Tujikumbushie MOVIES za zamani za KIZUNGU!

Bonge la movie linaitwa No Retreat No Surrender,akina Michael Didcoof,Sugar Suge,usipime! ilikuwepo ile nyingine ya Alex akiwa mjeshi na Vandame mateka wanatupwa kwenye bwawa la mamba...enzi hizo kabla ya movie inaanza miziki ya akina Loketo,Mabere,marehemu Pepe Kalee,mitaa ya majengo shy town....za bongo sijuhi zina creativity gani?

No retreat No surrender naipenda kweli!!

Ngoja nitafute muda wa kuangalia movie za zamani tu!!
 
No retreat No surrender naipenda kweli!!

Ngoja nitafute muda wa kuangalia movie za zamani tu!!
Mwaka 1996, nilipokuwa Poland jijini Warsaw [Warszawa tamka varˈʂava], kulikuwa na jumba moja la sinema, wao wanaonyesha movies za zamani tu, yaani classic movies tu. Nadhani na bongo wangefanya kitu kam hicho japo kwa wiki mara mbili.
 
Wakuu, naomba msaada wenu, kuna movie flani hivi miaka ya nyuma jamaa alikuwa ana act amevaa kipensi hadi tuka muita komandoo Kipensi, alikuwa anatumia michale sana kwenye muvi yake moja hivi.... Kwa mdau yoyote atakayeweza kunitajia jina la huyo actor na jina la hiyo movie yake tafadhali.
 
Filam inaitwa Predator ni filam ya mwaka 1987.
 
Dah! Yale Mamovies ya kina Chuck Noris, Jet Lee, Anold, ect nikiyakumbuka waga yananikumbushaga mbali saana!
Enzi hizo tulikuwa tunazamia katika mabanda ya kuonesha hzo movies. Tulikuwa tunayaita 'Mbavu za Mbwa' unalipia kihamsini chako unachoma ndani!
Wale wezangu na mimi ukikodisha hizo VHS kwa Video Library, Baba au Mama anakugombeza kinyama eti utachafua deki na hizo VHS zako, kwa hiyo wazaz wengi walikua wana nunua sana hizo kanda na ndani huwezi ukakosa ile ''HEAD CLEANER"(kwa wanaouzikumbuka)
Na kwa zile kanda zilikuwa zimetafsiriwa kwa kiswahili zilijaa uwongo mtupu. aisee wale walokuwa wanatafsiri(majina yao yamenitoka) walitupotosha sana!
Muvi kama Delta Force, The Bodyguard, Seven Kids zilitamba sana...ebu nawewe nikumbushe mamovies mengine yalofunika
Hapo kwenye RED...Mmoja alikuwa anajiita '''Profesa Mkandala''
ahahahahhaah umenikumbusha mbali sana mkuu...
 
kuna muvi moja ya kichina miaka ya 80 mwanzoni tulikua tunaiona kwenye ma-bar ya Wang U "miruzi". Kuna anayejua jina lake?
 
KITU ENTER THE DRAGON CHA BRUCE LEE,DAAAAA! enter-the-dragon.jpg :lock1:
 
kuna muvi moja ya kichina miaka ya 80 mwanzoni tulikua tunaiona kwenye ma-bar ya Wang U "miruzi". Kuna anayejua jina lake?
Alikuwa anaitwa Jimmy Wang Yu, Nadhani hiyo filam kama si One Armed Boxer basi itakuwa Chinese Boxer.
 
Kwa wale walio wahi kuishi mbarali 1986-1992.Kulikuwa na ukumbi wa wellfare tuliuita(orofea).Tulikuwa tukitizama movies kama.John comando,no retreat no surrender,manila tuday,check noris,five comandos,The vietinam war e.t.c..Pia kulikuwa na nyimbo kama JIM JIM JIM ACHE NA CHE NA CHE,YVONE CHAKACHAKA,MBILIABELL. e t all.Usinikumbushe kwa wakazi wa UBARUKU tulivyo pambana na sungu sungu wakati wa kurudi nyumbani.Dah ilikuwa kali Wilaya nzima kulikuwa na video sizaidi ya tatu.Tumetoka mbali.
 
Ah ah ah ah, sisi wengine tulianza kuangalia filam za Chale Mnene (Chale Mbwambwa) na Chale Mwembamba (Laurel and Hardy) pia filam za Charles Chaplin, pale Kigamboni, Kanisa la Bikira Maria Consolata...!
 
Kuna muvi moja ya Michael Jackson nilikuwa naiogopa sana nilipokuwa mdogo inafahamika kwa jina la "The Thriller" miaka ya themanini huko, aisee kila nikiona sura inayobadilika ya Michael nilikuwa naificha uso wangu kwenye migongo ya watu hahahaha! Those days bana ilikuwa burudani haswaa!
Alaf kuna muvi hizi zilikuwa kali kinoma "Escape from Sobibor" na nyingine "One Way". Hii One way,nilimwonea huruma sana yule mweusi aliyekatwa mguu na mamba akawa hawezi tena kuendelea na safari na alikuwa na wenzake wawili makomandoo,jamaa alipigwa shaba na mkuu wa kikosi cha maadui maana alishambulia bila mpangilio,duh hii sinema kai aisee!
 
Pale Bukoba opposite na central police ulikuwepo ukumbi unaitwa NULITE CINEMA, ukilikiwa na mhindi mmoja anaitwa Mheta. Movie ya saa mbili na nusu usiku inaitwa cinema ya 'mid night'
 
Back
Top Bottom