATIKA ORODHA HII WAMEKIUKA NA/AU KUVUNJA MASHARTI YA

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO
A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

1. DR. DAUDI T.S. BALALI
Dr. Daudi Balali amekuwa na bado ni
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
tangu mwaka 1997. Katika kipindi
hicho cha miaka kumi, Gavana Balali
amehujumu taifa la Tanzania kama
ifuatavyo:
i. Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali,
ameruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufikia
Shilingi 522, 459, 255,000 katika ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyoko barabara
ya Mirambo, Dar es Salaam na Gulioni, Zanzibar. Aidha taarifa kutoka vyanzo vingine zinaonyesha
kwamba mwaka 1998 kampuni ya Skanska Jensen ya Sweden ilituhumiwa kutoa hongo ya Dola za
Marekani milioni 5 kwa Gavana Balali tuhuma zilizopelekea kampuni hiyo kupigwa marufuku
kushiriki tenda ya ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, katika mazingira yanayoashiria ufisadi
mkubwa, kampuni ya Group 5 ya Afrika ya Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Skanska Jensen
ilipewa tenda ya kujenga majengo hayo ya Benki Kuu;
ii. Kufuatana na barua iliyotajwa katika aya ya (i) hapo juu, Gavana Balali aliidhinisha na/au kuruhusu
na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 118,396,460.36 zilizopelekwa katika akaunti
isiyojulikana ya Benki ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini kama malipo ya madeni ya kampuni muflisi
ya Meremeta Ltd. iliyokuwa inachimba dhahabu katika eneo la Buhemba wilaya ya Musoma, Mkoa
wa Mara. Kwa miaka mingi Serikali ilikuwa ikitoa taarifa za uongo kwamba Meremeta Ltd. ilikuwa
ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili
ya mradi wake wa Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Hata hivyo, nakala ya usajili iliyotolewa na
Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales inaonyesha kwamba kampuni hiyo iliandikishwa
nchini Uingereza tarehe 19 Agosti 1997 na ilifilisiwa huko huko Uingereza tarehe 10 Januari 2006.
Aidha, taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya tarehe 31 Mei 2005
inaonyesha kwamba Meremeta Ltd. ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania kama tawi
tarehe 3 Oktoba, 1997. Vile vile taarifa hiyo inaonyesha kwamba hisa 50 za Meremeta Ltd.
zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini na hisa 50 zilizobaki
zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa kupitia kwa Msajili wa Hazina katika Wizara ya
Fedha. Inajulikana vile vile kwamba Gavana Balali aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Meremeta Ltd. kati ya mwaka 2004 na 2005. Hata hivyo, kuna utata mkubwa juu
ya nani ni mmiliki hasa wa Meremeta Ltd. kwa kuwa taarifa ya BRELA inaonyesha pia kwamba
makampuni mawili ya Kiingereza – London Law Services Ltd. na London Law Secretarial Ltd. – nayo
yanamiliki hisa moja moja za Meremeta Ltd. Makampuni hayo yanatumia anwani moja iliyoko 84
Temple Chambers, Temple Avenue, jijini London. Haijulikani ni kwanini Gavana Balali aliruhusu
fedha za umma kutumika kulipia madeni yote ya kampuni ambayo Serikali ilikuwa inamiliki hisa 50
tu wakati makampuni mengine ya kigeni yalikuwa yanamiliki hisa 52. Na kama ilivyosema barua ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, uhalali wa Serikali kulipa madeni ya Meremeta Ltd. kwa Nedbank Ltd.
badala ya kuiacha benki hiyo kudai malipo hayo kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na
wadeni wengine haujulikani;
iii.
Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu, Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au
kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kampuni ya Tangold Ltd. Katika hotuba yake
Bungeni ya tarehe 27 Juni 2007, Waziri wa Madini na Nishati Mheshimiwa Nazir Karamagi alidai kwamba
“… mali na madeni ya MEREMETA yamehamishiwa kwenye kampuni mpya ya TANGOLD ambayo
inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.” Hata hivyo, barua ya BRELA ya tarehe 4 Julai 2007
inatamka wazi kwamba “Tangold Limited ni kampuni ya kigeni iliyosajiliwa kwa mara ya kwanza nchini
Jamhuri ya Mauritius, na baadae kuandikishwa nchini Tanzania kama tawi la kampuni ya kigeni.” Barua
hiyo inaongeza kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania mnamo tarehe 20
Februari 2006 na kwamba Katiba ya kampuni hiyo haikuonyesha “majina ya wanahisa wa kampuni na
mgawanyo wa hisa.” Barua hiyo ya BRELA inaonyesha kwamba wakurugenzi wa Tangold Limited ni pamoja
na Gavana Balali, Gray S. Mgonja ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Andrew J. Chenge ambaye ni
Waziri wa sasa wa Miundo Mbinu, Patrick W.R. Rutabanzibwa ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Vincent F. Mrisho ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha fomu Na. 1F inayohusu usajili wa
kampuni za kigeni iliyowasilishwa BRELA na mawakili wa Tangold Limited na kusainiwa na Gavana Balali
tarehe 20 Mei 2005 inaonyesha kwamba kampuni hii imetokea “Jamhuri ya Mauritius” na anwani yake iko
Suite 520, Barkly Wharf, Le Caudan, Waterfront, Port Louis, Mauritius. Hivyo ndivyo kinavyoonyesha cheti
cha usajili kilichotolewa na Msajili wa Makampuni wa Jamhuri ya Mauritius mnamo tarehe 5 Aprili 2005 na
pia leseni ya biashara iliyotolewa kwa Tangold Ltd. Port Louis nchini Mauritius tarehe 8 Aprili 2005.
nyaraka hizi pia zinaonyesha kwamba Tangold Limited ni kampuni binafsi (private company limited by
shares). Kuna utata zaidi kwani kifungu cha 7(e) cha Katiba ya Tangold Ltd. kinaruhusu hisa za
wanaomiliki kampuni hiyo binafsi kuhamisha hisa zao kwa wanandoa, baba, mama, watoto, wajukuu au
wakwe zao wa kike au wa kiume! Sasa kama ni kweli kwamba Tangold Ltd. inamilikiwa na Serikali ya
Tanzania kwa asilimia mia moja, je nani ni mke au mume au baba au mama au motto au mjukuu au mkwe
wa kike au wa kiume wa Serikali ya Tanzania ambaye anaweza kuhamishiwa hisa za kampuni hiyo? Katika
barua yake ya ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alidai kwamba Ofisi yake ilishindwa kuelewa uhalali wa
malipo ya dola za Marekani 13,340,168.37 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Tangold Limited;
iv. Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia mkopo usio na riba wa Dola za
Marekani 5,512,398.55 kwa kampuni ya Mwananchi Gold Co. Ltd. kati ya mwaka 2004 na tarehe 30
Juni 2006. Kati ya fedha hizo, deni la dola 2,807,920 limedhaminiwa kwa dhahabu ghafi ambayo
ingenunuliwa kutokana na fedha za mkopo zilizotolewa na Benki Kuu yenyewe! Kwa maana rahisi
ni kwamba kampuni ya Mwananchi Gold haijatoa dhamana yoyote inayoeleweka kwa mabilioni ya
shilingi ilizokopeshwa na Benki Kuu chini ya Gavana Balali. Kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu, hadi kufikia mwezi Desemba 2006 Mwananchi Gold Co. Ltd. ilikuwa imeshindwa kulipa hata
riba ya mkopo huo kwa kiasi cha dola za Marekani 62,847.91. “Katika mazingira haya”, inasema
barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, “hatukuweza kujiridhisha kwamba deni la dola la Marekani
5512398.55 inalodaiwa (Mwananchi Gold Co. Ltd.) hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006 linaweza
kulipika.” Je, ni kampuni gani hii iliyopewa mamilioni ya fedha za umma katika fedha za kigeni bila
kudaiwa riba au kupewa kipindi maalumu cha kulipa mkopo huo? Kufuatana na taarifa za BRELA,
Mwananchi Gold Co. Ltd. ni kampuni binafsi ambayo wanahisa wake ni Benki Kuu ya Tanzania
yenye hisa 500, Shirika la Maendeleo la Taifa (hisa 500), Mwananchi Trust Co. Ltd. (hisa 1,123) na
Chimera Co. Ltd. (hisa 500). Kampuni hii ilisajiliwa kama kampuni binafsi tarehe 12 Desemba
2002. Mawakili wake ni kampuni ya mawakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Associates
ikiwashirikisha aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wakati huo marehemu Francis L. Nyalali, Waziri
Mkuu wa zamani Joseph Sinde Warioba na aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa
R. Mahalu. Wakurugenzi wa Mwananchi Gold ni Joseph Sinde Warioba, Gavana Daudi Balali, Col. J.
Simbakalia, Vulfrida Grace Mahalu, Yusuf H. Mushi na raia wawili wa Italia, Paolo Cesari na Patrizio
Magrini. Vulfrida Mahalu ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa kampuni binafsi ya VMB Holdings (1996) Ltd.
na pia ni mke wa Profesa Mahalu ambaye kwa sasa anakabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi
kutokana na madai ya wizi wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Serikali wakati akiwa balozi wa
Tanzania nchini Italia! Kanali Simbakalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Taifa
na Yusuf Mushi ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni binafsi ya Business Machines Consultants (T)
Ltd;
v. Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya shilingi 131,950,750,000
kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. Vile vile Gavana Balali
anadaiwa kuidhinisha malipo ya shilingi bilioni 4,228,658,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa
kuingiza fedha za kigeni nchini. “Katika mazingira haya”, inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, “hatukuridhika na uhalali wa hasara ya shillingi bilioni 131.9
zinazoonekana katika taarifa za fedha hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006….” Kwa mantiki hiyo,
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu aliiasa Benki Kuu kuanzisha uchunguzi wa malipo yaliyosababisha
hasara ya shilingi 131,950,750,000 na shilingi 4,228,658,000 zilizolipwa kama malipo ya madeni
ya nje. Waziri wa Fedha Zakia Meghji mwenyewe amekiri kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha
za umma katika akaunti za malipo ya madeni ya nje katika barua yake kwa Mkurugenzi wa Shirika
la Fedha la Kimataifa (IMF). IMF yenyewe katika taarifa kwa vyombo vya habari ya tarehe 27 Juni
2007 imetamka kwamba “Serikali (ya Tanzania) imekwisha kusimamisha malipo kutoka akaunti
hiyo hadi uchunguzi huo utakapokamilika.” Wakati Serikali ikitoa taarifa hizi kwa IMF imekataa
kata kata kutoa taarifa hizi kwa umma wa Watanzania wala wawakilishi wao Bungeni.

2. ANDREW J. CHENGE
Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa
Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu
katika Serikali ya sasa ya Rais Jakaya Mrisho
Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge
alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa
miaka yote kumi ya utawala wa Rais
Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo,
Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa “mshauri
wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya
mambo ya sheria na … aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria,
na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria….”[6] Katika kipindi hicho cha miaka
kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za
Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
• Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri
vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa
katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
• Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa
Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya
kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake
Bungeni tarehe 6 Novemba 2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe
alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu
yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo
yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la
mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika
kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega ulipofunguliwa hadi mwaka
huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.614
wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge
angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa
linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.

3. BASIL P. MRAMBA
Mheshimiwa Basil Mramba ni Mbunge wa
muda mrefu wa Jimbo la Rombo na Waziri wa
Viwanda na Biashara na kwa miaka kumi ya
utawala wa Rais Mkapa alikuwa ndiye Waziri
wa Fedha. Katika kipindi hicho cha miaka
kumi, Mheshimiwa Mramba amehujumu taifa
la Tanzania kama ifuatavyo:
i. Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers)
Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya
makampuni ya uchimbaji dhahabu. Chini ya mkataba wake na Serikali ya Tanzania, Kampuni hiyo inalipwa
asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya
dhahabu. Kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart
(Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi wa mahesabu ya makampuni ya
dhahabu, ijapokuwa “hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu ukaguzi uliofanywa
katika mwaka 2005/06”! Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alisema katika barua yake kwamba “hakuna
ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa
zabuni ya ushindani.”
ii.
Vile vile kuna taarifa za kuwepo kwa rushwa na/au ufisadi mkubwa kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex
Stewart Assayers. Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya
Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye jina la Bwana Basil ambaye ana wadhifa wa Waziri katika serikali ya
Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye
kampuni hiyo na kuwa analipwa na kampuni hiyo. Kwa mujibu wa Flores, hakuwezi kukawa na ushahidi wowote
kuthibitisha kwamba ‘Bwana Basil’ anapokea malipo kutoka kwa Alex Stewart kwa vile malipo yote kwake yamekuwa
yakifanyika nje ya nchi. Kwa kadri tunavyofahamu, mtu pekee aliyekuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Tatu na
ambaye pia ni waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na ambaye ana jina la ‘Basil’ ni Mheshimiwa Basil Pesambili
Mramba. Tumemtaka Waziri wa Fedha kutupatia nakala ya Mkataba kati ya Benki Kuu na Alex Stewart, na kuwataka
Mheshimiwa Basil Mramba na Erwin Flores walete maelezo yao kwetu kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka, Haki na Kinga
za Bunge ya mwaka 1988 kwa barua yetu ya tarehe 18 Julai 2007 ili waweze kujibu tuhuma hizi. Bado tunasubiri majibu
hayo.
i. Mheshimiwa Mramba amehusishwa pia na ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za umma na uuzaji holela
wa rasilmali za taifa letu. Kashfa hizo ni pamoja ni ununuzi wa rada ya kijeshi, ununuzi wa ndege ya Rais, na
ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na National Microfinance Bank (NMB).

4. GRAY S. MGONJA
Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku
nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni
Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na
anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika
kampuni ya kigeni ya Tangold Limited
ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana
na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na
Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake
kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,
Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile
Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa
mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa
wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.
. PATRICK W.R. RUTABANZIBWA
Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa
alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini wakati mikataba mibovu ya madini
inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea.
Kwa sasa Bwana Rutabanzibwa ni Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi
wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited.
Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina
katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna mgongano mkubwa kati maslahi yake
binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa
kuyalinda akiwa kama kiongozi wa umma

6. NIMROD ELIREHEMA MKONO
Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa
Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa
kampuni ya mawakili ya Mkono & Company
Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya
Serikali inaainisha kuwa Benki Kuu imekuwa
ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co.
Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya
Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla
ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya
wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates
wamekwishalipwa shilingi 8,128,375,237 kwa
fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia 13.5 ya deni lote
inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo
inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.
Lakini hoja nyingine ya kimsingi ni kama malipo haya kwa mawakili yanaruhusiwa chini ya Kanuni za Malipo ya Mawakili
na Uamuzi ya Gharama za Kesi za mwaka 1991, Tangazo la Serikali Na. 515 la mwaka 1991 (Advocates’ Remuneration
and Taxation of Costs Rules, 1991). Kanuni hizi zimeweka kiwango cha malipo ya mawakili katika kesi ambazo fedha
inayodaiwa ni zaidi ya Shilingi milioni 10 kuwa ni asilimia tatu. Kwa kufuata masharti ya sheria hii ya malipo ya
mawakili, kampuni ya Mkono & Co. Advocates ilipaswa kulipwa Shilingi bilioni 1.8.
Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au
ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni
ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G.
Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme’ iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi
Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: “Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako
tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba
yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De
Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA
AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)
Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: “Mheshimiwa Spika,
ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza
hapa haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli
za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art
(reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu
kinafichwa. Nimrod Mkono alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya
Marcus Ltd., makampuni ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya
utaratibu wa DCP.”

7. NAZIR KARAMAGI
keshafulia lakini hajaonja mahakama by 2011

8. ROSTAM AZZIZ
Huyu sasa ndie bosi wa DOWANS LTD... Keshatapeli saana kabakisha mapanki tuu by 2011 watu watadili nae

9. EDWARD LOWASSA
Tajiri wa RICHMOND ambaye atagombea uraisi 2015... Kazi tunayo

10. BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005
alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais
Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi
unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au
washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources
Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira
Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa
kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba
wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana
Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini
wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal
Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa
kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo
utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi
cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba.

11. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE(Mkuu wa kaya)
Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais,
Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha
1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na
Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya
madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha
wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa
madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu,
Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu
waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao
hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa
eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni
253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha
fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la
Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.
Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama
Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu
unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka
1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama
Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika
eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na
Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni
280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

source : Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
 
Kaka umekuna nadhani hii inatosha kumalizia yale mambo yetu ya Misri na Tunisia
 
Kwa maana halisi ya neno fisadi hata Dr. Slaa naye pia ni fisadi kwani amepora mke wa mtu. kwa maana hiyo basi:

12. DR. WILBROAD SLAA
Amepora mke wa mtu na amempa mimba
 
Wewe, Bwana, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele. Wasio haki hutembea pande zote, Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu. Zaburi 12:8
 
Kupambana na mafisadi kunahitaji Hekima na Busara ya hali ya juu, sivyo watatuchezea na gharama yetu wenyewe.
 
Kwa maana halisi ya neno fisadi hata Dr. Slaa naye pia ni fisadi kwani amepora mke wa mtu. kwa maana hiyo basi:

12. DR. WILBROAD SLAA
Amepora mke wa mtu na amempa mimba

GB mbona umenga'ng'ania sana kuwa amepora mke wa mtu? hebu tupe maana halisi ya neno PORA, maana nahisi unalitumia ambapo halikupaswa kutumiwa.
 
Vipi umegoma kushinikiza 10,000 au uwe na muda wa kuja hapa JF ulete upupu?
TUJIKUMBUSHE WAPORA WAKE ZA WATU 2010 nani umjuaye....
 
Hivi wewe umeshawahi kuishi uswahilini uone namna wanawake na watoto wanavyoteseka kwa umaskini?
wenzako tunamshukuru mungu amewezesha mawazo ya wtz kubadilika wewe unakasirika.Mbaya zaidi wewe ni University graduate ungekuwa na diploma nugekuwaje?

HAYA TUJIKUMBUSHE WALIOFIKUZWA UALIMU kwa sababu ya vibinti vya darasa la tatu
 
Vipi umegoma kushinikiza 10,000 au uwe na muda wa kuja hapa JF ulete upupu?
TUJIKUMBUSHE WAPORA WAKE ZA WATU 2010 nani umjuaye....

Hahaha naona hoja ya msingi imekukuna saaana ww.... hayo mengine baadae LETS GO BACK TO MAIN TOPIC
 
Na mpk sasa hakuna aliyechukuliwa hatua zaidi ya vijikesi vya uongo na kweli na kufungwa tumiaka tuchache kma liyumba
 
Ni ajabu sana hawa wajamaa pamoja na kashfa zote hizi bado wapo nje wanakula raha tu, na tena ni mawaziri na wabunge.

Ila 2015 tunawapeleka lupango...
 
Orodha ya Mafisadi (List of Shame)
KANUNI/ VIGEZO VILIVYOTUMIKA

A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
Katika kundi hili wamo viongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/au washirika wao katika sekta binafsi
ambao kwa namna mbali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/au fedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na
umma wa Watanzania ufukara na/au umaskini mkubwa.

B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI
Katika kundi hili wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa umma
wamefanya maamuzi ambayo kwayo taifa limepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake na kuwaneemesha raia na/
au taasisi za kiuchumi na/au za kibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa umma walioshiriki katika kusaini mikataba
mibovu katika sekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengine yenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na
jamii ya Watanzania.

MISINGI YA KISHERIA/KISIASA YA ORODHA YA MAFISADI
A. KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, 1977
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sura ya 2 ya Sheria za Tanzania imeweka Malengo Muhimu na
Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:[1]
a. Kwamba wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka
kwa wananchi.;
b. Kwamba lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi; na
c. Kwamba Serikali itawajibika kwa wananchi.
d. .
Katika kutekeleza malengo na misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali iliyotajwa, Mamlaka ya Nchi na vyombo
vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
a.
b. Kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;
c. Kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba wa Taifa unaendelezwa,
unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu
mwingine;
d. Kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
a.
b.
c.
d. Kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
e. Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa
kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;
f. Kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za
uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;
g. . [2]
Ibara ya 7(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeamuru kuwa Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote na
mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki,
watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii ya Katiba.
Katiba pia imewapa viongozi wa umma wajibu wa kufuata na kuitii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya
Muungano.[3] Aidha, viongozi wa umma wamepewa wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya
Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi.[4] Vile vile viongozi wote wa umma
watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi nay a pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na
ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa
lao.[5]
Licha ya masharti ya kikatiba yaliyotajwa hapo juu, viongozi wa umma waliotajwa katika Orodha hii ya Mafisadi
walikuwa wanabanwa na masharti ya sheria nyingine za nchi yetu kama ifuatavyo:

B. SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA, 1995
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga
maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani
ya Serikali na katika sekta ya umma. Katika kutekeleza wajibu wake, Rais anatakiwa kuweka taratibu thabiti za maadili
katika utumishi wa umma ambazo:
a. Zitahakikisha kwamba kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na
wajibu wake kama kiongozi wa umma;
b.
c. Zitaweka taratibu za wazi za maadili kuhusu migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wa kuchaguliwa na
wa kuteuliwa;
d. Zitapunguza uwezekano wa migongano inayotokana na maslahi binafsi kuingiliana na shughuli za umma za
viongozi wa umma na kuweka taratibu za utatuzi wa migongano hiyo inapotokea.
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa
umma:
a.
kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na
watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa
Serikali;
b. kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na
kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na
haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu;
c. kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa
maslahi ya umma;
d. kuhusiana na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa
na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya;
e. kuhusiana na maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma watapanga masuala
yao kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale
ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia
zaidi maslahi ya umma;
f. kuhusiana na zawadi, viongozi wa umma hawatadai au kupokea manufaa ya kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo
ndogo, ukarimu wa jadi/takrima au manufaa mengine yenye thamani ishara, isipokuwa tu kama manufaa hayo
yatatokana na mkataba au mali ya kiongozi wa umma;
g. kuhusiana na upendeleo, viongozi wa umma hawatatumia vyeo vyao rasmi katika kusaidia taasisi au watu
binafsi katika mahusiano yao na serikali iwapo kufanya hivyo kutasababisha upendeleo kwa mtu yeyote;
h.
i. Kuhusiana na mali ya serikali ambayo viongozi wa umma hawatatumia ama moja kwa moja ama kisiri siri, au
kuruhusu kutumiwa kwa mali ya serikali ya aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mali ya serikali iliyokodishwa kwa
ajili ya kumnufaisha kiongozi wa umma;
j. Kuhusiana na ajira baada ya utumishi wa umma, viongozi wa umma hawatafanya vitendo vitakavyoshusha
hadhi na heshima ya utumishi wa umma baada ya kuondoka katika utumishi ili kupunguza uwezekano wa
matarajio ya ajira kuleta migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wanapokuwa katika utumishi wa
umma; kupata upendeleo baada ya kuondoka katika utumishi wa umma; kutumia taarifa zinazopatikana
kutokana na utumishi wa umma kwa maslahi binafsi; na kutumia utumishi wa umma kwa ajili ya kupatia nafasi
za ajira nje ya utumishi wa umma.

VIONGOZI WA UMMA WALIOKO KATIKA ORODHA HII WAMEKIUKA NA/AU KUVUNJA MASHARTI YA

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO
A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI

1. DR. DAUDI T.S. BALALI
Dr. Daudi Balali amekuwa na bado ni
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
tangu mwaka 1997. Katika kipindi
hicho cha miaka kumi, Gavana Balali
amehujumu taifa la Tanzania kama
ifuatavyo:
i. Kufuatana na barua ya wataalamu wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali,
ameruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufikia
Shilingi 522, 459, 255,000 katika ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyoko barabara
ya Mirambo, Dar es Salaam na Gulioni, Zanzibar. Aidha taarifa kutoka vyanzo vingine zinaonyesha
kwamba mwaka 1998 kampuni ya Skanska Jensen ya Sweden ilituhumiwa kutoa hongo ya Dola za
Marekani milioni 5 kwa Gavana Balali tuhuma zilizopelekea kampuni hiyo kupigwa marufuku
kushiriki tenda ya ujenzi wa majengo hayo. Hata hivyo, katika mazingira yanayoashiria ufisadi
mkubwa, kampuni ya Group 5 ya Afrika ya Kusini ambayo ni kampuni tanzu ya Skanska Jensen
ilipewa tenda ya kujenga majengo hayo ya Benki Kuu;
ii. Kufuatana na barua iliyotajwa katika aya ya (i) hapo juu, Gavana Balali aliidhinisha na/au kuruhusu
na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 118,396,460.36 zilizopelekwa katika akaunti
isiyojulikana ya Benki ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini kama malipo ya madeni ya kampuni muflisi
ya Meremeta Ltd. iliyokuwa inachimba dhahabu katika eneo la Buhemba wilaya ya Musoma, Mkoa
wa Mara. Kwa miaka mingi Serikali ilikuwa ikitoa taarifa za uongo kwamba Meremeta Ltd. ilikuwa
ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili
ya mradi wake wa Nyumbu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Hata hivyo, nakala ya usajili iliyotolewa na
Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales inaonyesha kwamba kampuni hiyo iliandikishwa
nchini Uingereza tarehe 19 Agosti 1997 na ilifilisiwa huko huko Uingereza tarehe 10 Januari 2006.
Aidha, taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ya tarehe 31 Mei 2005
inaonyesha kwamba Meremeta Ltd. ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania kama tawi
tarehe 3 Oktoba, 1997. Vile vile taarifa hiyo inaonyesha kwamba hisa 50 za Meremeta Ltd.
zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini na hisa 50 zilizobaki
zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa kupitia kwa Msajili wa Hazina katika Wizara ya
Fedha. Inajulikana vile vile kwamba Gavana Balali aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Meremeta Ltd. kati ya mwaka 2004 na 2005. Hata hivyo, kuna utata mkubwa juu
ya nani ni mmiliki hasa wa Meremeta Ltd. kwa kuwa taarifa ya BRELA inaonyesha pia kwamba
makampuni mawili ya Kiingereza London Law Services Ltd. na London Law Secretarial Ltd. nayo
yanamiliki hisa moja moja za Meremeta Ltd. Makampuni hayo yanatumia anwani moja iliyoko 84
Temple Chambers, Temple Avenue, jijini London. Haijulikani ni kwanini Gavana Balali aliruhusu
fedha za umma kutumika kulipia madeni yote ya kampuni ambayo Serikali ilikuwa inamiliki hisa 50
tu wakati makampuni mengine ya kigeni yalikuwa yanamiliki hisa 52. Na kama ilivyosema barua ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, uhalali wa Serikali kulipa madeni ya Meremeta Ltd. kwa Nedbank Ltd.
badala ya kuiacha benki hiyo kudai malipo hayo kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na
wadeni wengine haujulikani;
iii.
Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu, Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au
kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kampuni ya Tangold Ltd. Katika hotuba yake
Bungeni ya tarehe 27 Juni 2007, Waziri wa Madini na Nishati Mheshimiwa Nazir Karamagi alidai kwamba
mali na madeni ya MEREMETA yamehamishiwa kwenye kampuni mpya ya TANGOLD ambayo
inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja. Hata hivyo, barua ya BRELA ya tarehe 4 Julai 2007
inatamka wazi kwamba Tangold Limited ni kampuni ya kigeni iliyosajiliwa kwa mara ya kwanza nchini
Jamhuri ya Mauritius, na baadae kuandikishwa nchini Tanzania kama tawi la kampuni ya kigeni. Barua
hiyo inaongeza kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania mnamo tarehe 20
Februari 2006 na kwamba Katiba ya kampuni hiyo haikuonyesha majina ya wanahisa wa kampuni na
mgawanyo wa hisa. Barua hiyo ya BRELA inaonyesha kwamba wakurugenzi wa Tangold Limited ni pamoja
na Gavana Balali, Gray S. Mgonja ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Andrew J. Chenge ambaye ni
Waziri wa sasa wa Miundo Mbinu, Patrick W.R. Rutabanzibwa ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Vincent F. Mrisho ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha fomu Na. 1F inayohusu usajili wa
kampuni za kigeni iliyowasilishwa BRELA na mawakili wa Tangold Limited na kusainiwa na Gavana Balali
tarehe 20 Mei 2005 inaonyesha kwamba kampuni hii imetokea Jamhuri ya Mauritius na anwani yake iko
Suite 520, Barkly Wharf, Le Caudan, Waterfront, Port Louis, Mauritius. Hivyo ndivyo kinavyoonyesha cheti
cha usajili kilichotolewa na Msajili wa Makampuni wa Jamhuri ya Mauritius mnamo tarehe 5 Aprili 2005 na
pia leseni ya biashara iliyotolewa kwa Tangold Ltd. Port Louis nchini Mauritius tarehe 8 Aprili 2005.
nyaraka hizi pia zinaonyesha kwamba Tangold Limited ni kampuni binafsi (private company limited by
shares). Kuna utata zaidi kwani kifungu cha 7(e) cha Katiba ya Tangold Ltd. kinaruhusu hisa za
wanaomiliki kampuni hiyo binafsi kuhamisha hisa zao kwa wanandoa, baba, mama, watoto, wajukuu au
wakwe zao wa kike au wa kiume! Sasa kama ni kweli kwamba Tangold Ltd. inamilikiwa na Serikali ya
Tanzania kwa asilimia mia moja, je nani ni mke au mume au baba au mama au motto au mjukuu au mkwe
wa kike au wa kiume wa Serikali ya Tanzania ambaye anaweza kuhamishiwa hisa za kampuni hiyo? Katika
barua yake ya ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alidai kwamba Ofisi yake ilishindwa kuelewa uhalali wa
malipo ya dola za Marekani 13,340,168.37 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Tangold Limited;
iv. Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia mkopo usio na riba wa Dola za
Marekani 5,512,398.55 kwa kampuni ya Mwananchi Gold Co. Ltd. kati ya mwaka 2004 na tarehe 30
Juni 2006. Kati ya fedha hizo, deni la dola 2,807,920 limedhaminiwa kwa dhahabu ghafi ambayo
ingenunuliwa kutokana na fedha za mkopo zilizotolewa na Benki Kuu yenyewe! Kwa maana rahisi
ni kwamba kampuni ya Mwananchi Gold haijatoa dhamana yoyote inayoeleweka kwa mabilioni ya
shilingi ilizokopeshwa na Benki Kuu chini ya Gavana Balali. Kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu, hadi kufikia mwezi Desemba 2006 Mwananchi Gold Co. Ltd. ilikuwa imeshindwa kulipa hata
riba ya mkopo huo kwa kiasi cha dola za Marekani 62,847.91. Katika mazingira haya, inasema
barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, hatukuweza kujiridhisha kwamba deni la dola la Marekani
5512398.55 inalodaiwa (Mwananchi Gold Co. Ltd.) hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006 linaweza
kulipika. Je, ni kampuni gani hii iliyopewa mamilioni ya fedha za umma katika fedha za kigeni bila
kudaiwa riba au kupewa kipindi maalumu cha kulipa mkopo huo? Kufuatana na taarifa za BRELA,
Mwananchi Gold Co. Ltd. ni kampuni binafsi ambayo wanahisa wake ni Benki Kuu ya Tanzania
yenye hisa 500, Shirika la Maendeleo la Taifa (hisa 500), Mwananchi Trust Co. Ltd. (hisa 1,123) na
Chimera Co. Ltd. (hisa 500). Kampuni hii ilisajiliwa kama kampuni binafsi tarehe 12 Desemba
2002. Mawakili wake ni kampuni ya mawakili ya Nyalali, Warioba & Mahalu Associates
ikiwashirikisha aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wakati huo marehemu Francis L. Nyalali, Waziri
Mkuu wa zamani Joseph Sinde Warioba na aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa
R. Mahalu. Wakurugenzi wa Mwananchi Gold ni Joseph Sinde Warioba, Gavana Daudi Balali, Col. J.
Simbakalia, Vulfrida Grace Mahalu, Yusuf H. Mushi na raia wawili wa Italia, Paolo Cesari na Patrizio
Magrini. Vulfrida Mahalu ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa kampuni binafsi ya VMB Holdings (1996) Ltd.
na pia ni mke wa Profesa Mahalu ambaye kwa sasa anakabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi
kutokana na madai ya wizi wa zaidi ya shilingi bilioni tatu za Serikali wakati akiwa balozi wa
Tanzania nchini Italia! Kanali Simbakalia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Taifa
na Yusuf Mushi ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni binafsi ya Business Machines Consultants (T)
Ltd;
v. Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya shilingi 131,950,750,000
kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini. Vile vile Gavana Balali
anadaiwa kuidhinisha malipo ya shilingi bilioni 4,228,658,000 kwa watu wasiojulikana wanaodaiwa
kuingiza fedha za kigeni nchini. Katika mazingira haya, inasema barua ya Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Mahesabu ya Serikali, hatukuridhika na uhalali wa hasara ya shillingi bilioni 131.9
zinazoonekana katika taarifa za fedha hadi kufikia tarehe 30 Juni 2006. Kwa mantiki hiyo,
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu aliiasa Benki Kuu kuanzisha uchunguzi wa malipo yaliyosababisha
hasara ya shilingi 131,950,750,000 na shilingi 4,228,658,000 zilizolipwa kama malipo ya madeni
ya nje. Waziri wa Fedha Zakia Meghji mwenyewe amekiri kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha
za umma katika akaunti za malipo ya madeni ya nje katika barua yake kwa Mkurugenzi wa Shirika
la Fedha la Kimataifa (IMF). IMF yenyewe katika taarifa kwa vyombo vya habari ya tarehe 27 Juni
2007 imetamka kwamba Serikali (ya Tanzania) imekwisha kusimamisha malipo kutoka akaunti
hiyo hadi uchunguzi huo utakapokamilika. Wakati Serikali ikitoa taarifa hizi kwa IMF imekataa
kata kata kutoa taarifa hizi kwa umma wa Watanzania wala wawakilishi wao Bungeni.

2. ANDREW J. CHENGE
Mheshimiwa Andrew Chenge ni Mbunge wa
Bariadi Magharibi na Waziri wa Miundombinu
katika Serikali ya sasa ya Rais Jakaya Mrisho
Kikwete. Kabla ya hapo, Mheshimiwa Chenge
alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa
miaka yote kumi ya utawala wa Rais
Benjamin W. Mkapa. Kwa wadhifa huo,
Mheshimiwa Chenge ndiye alikuwa mshauri
wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya
mambo ya sheria na aliwajibika kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria,
na kutekeleza shughuli nyinginezo zozote zenye asili ya au kuhusiana na sheria.[6] Katika kipindi hicho cha miaka
kumi na mbili, Mheshimiwa Chenge amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:
Kama Mkurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited alishiriki na/au kufaidika na malipo haramu ya dola za
Marekani 13,736,628.73 ambazo zimeelezewa kwa kirefu katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri
vizuri Benki Kuu ya Tanzania na kusababisha ufujaji wa mabilioni ya fedha za umma ambayo yameelezewa
katika sehemu inayomhusu Gavana Balali;
Kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Chenge ameshiriki moja kwa moja katika kutoa ushauri kwa
Serikali na/au Wizara ya Nishati na Madini kuingia mikataba mibovu na makampuni mbali mbali ya madini ya
kimataifa ambayo kwayo taifa limepoteza mabilioni ya fedha za kigeni. Kwa mfano, katika hotuba yake
Bungeni tarehe 6 Novemba 2006, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Bernard Membe
alitoa taarifa kwamba katika kipindi cha miaka mitatu hadi kufikia 2006, makampuni ya uchimbaji dhahabu
yaliyoko Tanzania yaliuza dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 2,340 wakati ambapo makampuni hayo
yalilipa mrahaba na kodi nyinginezo kwa Serikali za shilingi bilioni 72. Katika kikao cha Bunge la Bajeti la
mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja aliliambia Bunge kwamba katika
kipindi cha kuanzia mwaka 1998 Mgodi wa kwanza wa dhahabu wa Lusu Nzega ulipofunguliwa hadi mwaka
huu, makampuni ya uchimbaji dhahabu yaliuza nje dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.614
wakati Serikali ikiambulia mrahaba wa dola milioni 78 tu! Endapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Chenge
angeishauri vema Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama alivyotakiwa na Katiba ya nchi yetu, taifa lisingekuwa
linapoteza utajiri wake wa madini kwa kiasi kikubwa namna hii.

3. BASIL P. MRAMBA
Mheshimiwa Basil Mramba ni Mbunge wa
muda mrefu wa Jimbo la Rombo na Waziri wa
Viwanda na Biashara na kwa miaka kumi ya
utawala wa Rais Mkapa alikuwa ndiye Waziri
wa Fedha. Katika kipindi hicho cha miaka
kumi, Mheshimiwa Mramba amehujumu taifa
la Tanzania kama ifuatavyo:
i. Kwa kutumia wadhifa wake kama Waziri wa Fedha, alishinikiza kampuni ya Alex Stewart (Assayers)
Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani kupewa kazi ya kukagua mahesabu ya
makampuni ya uchimbaji dhahabu. Chini ya mkataba wake na Serikali ya Tanzania, Kampuni hiyo inalipwa
asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya
dhahabu. Kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart
(Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi wa mahesabu ya makampuni ya
dhahabu, ijapokuwa hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu ukaguzi uliofanywa
katika mwaka 2005/06! Vile vile Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alisema katika barua yake kwamba hakuna
ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa
zabuni ya ushindani.
ii.
Vile vile kuna taarifa za kuwepo kwa rushwa na/au ufisadi mkubwa kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex
Stewart Assayers. Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya
Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye jina la Bwana Basil ambaye ana wadhifa wa Waziri katika serikali ya
Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye
kampuni hiyo na kuwa analipwa na kampuni hiyo. Kwa mujibu wa Flores, hakuwezi kukawa na ushahidi wowote
kuthibitisha kwamba Bwana Basil anapokea malipo kutoka kwa Alex Stewart kwa vile malipo yote kwake yamekuwa
yakifanyika nje ya nchi. Kwa kadri tunavyofahamu, mtu pekee aliyekuwa waziri katika serikali ya Awamu ya Tatu na
ambaye pia ni waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne na ambaye ana jina la Basil ni Mheshimiwa Basil Pesambili
Mramba. Tumemtaka Waziri wa Fedha kutupatia nakala ya Mkataba kati ya Benki Kuu na Alex Stewart, na kuwataka
Mheshimiwa Basil Mramba na Erwin Flores walete maelezo yao kwetu kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka, Haki na Kinga
za Bunge ya mwaka 1988 kwa barua yetu ya tarehe 18 Julai 2007 ili waweze kujibu tuhuma hizi. Bado tunasubiri majibu
hayo.
i. Mheshimiwa Mramba amehusishwa pia na ufujaji na/au matumizi mabaya ya fedha za umma na uuzaji holela
wa rasilmali za taifa letu. Kashfa hizo ni pamoja ni ununuzi wa rada ya kijeshi, ununuzi wa ndege ya Rais, na
ubinafsishaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na National Microfinance Bank (NMB).

4. GRAY S. MGONJA
Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku
nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni
Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na
anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika
kampuni ya kigeni ya Tangold Limited
ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana
na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na
Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake
kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,
Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile
Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa
mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa
wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.
. PATRICK W.R. RUTABANZIBWA
Kwa miaka mingi Patrick Rutabanzibwa
alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini wakati mikataba mibovu ya madini
inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea.
Kwa sasa Bwana Rutabanzibwa ni Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi
wa kampuni ya kigeni ya Tangold Limited.
Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina
katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna mgongano mkubwa kati maslahi yake
binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa
kuyalinda akiwa kama kiongozi wa umma

6. NIMROD ELIREHEMA MKONO
Mheshimiwa Nimrod E. Mkono ni Mbunge wa
Jimbo la Musoma Vijiji na Mshiriki Mkuu wa
kampuni ya mawakili ya Mkono & Company
Advocates ya Dar es Salaam. Barua ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya
Serikali inaainisha kuwa Benki Kuu imekuwa
ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co.
Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya
Valambhia ambapo Benki Kuu inadaiwa jumla
ya shilingi bilioni 60. Kwa mujibu wa barua ya
wakaguzi tayari Mkono & Co. Advocates
wamekwishalipwa shilingi 8,128,375,237 kwa
fedha taslimu kwa kesi hiyo ambayo bado iko mahakamani. Malipo haya ni sawa na asilimia 13.5 ya deni lote
inalodaiwa Benki Kuu. Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo
inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.
Lakini hoja nyingine ya kimsingi ni kama malipo haya kwa mawakili yanaruhusiwa chini ya Kanuni za Malipo ya Mawakili
na Uamuzi ya Gharama za Kesi za mwaka 1991, Tangazo la Serikali Na. 515 la mwaka 1991 (Advocates Remuneration
and Taxation of Costs Rules, 1991). Kanuni hizi zimeweka kiwango cha malipo ya mawakili katika kesi ambazo fedha
inayodaiwa ni zaidi ya Shilingi milioni 10 kuwa ni asilimia tatu. Kwa kufuata masharti ya sheria hii ya malipo ya
mawakili, kampuni ya Mkono & Co. Advocates ilipaswa kulipwa Shilingi bilioni 1.8.
Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au
ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni
ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G.
Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi
Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako
tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba
yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De
Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA
AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)
Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: Mheshimiwa Spika,
ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza
hapa haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli
za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art
(reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu
kinafichwa. Nimrod Mkono alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya
Marcus Ltd., makampuni ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya
utaratibu wa DCP.

7. NAZIR KARAMAGI
keshafulia lakini hajaonja mahakama by 2011

8. ROSTAM AZZIZ
Huyu sasa ndie bosi wa DOWANS LTD... Keshatapeli saana kabakisha mapanki tuu by 2011 watu watadili nae

9. EDWARD LOWASSA
Tajiri wa RICHMOND ambaye atagombea uraisi 2015... Kazi tunayo

10. BENJAMIN WILLIAM MKAPA
Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005
alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais
Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi
unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au
washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources
Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira
Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa
kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba
wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana
Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini
wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal
Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa
kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo
utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi
cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba.

11. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE(Mkuu wa kaya)
Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais,
Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha
1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na
Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya
madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha
wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa
madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu,
Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu
waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao
hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa
eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni
253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha
fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la
Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.
Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama
Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu
unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka
1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama
Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika
eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na
Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni
280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

source : Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
jf
 
Huyo babu naye njaa; ukitoa number 9 hao wengine wote wapo CCM na amejiuinga nao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom